Serikali: Suala la Kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari si la Serikali pekee

Serikali: Suala la Kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari si la Serikali pekee

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mei 3 ni siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambapo serikali ya Tanzania imesema inawahakikishia kulinda Uhuru wa Vyombo vya Habari.

Hata hivyo serikali imesisitiza jukumu la kuweka maslahi ya Taifa mbele kama ambavyo tasnia nyingine zimekuwa zikifanya.

Aidha wamesema Jukumu la kulinda uhuru wa Vyombo vya Habari sio la serikali pekee bali pia wadau wote.

Siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari inafanyika Arusha Kitaifa ambapo mgeni rasmi ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa.

IMG_20210502_175923_373.jpg
 
Unafiki na Uzandiki ndio unauwa vyombo vya habari.

wanahabari mnapaswa kutoa taarifa ya kweli na ya haki ambayo imejitosheleza,
wanahabari acheni unafiki msikubali kuwa vibaraka, bila kusahau kuwa wazalendo kwa Taifa lenu.

Bado kuna changamoto ya kutokuwa na Uzalendo kwa baadhi ya wanahabari.

Awamu ya 6 imetoa uhuru wa kukosolewa na kuibua ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma ktk serikali kwa masilahi ya umma.
 
Back
Top Bottom