Serikali tatu ndio dawa ya muungano!

Serikali tatu ndio dawa ya muungano!

Hadoop

Member
Joined
Oct 28, 2011
Posts
88
Reaction score
15
Ndugu zangu, tukiwa tunajiandaa na serikali tatu, nashauri watanganyika tuanze kujianda na yafuatayo:-

1. Tuwaambie kabisa wapenzi wa muungano huu, waanze kuanda ikulu yao atakayeishi rais wa huo muungano. Ikulu ya sasa ni mali ya Tanganyika.

2. Tuanze ku edit katiba yetu, YES ni ku edit tuu, kwani tunayo toka 1961 tulpopata uhuru, hivyo tunatakiwa kuondoa mapungufu na kuingiza mawazo mapya, hasa yale ya wazee wa chadema, yeah na ccm kwa ujumla.


3. Tuwaambie hao waumini wa muungano waombe mkopo kutoka ulaya mapema kujenga ukumbi wao wa bunge lao, yeah, otherwise watafanyia kwenye boti za azam, yeah si mbaya azam atauza juice pia.

4. Tuweke mipaka kabisa ya nini kinaruhusiwa kuguswa na muungano na kipi hakiruhusiwi.

Nimeongea kwa lugha ya utani, lakini ukweli ndio huu, vya Tanganyika mwachie Tanganyika, vya sultani mwachie sultani.
Hongera warioba, serikali tatu ndio dawa ya muungano.
 
Nakubaliana na wewe kabisa, tukiishapata serikali tatu tuanzishe part 2 ya mjadala wa jinsi yakuendelea kuungana na Zanzibar, namaanisha jinsi ya kuifanya Zanzibar kuwa WILAYA mojawapo ya Tanganyika.
 
Mkuu mi nadhani inatakiwa Muungano uvunjike kabisa sasa hivi, ili tuanze kulewana upya tuungane vipi kuelekea kwenye serikali kuu moja ambayo ndo itakuwa inafaa zaidi.
 
Mkuu mi nadhani inatakiwa Muungano uvunjike kabisa sasa hivi, ili tuanze kulewana upya tuungane vipi kuelekea kwenye serikali kuu moja ambayo ndo itakuwa inafaa zaidi.

Serikali 3 ndio mpango wenyewe wa kuua muungano kisomi zaidi.
 
watanganyika ni watu pori tu, hawasarifiki wamekaa kama mi---------, nani kakwambieni Wazanzibari wana haja na muungano na tanganyika? nyerere alimtisha tu karume nae kwa sababu alikuwa ni mnyasa akakubali,,,uvunjike tuone nani atakaemuomba mwenzake? manake Zanzibar from 1963 to 1964 before union ilikuwa inazisaidia nchi nyingi fedha tena cash,,ila watanganyika pamoja na kuwaibia wazanzibari hadi leo wanaomba mchele kwa vinchi vidogo kama TAILAND. ni aibu tupu kuungana na wanyamapori hawa.
 
Dawa ya muungano ni serikali mbili tu.

Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.

Hii dawa ilishatolewa mwaka 1994 lakini CCM ndio karata yao ya kubakia madarakani.

Umewasikia walivyopitisha maazimio yao katika vikao vyao. Wanataka mfumo uliopo uendelee.

Lakini Mwalimu Nyerere alishaweka kumbukumbu yake, alishauri haya:

Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar.Uk 11-12 link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

Je Nchi za Afrika Mashariki zimeamua kuungana?

Soma hapa Towards the EAC Political Federation


Jumuia ya Afrika Mashariki ina nia ya kuwa Shirikisho la Afrika Mashariki. Kwa nini hatuelekezi nguvu zetu huko?


Mchakato wa kuunganisha Afrika Mashariki unasema hivi:


Kuhusu hatua ya mwisho ya shirikisho la kisiasa, katika Mkutano Usio wa Kawaida mwaka 2004 Wakuu wa Nchi wa Kenya, Tanzania na Uganda waliazimia kuunda Kamati ya Kuharakisha Shirikisho la Afrika Mashariki. Kamati hiyo inayoongozwa na Amos Wako iliwasilisha taarifa yake kwa Wakuu wa Nchi mwezi November mwaka huo huo katika Mkutano wa Sita wa Wakuu wa Nchi.
Miongoni mwa mambo mingine, kamati hiyo ilitengeneza ratiba iliyotaka mambo yafuatayo:

a. Rasimu ya katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki ifi kapo Desemba 2007
b. Kupitishwa katiba na mkutano wa Wakuu wa Nchi mwezi Januari 2009
c. Kura ya maoni kuhusu katiba ifi kapo Desemba 2009
d. Shirikisho la kisiasa lenye urais wa mzunguko ifi kapo 2010 na uchaguzi wa rais ifi kapo 2013
Mkutano wa Wakuu wa Nchi Usio wa Kawaida uliofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2005 ulielekeza kuundwa kwa utaratibu wa mashauriano ya kitaifa kukusanya maoni kutoka kwa Waafrika Mashariki juu ya Shirikisho la Afrika Mashariki na kuharakisha mchakato huo. Uk 90 -92 link
http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27

 
Mkuu mi nadhani inatakiwa Muungano uvunjike kabisa sasa hivi, ili tuanze kulewana upya tuungane vipi kuelekea kwenye serikali kuu moja ambayo ndo itakuwa inafaa zaidi.

mnanifuraisha sana.. yani mkisikia watanganyika wanataka serikali yao mnakimbilia ooh tuwe na serikali moja???
akha ah ah mshindwe uku mkijua nasi tunataka serikali yetu. mbona zanzibar wamekuwa na serikali yao almost 49 years sie atukupepesa macho?? tnahitaji serikali tatu na hata zbar km wanapanga kuuvunja muungano kivyao vyao
 
kwa hiyo sisi watanganyika ni wanyama pori sio,
nyie mtakuwa wakufugwa. bara tutawafuga.
 
Back
Top Bottom