The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Serikali kupitia ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa - TAMISEMI (Afya) imeahidi kuchangia zaidi ya Milioni 600 hadi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya cha Ukumbi kilichopo Kata ya Ukumbi Wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa.
Ahadi hii imetolewa na Naibu Waziri wa ofisi hiyo Dkt. Festo Dugange katika ziara yake ya kikazi Wilaya ya Kilolo baada ya kusomewa Risala iliyo jaa adhaa wanazopitia wananchi hao kwa kutokukalilika kwa Kituo hicho cha Afya.
Soma pia: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kata hiyo ya Ukumbi haina kituo cha Afya, ina Zahanati moja pekee inayohudumia wananchi wa vijiji vyote vitano vya kata hiyo Kijiji cha Mawambala, Kitowo, Masalali, Winome na Ukumbi yenyewe hali inayohatarisha Afya ya Wananchi hao.
Baadhi ya wananchi kijijini hapo wameeleza adha wanazopitia kwa kutokamilika kwa Kituo hicho cha Afya kilicho anza kujengwa kwa nguvu ya wananchi tangu Mwaka 2011 na kughalimu zaidi ya milioni 45.
"Tunatembea zaidi ya Kilometa 60 kufuata kituo cha Afya jirani muda mwingine tunajifingua njiani, tunapoteza ndugu zetu hata usafiri ni gharama zaidi hasa kipindi cha mvua ambacho barabara hazipitiki kabisa" Alishuhudia