Serikali tegeni ndoo mahali panapovuja, tutapunguza tatizo la ajira nchini!

Serikali tegeni ndoo mahali panapovuja, tutapunguza tatizo la ajira nchini!

SubTopic

Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
95
Reaction score
175
Nawasalimu kwa jina la JMT,

Nadhani kwa wale tuliowahi kuishi nyumba zinazovuja mtanielewa kwa haraka.

Mvua inapokuwa inanyesha sehemu za paa zenye matundu huanza kuchuruza maji na ili kupunguza tatizo huwa tunatega chombo kwa ajili ya kuyakinga yale maji yanayovuja.

Sasa turudi kwenye mada yetu, yapo maeneo mengi tu ambayo mapato ya Serikali yanavuja na leo nitazungumzia hasa maduka ya vifaa vya vya ujenzi (hardware).

Pamoja na uwepo wa mashine za EFD bado kuna udanganyifu wa viwango vinavyokusanywa na wauzaji wa maduka haya kwa mfano unaweza ukanunua vifaa vya sh milioni 2 lakini akakuomba akuandikie risiti ya sh laki 5 au umenunua vifaa vya laki 1 risiti akakupa ya sh elfu ishirini tu.

Haya ni mapato yanayopotea na kuyadhibiti ni vigumu.

Maoni yangu:

Serikali iajiri watu kwa ajiri ya ku-monitor haya maduka yani kwenye kila hadware Serikali iweke mtu wake pale ambaye atakuwa mwangalizi kuhakikisha Serikali haiibiwi. Inaweza kuwalipa mshahara hata wa 50,000 tu kwa mwezi.

Najua wenye maduka watajaribu kuwapoza kwa chochote hawa wasimamizi wenu ili wasiwachome.

Nyie muwashauri wapokee tu hizo hela za wenye maduka maana ndo zinazovuja na kwa njia hiyo tutagawana kile kinachopotea.

Kwa mfano mwenye duka ataona chini ya usimamizi huu ataweza kupoteza kwa siku sh laki 2 aliyokuwa anaipata kwa kuepuka kodi hivyo hataona hatari kumpa msimamizi wenu sh elfu kumi kwa siku ili yeye aendelee kuiba. Sasa chukua kila siku kampa sh 10,000. ukizidisha x siku 30 unapata sh laki 3 kwa mwezi huo ni mshahara tayari.

Hapo nawashauri kateni ile 50,000 yenu huyu mtu abaki na 250,000.

Kiuhalisia msimamizi wenu atalipwa ile hela inayovuja ambayo hamuwezi kuipata nyie.

Nawasilisha.
 
Mawazo ya kishetani haya. Watu wanahangaika kutafuta juani, nyinyi mnataka tu kula kwa urahisi kivulini.

Si ungeishauri hiyo serikali yako ya kifisadi kuwapa mtaji ili muanzishe na nyinyi hizo hardware, badala ya kutaka mteremko?
 
Ukiachana na mapato mimi kwa upande wangu naishauri serikali idhibiti kwanza matumizi ya hovyohovyo na ya anasa kwenye pesa za umma.
Kila pesa inayokusanywa ikidhibitiwa matumizi yake hata wakwepa kodi wenyewe wataona aibu kukwepa kuichangia serikali.
 
Back
Top Bottom