Serikali, TFF, Bodi ya Ligi na TAKUKURU; Kwa uhuni huu wa GSM ile "Fair Competition" inayotakiwa na FIFA ipo wapi?

Coastal Union mmeshawapa laki mbili mbili zao. Au bado mnawazingua. Acha ujinga!

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Hawana akili hawa Makolo
 
GSM kapania kuchukua ubingwa anapambana nje na ndani ya uwanja hilo lipo wazi kabisa haihitaji ubishi.
Mifano ni mingi tu - Senzo kwenda Yanga , Manara kwenda Yanga hao sio wachezaji kumbuka na watamsajili mchezaji yeyote Simba ambaye ni kipenzi cha Simba kuleta taharuk, hii yoote sio kwa ajili mpira wana malengo yao.
Gsm wanajulikana hata kibiashara hawapendi fair wanapenda fitna na kona nyingi kutumia pesa n.k.
Ni waharibifu lakini kwa Yanga watapata mafanikio ya muda mchache na wataharibu saana na hapo Yanga wamewekwa tu waliitaka Simba zaidi - malengo yao kwa anao wajua yapo wazi kabisa, wana pesa nyingi za mkato nyingi tu na hapa nchini watafanikiwa hassa zama hizi.
Muda utaongea.
 
Ndhani ukisoma hii hapa itakupa mwanga

- Baadhi ya wachambuzi wameshikia bango suala la FAIR COMPETITION kuhusu (GSM) kuvidhamini baadhi ya vilabu vya ligi kuu 🇹🇿

- Hoja hizo zimeibuliwa na Jemedari Said, Mkazuzu na Shaffih Dauda,, acha nami nitoe mchango wangu kuhusu hilo.

- Hili suala la udhamini unaofanywa na kampuni ya GSM kwa vilabu tofauti limeanza tangu misimu kadhaa nyuma iliyopita,, kwa nini hoja hizi zinaibuka sasa ?

- (FIFA) inazuia vilabu zaidi ya kimoja kumilikiwa na kampuni / mtu mmoja kwenye ligi moja, haizuii UDHAMINI (SPONSORSHIP).

- Kampuni ya (GSM) haimiliki klabu ya Coastal union wala Namungo fc, bali inavidhamini (SPONSORSHIP) hivyo haiwezi kuathiri competition husika.

- Kampuni ya Azam inayomilikiwa na Bakhresa, ina timu ligi kuu Tanzania bara inayoitwa Azam fc, lakini pia inadhamini timu zote kwenye ligi hiyo,, kwa nini wasihoji FAIR COMPETITION kuhusu suala hilo ?!.

- Azam ndio wanatoa pesa nyingi zaidi kwa vilabu, vipi wakiamua kuchelewesha pesa hizo kwa vilabu kwa makusudi, wazuie replay za matukio uwanjani ambayo yanaibeba timu yao hiyo FAIR COMPETITION itakuwepo ?

- Msimu uliopita kampuni ya Metl inayomilikiwa na Mohamed Dewji ilikuwa inaidhamini klabu ya Namungo fc kupitia sabuni ya MO POA, wakati huohuo Metl inaidhamini Simba sc na sio kuidhamini pekee, mmiliki wa kampuni hiyo ana hisa katika klabu ya Simba kwamba ni sehemu ya umiliki wa klabu ya Simba sc,, kwa nini suala la FAIR COMPETITION halikuhojiwa wakati huo ?

- Baada ya Mo sabuni kufika mwisho wa udhamini kwa Namungo fc na GSM kama kampuni kuingia Namungo ndipo hoja za FAIR COMPETITION zimeibuka sasa,, kuna agenda gani ya siri hapo ?!

- Kitu pekee (FIFA) wanapinga ni timu mbili au zaidi KUMILIKIWA na kampuni / mtu mmoja, hawana shida kabisa na kampuni kudhamini timu hata ziwe timu 200 zimedhaminiwa na mtu mmoja.

- Kabla ya Mohamed Dewji kununua hisa Simba sc alikuwa mmiliki wa klabu ya African Lyon, wakati huohuo akiwa mfadhili wa klabu ya Singida Utd,, hoja hizo mbona hazikuibuliwa iwe sasa ?!

- Tangu msimu juzi (GSM) anaidhamini Coastal union, msimu uliopita Yanga sc alifungwa mabao (2-1) na Coastal union, kabla ya kupoteza mchezo dhidi ya Coastal union Yanga ilikuwa haijapoteza mchezo wowote,, hiyo FAIR COMPETITION isingekuwepo Coastal angeweza vipi kuifunga Yanga sc tena wakati Yanga ikiuhitaji zaidi ushindi katika harakati za kuusaka ubingwa !!!

- Kwa sasa naona nibora tumpongeze Azam kuweka pesa kwenye ligi yetu, pesa ambazo zimesababisha ligi iwe ngumu na sio kutafuta vijisababu ambavyo havipo.
 
Tukiomba uthibitisho wa hiko ulichoandika sina hakika kama unaweza fanya hivyo. Kwahiyo hata Makolo FC pia mmehongwa?
 
Akili za kipumbavu hizi. Kwa hiyo watendaji wa vilabu kuhama ni njama? Mbona ninyi mlimuiba Morrison? Lengo sio kuidhoofisha Yanga? Tumia akili sio ushabiki mbele
 
Mkuu hawa akina mkazuzu na jemedari ni wachambuzi njaa tu wakipigwa laki 2 wanaibuka na vioja visivyo na kichwa wala miguu.
 
Yanga na Msukule wao baada ya kuona yamestukiwa... Yakaanzisha mada ya Chama.... Big up mkazuzu na Shiffih
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…