Serikali subirini Bodi ya ligi ijiuzulu kwanza dabi itachezwa

Serikali subirini Bodi ya ligi ijiuzulu kwanza dabi itachezwa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Mpira unaendeshwa kwa kanuni, kama anaesimamia kanuni hizo ameshindwa kusimamia anapaswa kujiuzulu kwanza kabla kitu kikubwa kama wizara kufanya kitu kilekile walichoshindwa bodi ya ligi kukifanya. Serikali isaidie kutupatia mazingira sahihi ya kucheza mpira lakini sio namna ya kuucheza mpira. Tuliwapa mamlaka ya kusimamia namna ya kuucheza mpira wapo lakini wameshindwa kuaidia dabi ichezwe. Na bahati mbaya sana bodi ya ligi inalalamikiwa sio tu kuvuga dabi lakini hata kwa mabo mengine ya mpira. Hili la dabi ni ushahidi tu kuwa bodi ya ligi/TFF wamelalia upende (inclined).

SERIKALI kuendelea kutoa maelekezo ya namna gani mpira uchezwe sio sawa kwasababu inatengeneza kitu kinachoitwa vicious cycle, positive feedback, mwangwi, presidency, kudekeza, kulea uzembe. Watanzania hawataupenda mpira kwa wingi kama serikali inaingiza busara au kutishia watu kwenye mpira. Watu hawatatoka mbali kuja Dar es Salaam/Tanzania kuja kutizama dabi wakati hawana uhakika kama itachezwa au la, itakuwepo au la.

Tujuavyo sisi kunguru hana kibiongo, ukiona kibiongo kainama, na akiinama anaokota kitu, hivyo lazima awahiwe kabla hajaruka nacho maana anaweza kuruka ni kitu usichopenda aruke nacho kama vile kifaranga, chupi, au bangili ya dhahabu. Kwavyovyote vile Simba/Bodi ya ligi hawawezi kuahirisha dabi masaa 3 kabla ya mchezo kuchezwa, lazima kulikuwa na nguvu imara iliyotumika kuuahirisha mchezo. kama serikali inajiingiza kwenye kutatua mgogoro huu wa dabi haitakuwa jambo zuri kuwazuia baadhi ya wadau kuamini kuwa kigogo (serikalini) alihusika, alitumika, alifanikisha kuahilishwa dabi.
 
Naona madai ya pwenti 3 na magoli matatu za mezani yameyeyuka, mmebaki na bodi ijiuzulu sijui kigogo amehusika.

Yaani ni vilio tu huko utopoloni na hapo mmefinywa tu.
 
Back
Top Bottom