Mie kwa mtazamo wangu, serikali tatu bado ni wazo zuri endapo kila upande wataheshimu Katiba na mipaka ya mambo yasiyohusu muungano. Nchi haiongozi kwa chama bali kwa katiba ambayo inapaswa isiwe na masilahi ya upande wowote kuruhusu kila upande kufuata misingi iliyowekwa ndani ya katiba.
Navyo ona mimi kwa sasa watu wamenza kuaminisha umma kuwa serikali tatu haifai kwa kuwa wanaweka masilahi binafsi kwanza na sio maslahi ya pande zote mbili. Mie najaribu kufikiria kama zanzibar ikiwa Nchi huru na Tanganyika ikwa huru tukawa na serikali inayotunganisha, Kila upande utakuwa na uhuru wakujiamulia mambo yao wanayoamini yatawafikisha hatu ya juu zaidi kimaendeleo. Lakini kwakua mchakato wa katiba wananchi kushirikishwa ni geresho, mwisho wasiku kile Serekiali inachokiamini kuwa sahihi ndichokitachowekwa kwenye katiba. Mie ndio maana bado naami swala la muungano lilitakiwa lipigiwe kura jambo ambalo watawala hawawezi kulifanya maana wanajua matokeo yake tayari.
Lakini haya ya kukandamiza democrasia yakweli yatafikia mwisho pale tu kila mtanzania atakapochukia na kutoridhika na hali aliyonayo na kujaribu kufikria sababu za kuwa katika hali aliyonayo ndipo fikra, udadisi na utayari wa kuhoji unajengeka na kuwa tayari kusimamia yale unayo yaamini. Kwa wengi wanaona maisha bado ni possible japo kwa njia ya kuuza rambo kariakoo na kupata kipato kidogo kwa shida kubwa na mwishowe hata hicho chako kidogo kinagombaniwa na watawala kama mpira wa kona kwa kurudhika na hali hiyo mabadiliko yatachukua muda sana. Linalotia matumaini kwa sasa na faraja ni hujuma na mabaya yanayotekelezwa na watawala kwa raia, wanasaidia na kuwa sehemu ya kuharakisha mchakato wa mabadiliko, na ndipo watanzania waingie mchakato wa tatu wakupata katiba huru.