Serikali toa tamko kuhusu Balozi Nchimbi kutenguliwa kisha kurudishwa kisiri siri kazini bila umma kutangaziwa

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
1,831
Reaction score
5,489
Serikali itoe taarifa kwa umma kama utenguzi wa Balozi wa Tanzania nchini Misri ulifutwa ama laa.

Tarehe 15 August 2023 Rais Samia alifanya mabadiliko ya vituo vya kazi na utenguzi wa mabalozi na kumrejesha nyumbani Balozi wa Misri Nchini Tanzania Ndugu Emmanuel Nchimbi, na nafasi yake ikachululiwa na Balozi Meja General Makazo.
Taarifa hiyo ilitolewa kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Tangu hapo hakukuwepo na taarifa yoyote ya mabadiliko juu ya nafasi hiyo.

Lakini siku 42 baadae yaani juzi baada ya Tanzania kupata nafasi ya kuwa mwenyeji wa AFCON 2027, Msafara wa Tanzania uliongozwa na Balozi wa Tanzania nchini Misri ambae ni Dr Emmanuel Nchimbi ambae taifa linajua alitenguliwa na kurejeshwa Tanzania. Taifa linatakiwa kutangaziwa mabadiliko mengine kama yalifanywa na lifahamishwe Meja Jenerali Makanzo kapelekwa kituo gani cha kazi ikiwa Nchimbi bado anahudumu kama balozi nchini Misri.

Ni takwa la kikatiba na kisheria umma kutangaziwa mabadiliko ya nafasi yoyote ya uteule wa kirais na sio vinginevyo. Kama kuna Mabadiliko ya kimyakimya basi yanaleta mkanganyiko kwa umma.
 
Serikali huwa haifanyi shughuli zake kwa pupa, hususani kwenye masuala ya mambo ya Nje. Kuna kanuni zake.
 
Ni takwa la kikatiba na kisheria umma kutangaziwa mabadiliko ya nafasi yoyote ya uteule wa kirais na sio vinginevyo. Kama kuna Mabadiliko ya kimyakimya basi yanaleta mkanganyiko kwa umma[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmmh hayo sijui kwakweli
Ninachojua mie tu ni kwamba Nchimbi ni mwanasiasa mkongwe na mbobevu
Pia ni hazina kwa taifa kwa nyazifa kadhaa amabazo ametumikia kwenye nchi
Bado ni hazina ambayo ikihitajika wakati wowote itatumika kwa maendeleo ya nchi.

Sent from my V2026 using JamiiForums mobile app
 
Anafanana na Jonas Savimbi!
 
Wewe hujioni kuwa hazina ya taifa hili isipokuwa mwanasiasa mkongwe Nchimbi ? 😳
 
Nadhani ni kwa sababu walikosa sababu ya kuwaeleza wananchi kwa nini wamemrudisha.
 
Kwanza alitolewa brasil akarudi bongo akasota weeee ndio akaenda Egypt .....wanamuogopa sana ....siasa chafu ndio mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…