GSM ndiyo Wadhamini Wakuu wa Yanga SC ambayo kwa msimu huu wamedhamiria kuchukua Ubingwa wa NBC Premier League kwa Gharama yoyote na kwa Mbinu zote zile za ndani na nje ya Uwanja.
GSM kuona Mipango yao bado haijakaa sawa ili Kuibeba Yanga SC yao sasa wameamua kutumia Mbinu ya Kipumbavu ambayo hata kwa Sheria za FIFA na za FAIR COMPETITION si tu hazikubaliki bali hazitakiwi pia.
GSM sasa tena kwa kufanya Kimya Kimya / kwa Siri wameamua Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu yaani NBC PREMIER LEAGUE ili zikiwa zinacheza na Yanga SC yao ipate Unafuu wa Ushindi ila Vilabu hivyo vikiwa vinacheza na Wapinzani wao wakubwa Simba SC viwe vinaikazia kwa ama Kuifunga au hata tu kutoka nayo Sare.
Kinachonisikitisha zaidi Uhuni na Upumbavu huu usio na Haki katika Ushindani Michezoni unafanywa na GSM halafu Serikali kupitia Wizara ya Michezo imekaa Kimya, TFF na Bodi ya Ligi wamekaa Kimya na Wahusika Wakuu wa Kupambana na Kuzuia Rushwa na Dalili zake zote TAKUKURU wamekaa Kimya.
Akitokea tu Mtu Mmoja au Klabu Moja ikajipanga vyema kwa Sheria na Ushahidi wa Kutosha juu ya Uhuni na Upumbavu huu wa GSM katika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kwa nia ya kupata Unafuu ikicheza nazo na akaenda Kushtaki FIFA kuna uwezekano mkubwa NBC Premier League ikaingia matatizoni, Klabu Moja kubwa Kufungiwa, huyu Mdhamini wao Mkuu GSM Kushtakiwa na hata Mpira wa Tanzania Kuharibika rasmi.
Hakuna Mfanyabiashara Mstaarabu na Muungwana Tanzania hii kama Mzee Bakhressa na Kampuni yake ya Azam. Na hakuna pia Kampuni ambayo ni Tajiri Tanzania nzima kama ya Azam.
Azam Wana Timu yao ya Azam FC ila kwa miaka Saba sasa wanapambana Kuwa Mabingwa ila bado hawajafanikiwa. Lakini sijawahi ama Kuona au Kusikia mahala popote pale Azam wakizihonga Timu mbalimbali za Ligi Kuu ya Tanzania ili ziiachie na iwe Bingwa japo ina uwezo wa Kifedha maradufu ya hawa Matapeli wa GSM ila wameamua Kupambana kwa Kucheza tu Uwanjani.
Kama GSM kweli walikuwa na nia ya Kuvidhamini Vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania NBC PREMIER LEAGUE walikuwa wapi Kujitokeza pale TFF na Bodi ya Ligi walipokuwa wanatafuta Wadhamini?
Hivi leo hii Mo Dewji na Kampuni yake / Kampuni zake angeamua nae Kufanya Uhuni na Upumbavu huu usio wa Haki unaofanywa na GSM kwa Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu tena Kisirisiri / Kimya Kimya na kuwaambia wawe wanaikamia tu Yanga SC ila zikiwa zinacheza na Simba SC wawe wanailegezea FAIR COMPETITION ingekuwepo?
Sasa kama unatamba kuwa na Kikosi kizuri na unasema msimu huu Kombe ni lako kwa Soka Kubwa unalocheza kwanini unahangaika Kuvidhamini Vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu kisha unavipa Ahadi ya Tsh Milioni 15 vikiishinda Simba SC na Tsh Milioni 10 vikitoka nayo Sare mpaka unasababisha Wachezaji wa hizo Timu Kuikamia Simba SC, Kuwaumiza kwa Makusudi Wachezaji wake na pale Wakifungwa baada ya Filimbi ya mwisho badala ya kuondoka Uwanjani wanaanza Kuangua Vilio, Kugombana na Kulaumiana mno?
GSM wameshaiharibu Ligi Kuu ya NBC.
Ndhani ukisoma hii hapa itakupa mwanga
- Baadhi ya wachambuzi wameshikia bango suala la FAIR COMPETITION kuhusu (GSM) kuvidhamini baadhi ya vilabu vya ligi kuu 🇹🇿
- Hoja hizo zimeibuliwa na Jemedari Said, Mkazuzu na Shaffih Dauda,, acha nami nitoe mchango wangu kuhusu hilo.
- Hili suala la udhamini unaofanywa na kampuni ya GSM kwa vilabu tofauti limeanza tangu misimu kadhaa nyuma iliyopita,, kwa nini hoja hizi zinaibuka sasa ?
- (FIFA) inazuia vilabu zaidi ya kimoja kumilikiwa na kampuni / mtu mmoja kwenye ligi moja, haizuii UDHAMINI (SPONSORSHIP).
- Kampuni ya (GSM) haimiliki klabu ya Coastal union wala Namungo fc, bali inavidhamini (SPONSORSHIP) hivyo haiwezi kuathiri competition husika.
- Kampuni ya Azam inayomilikiwa na Bakhresa, ina timu ligi kuu Tanzania bara inayoitwa Azam fc, lakini pia inadhamini timu zote kwenye ligi hiyo,, kwa nini wasihoji FAIR COMPETITION kuhusu suala hilo ?!.
- Azam ndio wanatoa pesa nyingi zaidi kwa vilabu, vipi wakiamua kuchelewesha pesa hizo kwa vilabu kwa makusudi, wazuie replay za matukio uwanjani ambayo yanaibeba timu yao hiyo FAIR COMPETITION itakuwepo ?
- Msimu uliopita kampuni ya Metl inayomilikiwa na Mohamed Dewji ilikuwa inaidhamini klabu ya Namungo fc kupitia sabuni ya MO POA, wakati huohuo Metl inaidhamini Simba sc na sio kuidhamini pekee, mmiliki wa kampuni hiyo ana hisa katika klabu ya Simba kwamba ni sehemu ya umiliki wa klabu ya Simba sc,, kwa nini suala la FAIR COMPETITION halikuhojiwa wakati huo ?
- Baada ya Mo sabuni kufika mwisho wa udhamini kwa Namungo fc na GSM kama kampuni kuingia Namungo ndipo hoja za FAIR COMPETITION zimeibuka sasa,, kuna agenda gani ya siri hapo ?!
- Kitu pekee (FIFA) wanapinga ni timu mbili au zaidi KUMILIKIWA na kampuni / mtu mmoja, hawana shida kabisa na kampuni kudhamini timu hata ziwe timu 200 zimedhaminiwa na mtu mmoja.
- Kabla ya Mohamed Dewji kununua hisa Simba sc alikuwa mmiliki wa klabu ya African Lyon, wakati huohuo akiwa mfadhili wa klabu ya Singida Utd,, hoja hizo mbona hazikuibuliwa iwe sasa ?!
- Tangu msimu juzi (GSM) anaidhamini Coastal union, msimu uliopita Yanga sc alifungwa mabao (2-1) na Coastal union, kabla ya kupoteza mchezo dhidi ya Coastal union Yanga ilikuwa haijapoteza mchezo wowote,, hiyo FAIR COMPETITION isingekuwepo Coastal angeweza vipi kuifunga Yanga sc tena wakati Yanga ikiuhitaji zaidi ushindi katika harakati za kuusaka ubingwa !!!
- Kwa sasa naona nibora tumpongeze Azam kuweka pesa kwenye ligi yetu, pesa ambazo zimesababisha ligi iwe ngumu na sio kutafuta vijisababu ambavyo havipo.