Mr Bakari Yusuph
Member
- May 19, 2024
- 10
- 7
Chanzo: mtandaoni
Tatizo la ajira ndugu wa Tanzania limekuwa janga kubwa sana kwa vijana waliohitimi vyuo mbali mbali nchini ,Serikali inajaribu kifanya juu chini kuweza kupunguza makali yake.Wahitimu wengi wamekuwa wakitapatapa kujikwamua kimaisha kwa kutafuta ajira pamoja na mitaji kwa ajiri ya kujiajiri lakini mambo yamekuwa magumu hata kupata hiyo motaji.
Mikopo imekuwa ya masharti magumu mno,waajiri wamekuwa na masharti mengi wakisisitiza uzoefu zaidi kwa waombaji hali inapelekea kukosa sifa je tumesoma tuzidishe idadi ya wategemezi?
Serekali ianzishe mkakati wa lazima kwa Taasisi na makampuni binafsi kutenga asilimia 20% za ajira za Muda
MFUMO
(WASOMI BOOST)
Chanzo: Mtandaonu
Sheria hiyo itaruhusu na kuwataka wamiliki na waajiri wa Taasisi binafsi na serikali pamoja na makampuni yote ketenga 20% kwa ajili ya Ajira za muda kwa wahitimu
(1) Wahitimu waliotoka moja kwa moja vyuoni
(2)Ambao walishahitimu
UTEKELEZWAJI WA MFUMO
Serikali inatakiwa kupitia serikali mtandao kupitia Tamisemi kuanzisha mfumo wa maombi za ajira za muda ambapo kila kuhitimu ataomba kulingana na fakalti yake nakuomba pamoja na kupatiwa
Muda wa mkataba ya ajira hizo
Waajiri kupitia sheria hiyo elekezi watapaswa kuwaajiri na kuwapatia mkataba ya mwaka mmoja tu vijana waliopata nafasi
Maelekezo juu ya malipo na staiki zote kazini
Waajiri wanatakiwa kuwalipa waajiriwa hao wa muda 70% ya mshahara ila wafaidike na marupuru yote kama ilivyo kwa wengine.
Mfumo wa Malipo na usimamizi wake kulingana na Lengo la Mkakati wa Boost
Mkakati huu ifahamike ni kwa ajili ya kuondoa kabisa 80% kwa wasomi juu ya Ajira za moja kwa Moja na kuzingatia wasomi kujiajiri wenyewe.
(1) Malipo yote ya mradi wa Boost yatalipwa kupitia Bank ya serikali chini ya mfumo wa Boost ambapo.
Waajiriwa hao watapewa 40% ya basic salary zao pamoja na makusanyo ya posho zote.
Mwisho wa mkataba
Serikali itawalipa 60% ya mishahara Yao
MKAKATI ENDELEVU NA FUATILIVU WA BOOST
Serikali miezi mitatu kabla ya kuisha kwa mikataba ya ajira wa Boost wasomi ikusanye taarifa hizi
(1) Ni waajiriwa wangapi waajiri wamependa kubaki nao
(2) Waajiriwa ambao watamaliza mkataba Wana penda kujiajiri katika kitu gani
Mkakati Saidizi ya elimu na mafunzo ya fursa na kujuajiri kwa mfumo wa Boost wasomi
Serikali na wadau mbali mbali watawapatia vijana hao elimu na kuwafungulia Fursa mbali mbali vijana wa Wasomi Boost.
Mkakati saidizi
Serikali kupitia mfumo maalum ambao utaanzishwa utatakiwa kuwa weka kimakundi kulingana na mkoa waliopo vijana hao.
Kwa kutengenezea uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo vidogo kupitia 60% ya ile akiba ya Wasomi Boost
Kuanzia Kilimo,Usafirishaji, Uvuvi,Huduma za fedha,n.k.
USIMAMIZI JUU YA UENDELEVU WAKE
Serikali kupitia Watendaji na maafisa maendeleo ya kata wataratibu maendeleo ya miradi hiyo ngazi ya kata pamoja na wadau wengine.
FAIDA. YA MRADI WA BOOST WASOMI
1.Kuondoa utegemezi wa ajira serikalini na taasisi binafsi
2.kuanzishwa kwa wingi viwanda na wasomi
3.Serikali kuweza kurudisha kikamilifu marejesho ya mikopo ya elimu ya juu na wengine kunufaika zaidi
4.kuongezeka kwa ajira nyingi kutokana na miradi inayo anzishwa
5.Serikali kuaminika na kupendwa
6.Kupunguza matatizo ya afya ya akili kwa wasomi
Nahitimisha wasomi ni msingi muhimu wa maendeleo endelevu ya taifa tuwajali na tuwaonyeshe upendo huu kama alama ya kuwa jali na hii ndio TANZANIA TUNAYO ITAKA.
Upvote
3