Serikali tatu haiepukiki...

Serikali tatu haiepukiki...

B.G TANTAWI

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
495
Reaction score
379
Sasa ni wazi kuwa Muundo wa serikali tatu hauepukiki kwa nini?

Tanzania bara siyo Nchi na wala siyo jina lake, Jina halisi ni Tanganyika, kwa vyovyote vile hatuna katiba yetu sisi kama watu wa bara au watanganyika, tunatumia katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo ni Muungano wa nchi Mbili za ZANZIBAR NA TANGANYIKA, lakini cha kushangaza Zanzibar wana Katiba yao, Tanganyika hatuna katiba yetu. Well, ikiwa Rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya sasa itabadilishwa katika kipengele cha Serikali tatu kama inavyopendekezwa na Chama cha mapinduzi na baadhi ya watendaji serikalini italeta matatizo, yapi hayo?

Kutakuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, katiba ya zanzibar na Katiba ya Tanganyika.

Kumbuka kuwa Zanzibar wana katiba yao Tayari Inasimamiwa na kutekelezwa na Serikali Huru ya ZANZIBAR,

Tanganyika hatuna katiba yetu na hivyo ndo tunapigania mchakato uanze wa kuiandika, ikiwa tutakuwa nayo ni dhahiri kuwa itasimamiwa na kutekelezwa na Serikali huru ya Tanganyika.

Je! Katiba ya Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Itasimamiwa na kutekelezwa na nani?

Ijulikane wazi wazi kwamba "SAA YA UKOMBOZI NI SASA" Alijisemea Mchg. Mtikila, Nae Nyerere enzi zake aliwhi kusema, "Tumeonewa kiasi cha kutosha, Tumedhalilishwa kiasi cha kutosha na Tumenyanyaswa kiasi cha kutosha" Wapendwa enzi za kuendelea na unyonge huo zimepita, tuwashukuru CHADEMA kwa kuwa na sera hii kwenye Ilani yao, na Kipekee tuwashukuru CCM kwa kuamua kuwa wanatekeleza sera za CHADEMA. Sasa ujasiri wanautoa wapi wa kuturudisha tena nyuma eti serikali mbili? Ujasiri wa kuanza kutumia kauli na sera za Nyerere sasa wakati ni CCM hii hii tena Nyerere akiwa hai waaliamua kuliua na kulizika Azimio la Arusha kule katikati ya Bahari kama alivyozikwa Osama, sasa watujie na mbinu eti serikali mbili,

WAACHANE NA SISI TUSHA AMAKA, UKIMWAMSHA ALIYE LALA UTALALA WEWE.
 
Sasa ni wazi kuwa Muundo wa serikali tatu hauepukiki kwa nini?

Tanzania bara siyo Nchi na wala siyo jina lake, Jina halisi ni Tanganyika, kwa vyovyote vile hatuna katiba yetu sisi kama watu wa bara au watanganyika, tunatumia katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo ni Muungano wa nchi Mbili za ZANZIBAR NA TANGANYIKA, lakini cha kushangaza Zanzibar wana Katiba yao, Tanganyika hatuna katiba yetu. Well, ikiwa Rasimu ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya sasa itabadilishwa katika kipengele cha Serikali tatu kama inavyopendekezwa na Chama cha mapinduzi na baadhi ya watendaji serikalini italeta matatizo, yapi hayo?

Kutakuwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano, katiba ya zanzibar na Katiba ya Tanganyika.

Kumbuka kuwa Zanzibar wana katiba yao Tayari Inasimamiwa na kutekelezwa na Serikali Huru ya ZANZIBAR,

Tanganyika hatuna katiba yetu na hivyo ndo tunapigania mchakato uanze wa kuiandika, ikiwa tutakuwa nayo ni dhahiri kuwa itasimamiwa na kutekelezwa na Serikali huru ya Tanganyika.

Je! Katiba ya Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Itasimamiwa na kutekelezwa na nani?

Mbona hueleweki? swali lako hapo mwishoni naona kama una maana kuwa tutakuwa na serikali 2 na siyo tatu. Nini msimamo wako kwenye mada yako?
 
Angalau wadanganyika mnaanza kujitambua.
 
Ndugu wana JF, Ndugu wana JF, bila shaka mtakumbuka tambo za Katibu Itikadi na uenezi (CCM) kwamba wameteka mabaraza ya katiba kwa 90% upande wa Tanzania bara.

Lakini pia mtakumbuka malalamiko ya Nape wiki iliyopita akidai, "Warioba haitendei haki CCM" kisa kupendekeza muungano wa mfumo wa shirikisho wenye serikali tatu.

Turudi 2010, CCM walikuwa wapi kuingilia kati mabadiliko ya katiba iliyoitaja Zanzibar kuwa nchi? Kama waliona sawa, kwanini hawataki nchi iliyoungana na Zanzibar ionekane kwa sifa na mfumo, kuna siri gani? Tume ya mabadiliko ya katiba imetaja mambo 7 badala ya 22 yaliyopo sasa yaani Katiba na Mamlaka ya JMT, Ulinzi na usalama wa JMT, Uraia na Uhamiaji,Sarafu na Benki Kuu,Mambo ya Nje,Usajili wa vyama vya siasa na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.

HOJA;Upande wa Zanzibar, mambo yasiyo ya muungano yatatekelezwa na SMZ, je upande wa Tanganyika yatatekelezwa na nani?
 
Nakuunga mkono kwenye baadhi ya hoja, badala ya kutumia fedha kuhonga waandishi na kuwashawishi wananchi ni vema wakazitolea maelezo hoja hizi zilizopelekea kuwepo kinachoitwa kero za muungano.Ni kwani CCM hawataki serikali inayoshughulia masuala yasiyo ya muungano kwa upande wa bara iwepo?
 
Raga; Hapo ndipo pana hoja na siyo ngonjera za 1+1=2 au kwamba watu wakioana sharti wakae nyumba moja kwani muungano hauna mahusiano na hoja hizo dhaifu.Imekuwa bahati mbaya matukio yanatokea wakati ambapo watu hawataki kusumbua vichwa kusoma,kutafiti na kujadili hoja za msingi nje ya majungu ya kisiasa. Mfano, Ibara ya 1 na 2 za katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka kwamba (1) Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano. Ibara ya 2 (1) inasema, "eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania bara (Tanganyika) na eneo lote la Tanzania visiwani (Zanzibar) na ni pamoja na sehemu yote ya bahari ambayo Tanzania inapakana nayo". Kwa mujibu wa Katiba ya sasa ya JMT, Tanganyika na Zanzibar si nchi bali ni sehemu ya nchi moja inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ilitambua hilo lakini katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 inatamka kwamba ZANZIBAR NI NCHI, Dhana ya JMT kuwa nchi moja iko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Serikali tatu inaweza isiwe gharama kama walivyoeleza watu waliotangulia.
Tunaweza tukaunda serikali tatu ambazo zikawa na gharama ndogo kuliko serikali hizi mbili tulizonazo.

Mfano mmoja;
Tanzania nzima ina wabunge 357, kati ya hao 239 ni wa kuchaguliwa kutoka kwenye majimbo (57 Znz na 182 Bara). Na kwa upande wa Znz pia kuna ziada ya wawakilishi takriban 57, hawa ni wale wa baraza la wawakilishi Znz. Hizo zote ni gharama, na sio ndogo. Znz wanakuwa kama wana wabunge double double.

Ukiachana na wabunge na wawakilishi, kuna baadhi ya nyadhifa za serikali zinaweza zikaunganishwa kupunguza gharama. Tuongeze utendaji, tupunguze kulala-lala.

Nionavyo mimi hawa wabunge ni wengi mno na wengi wao kusema kweli hakuna wanachokifanya. Watanzania tumekuwa wavivu kwenye kufanya kazi, baadhi ya majimbo sio makubwa hivyo, na nina uhakika mtu mchapakazi anauwezo wa kuendesha hata majimbo mawili. Believe me mtu anaweza kuchukua chini ya siku moja kwa baiskeli kuyazungukia majimbo yote ya Dar, na kwa jinsi technologia ilivyokuwa siku hizi kazi nyingi mbunge anaweza kuzifanya digitally.

Tofauti ni kwamba mwanzo wa serikali tatu unaweza ukawa mwanzo wa kusema bye bye kwa muungano, serikali ya muungano inaweza ikaamka siku moja ikajikuta haina pa kutawala.
 
Bahati mbaya ndani ya ccm, hakuna anayeweza kutoa majibu ya maswali haya, kwani wao wameambiwa msimamo wa chama ni serikali 2 kwisha. Anayeweza fafanua ni m/kiti(rais), ndiyo maana wote wanamsubiri yeye. Kuna ujanjaujanja wamefanya, eti wamepeleka kwa wanachama, huu ni utapeli tu. Wanaccm wengi hawajui hata kusoma na kuandika hivyo hawajui katiba inasemaje, zaidi ya kulishwa maneno tu.
 
hapa naomba Mungu zanzibar mkaze uzi! Maana hawa ccm wanataka kuleta janja ya nyani
...serikali 2 ipi na ipi?,coz kuna zanzibar hakuna Tnyika,
...hapa ni serikali 3 au 1....2 ni uongo
 
Ndugu wana JF, Ndugu wana JF, bila shaka mtakumbuka tambo za Katibu Itikadi na uenezi (CCM) kwamba wameteka mabaraza ya katiba kwa 90% upande wa Tanzania bara.

Lakini pia mtakumbuka malalamiko ya Nape wiki iliyopita akidai, "Warioba haitendei haki CCM" kisa kupendekeza muungano wa mfumo wa shirikisho wenye serikali tatu.

Turudi 2010, CCM walikuwa wapi kuingilia kati mabadiliko ya katiba iliyoitaja Zanzibar kuwa nchi? Kama waliona sawa, kwanini hawataki nchi iliyoungana na Zanzibar ionekane kwa sifa na mfumo, kuna siri gani? Tume ya mabadiliko ya katiba imetaja mambo 7 badala ya 22 yaliyopo sasa yaani Katiba na Mamlaka ya JMT, Ulinzi na usalama wa JMT, Uraia na Uhamiaji,Sarafu na Benki Kuu,Mambo ya Nje,Usajili wa vyama vya siasa na ushuru wa bidhaa na mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na Mambo ya Muungano.

HOJA;Upande wa Zanzibar, mambo yasiyo ya muungano yatatekelezwa na SMZ, je upande wa Tanganyika yatatekelezwa na nani?
proCCM ni blind, hawajui wafanyalo, unajua tunavyo tetea uwepo serikali tatu hawajui hata kwa nini haswa, na hata hawataki kuuliza what is the reason behind! VIJANA WA CCM WA TANGANYIKA KASOMENI KATIBA YA ZANZIBAR YA 2010! Inagalau mtapata upeo, acheni siasa za kukaririshwa na mababu!
 
Watanganyika endeleeni kupiga soga,huku zanzbr tunafanya matayarisho ya mwisho kuitangaza zanzbr ni nchi huru na haina muungano na nchi yoyote,nadhani hapo watanganyika mtazindukana.
 
Watanganyika endeleeni kupiga soga,huku zanzbr tunafanya matayarisho ya mwisho kuitangaza zanzbr ni nchi huru na haina muungano na nchi yoyote,nadhani hapo watanganyika mtazindukana.
Na sisi majority hatulipendi hili lidudu muungano, ni viongozi plus walinzi wa nchi hii wakishinikizwa na viongozi, tunataka muishie zenu na tukae kwa amani!
 
Kasimba G; Ni kweli mkuu, mathalani kuhusu mamlaka ya Ukuu wa nchi ibara ya 33 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema, "kutakuwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano (ibara ya 33(1)" na ibara ya 33 (a) inasema, "Rais atakuwa Mkuu wa nchi,Kiongozi wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu". Lakini katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 inamtaja Rais wa Zanzibar kuwa, "Mkuu wa nchi ya Zanzibar na Kamanda Mkuu wa vikosi vya idara maalumu ya vyombo vya ulinzi na usalama Zanzibar" Swali; Dhana ya Rais wa JMT kuwa mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa pande zote za muungano iko wapi?
 
Akina Nape, Mwigulu and the likes wamekaririshwa, hawajui wanafanya nini! Wangejua kitu watakuja kujua kitu wanachotetea bila kujua while is too late!
 
Momentum kuelekea mamlaka kamili is irrevesible. CCM na mabaraza yao feki ya katiba watakwenda na maji tu.
 
Bobwe; Mtajitangaza mara ngapi mkuu? Sijui nimtupie lawama Rais Kikwete na Mwenyekiti wa CCM kwa kushindwa kuisimamia katiba aliyoapa kuilinda maana tunajiuliza, kwanini CCM yenye ushawishi Zanzibar ilikaa kimya mwaka 2010 lakini wanazinduka leo? Nadhani nitakuwa nimetenda haki nikiwalaumu Watanganyika wote haswa PRO-CCM, Kwa mfano Ibara ya 34 (1) inasema, "Kutakuwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya muungano katika Jamhuri ya Muungano na pia juu ya mambo mengineyo yote yahusuyo Tanzania Bara" Na kwa upande wa Zanzibar vivyo hivyo. Hoja ya CHADEMA kwenye kudai serikali tatu wanahoji, ni lini baraza la mawaziri la Muungano linakaa kujadili masuala ya Muungano na ni lini linakaa kujadili masuala ya Tanzania Bara bila kusahau uwepo wa Mawaziri toka Zanzibar?
 
Last edited by a moderator:
Watanganyika mkitaka mpate salama basi ni lazima tanganyika irudi.
 
Hilo halitawezekana kwa mfumo wa sasa mkuu kwani vyombo vya dola ni vya jamhuri yya Muungano wa Tanzania. Mkifanya hivyo itakuwa ni uasi na mtaporomoshewa mizinga na kupigwa makombora! Yaani kwa ufupi Zanzibar ni hand-capped na haina ubavu wa kujitoa kwa nguvu kwenye muungano hadi hapo bara itakapotaka iwe hivyo!
Watanganyika endeleeni kupiga soga,huku zanzbr tunafanya matayarisho ya mwisho kuitangaza zanzbr ni nchi huru na haina muungano na nchi yoyote,nadhani hapo watanganyika mtazindukana.
 
Back
Top Bottom