Serikali toeni ufafanuzi unaoelewekaa kuhusu kufunga barabara za jiji

Tanzania wanaopewa nyazifa hufanya maamuzi bila kuzingatia madharau ya hapo baadae, (the aftermath)
 
Wageni wapelekwe mpaka Sinza...ila Deligesheni ya South balaah unawez a fukuzwa kazi kisa UDENDA
 
Uzuri tangazo limeeleweka
We jitoe ufahamu ndo utaelewa wamemaanisha walichosema
 
Wabongo wengi vichwa maji sasa serikali imekataza bodaboda na bajaji haijakataza gari binafsi na daladala za garden posta na kivukoni
Unafahamu mchango wa bodaboda na bajaj kwenye shughuli za uzalishaji katika jiji hili la Dar es salaam? 😲
 
kwahiyo hata hao wageni wakiwa wamejifungia ukumbini wanasikiliza hotuba zao..barabara hazitotumika tena hadi wafunge mkutano warudi mahotelini kupumzika..tatizo tangazo limetolewa hovyo lilitakiwa waseme barabara zitafungwa kwa masaa kadhaa mfano muda wa viongozi kutoka hotelini kwenda ukumbi wa mikutano hapo barabara zitafungwa hadi viongozi wote wakishatimia ukumbi wa mkutano barabara zirudi kawaida..na muda wa kumaliza mkutano kurudi hotelini pia wanapishwa kwa muda hizo barabara na kwa speed ya misafara ya hawa jamaa masaa mawili yanawatosha kabisa maana wanapota njia tofauti tofautu hadi mahotelini..ila kwa vile wenye mamlaka wamezoea kutukomoa mbona tutakoma siku 4 hizo.!
 
Unafahamu mchango wa bodaboda na bajaj kwenye shughuli za uzalishaji katika jiji hili la Dar es salaam? 😲
Mbona kipindi cha nyuma bodaboda hazikuruhusiwa kuingia posta? Au unadhani zimekatazwa kuwepo dar nzima?
 
Cha kufanya mkutano ungefanyika dodoma moja ya mambo yanashangaza ni kujenga ikulu kubwa dodoma na kupafanya pawe makao mkuu ya serikali alafu hapatumiki
 
Kwahiyo huku Arusha sisi ndo hatuna shughuli za kufanya? Au unadhani tunatumia ungo kama means ya usafiri?
Barabara za Arusha ni chache.
Hapana,ila kwa kiasi chake Arusha ina mzunguko mdogo wa watu kuliko dar es salaam.

Athari zitakazopatika hapa dar kwa kufunga barabara hizo ni kubwa mara kadhaa kuliko mkoa mwingine.
 
Lakini nadhani matumizi ya barabara kwa maana ya magari hayana wingi kama dar.
 
Mji wa kibiashara unafunga barabara zote hizo kisa mkutano tu.

Shughuli za watu zinaharibika na serikali inapoteza mapato.
 
Hapana,ila kwa kiasi chake Arusha ina mzunguko mdogo wa watu kuliko dar es salaam.

Athari zitakazopatika hapa dar kwa kufunga barabara hizo ni kubwa mara kadhaa kuliko mkoa mwingine.
Huo ni mkutano mkubwa. Kama barabar nyingi hivyo zinafungwa huku dar basi huku Arusha watafunga barabara zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…