Serikali: Tutaanza kuwalipa fidia wananchi wa Kipunguni waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege

Serikali: Tutaanza kuwalipa fidia wananchi wa Kipunguni waliopisha upanuzi wa uwanja wa ndege

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Serikali imesema kuwa itaanza kufanya malipo ya fidia kwa wananchi wa Kipunguni waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam ambao madai yao yamehakikiwa na hayana vikwazo vyovyote.

Hayo yameelezwa bungeni, jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), alipokuwa akijibu swali la Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Azan Zungu, aliyetaka kujua wakati ambao Serikali itawalipa fidia wananchi wa Kipunguni waliopisha ujenzi wa Uwanja wa Ndenge wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Naibu Spika aliuliza swali hilo baada ya Naibu Waziri wa Uchukuzi , Mhe. David Kihenzile kujibu maswali mbalimbali ya wabunge kuhusu fidia za wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa Viwanja vya Ndege mbalimbali nchini.

Dkt. Nchemba, alisema kuwa wananchi walishapewa mwongozo na Serikali kwa kuwa iligundulika kuna baadhi ya wananchi walipewa maeneo mbadala ambayo yalikuwa sehemu ya madai na kuna baadhi ambao walikuwa wanahitaji fidia zaidi.

Alisema Serikali imeshapeleka timu ya wataalamu kwenda kufanya uhakiki ili kuainisha madai na kupata madai sahihi kutokana na kuwepo kwa madai ya kuwa kuna baadhi ya wananchi wanadai fidia zaidi.

“Sasa, tunaendelea kutafuta fedha ndani ya mwaka huu wa fedha unaoendelea ili kuanza kufanya malipo”, alibainisha Mhe. Dkt. Nchemba.

Dkt. Nchemba alisema kuwa tathimini mpya ya ardhi na mali iliyofanyika kwa wakazi 1,184 inaonesha kuwa Serikali italipa zaidi ya shilingi bilioni 144, ikilinganishwa na tathimini ya awali iliyofanyika mwaka 2009 ambayo ilionesha kuwa wakazi hao walistahili kulipwa shilingi bilioni 15.5.

Pia soma:
 
Bajeti ya wenza, wengine waliotuibia sana wakiwa madarakani, ilipatikana fasta; pesa ya wananchi maskini, bado "inatafutwa". Mungu anawaona viongozi wa nchi hii!
 
Zaidi ya wakazi 1,000 wa Eneo la Kipunguni huko Kipawa Dar Wanaidai Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni 144 za fidia baada ya kupisha Upanuzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Terminal 3.

Akitoa majibu ya Serikali Naibu Waziri wa Uchumi amesema Serikali inatafuta pesa kuwalipa.

View: https://www.instagram.com/reel/C5h64KOshNT/?igsh=bzRzcXIxNHBvbHV3

My Take
Hakuna wa kulipa Hayo Mabilioni labda ingekuwa kesi ya kina Downs au Ndege Kushikiliwa.
 
Huu ndio unyama wa ccm tunaousema , kipunguni inatia huruma , unaambiwa hata choo kikijaa hawatakiwi kurekebisha , wasubiri malipo !
 
Kama hawana Nia ya kulipa wawaache watu waendelee maeneo Yao na anayetaka kuuza awe huru kumuuzia mtu.

Serikali inawatia umaskini watu wake, hiyo ni issue ya kitambo Sana.
 
Huu ndio unyama wa ccm tunaousema , kipunguni inatia huruma , unaambiwa hata choo kikijaa hawatakiwi kurekebisha , wasubiri malipo !
Serikali inashindwa kuwalipa watu pesa hata Kwa awamu? Uzembe wa Hali ya Juu huu.
 
Mmmhhh tathmini toka ya awali Tshs 15.5 bilioni mwaka 2009 hadi tathimini mpya tshs 144 bil? Jamani, hapa mbona naona kuna maswali makubwa mnooooo, tofauti haiwezi kuwa kubwa hivyo, naona upigaji hapa, kuna kosa kubwa sana hapa, TAKUKURU mambo kama haya ndio inatakiwa inachukua chap na kufuatilia
 
Mmmhhh tathmini toka ya awali Tshs 15.5 bilioni mwaka 2009 hadi tathimini mpya tshs 144 bil? Jamani, hapa mbona naona kuna maswali makubwa mnooooo, tofauti haiwezi kuwa kubwa hivyo, naona upigaji hapa, kuna kosa kubwa sana hapa, TAKUKURU mambo kama haya ndio inatakiwa inachukua chap na kufuatilia
Mwakani ni uchaguzi mkuu, waziri wa fedhea Mwigulu Nchemba.
 
Ndugu zangu watanzania kuna vitu vikitokea unahisi kufa kabla ya kufariki

2017 walipima wakasema watu wa kipungun wasipangishe tena wala kujenga

Watu wakasubiria fidia ola ikawa kidia

Sasa 2022 wamepima tena kipungun wakambiwa wanaondolewa wakajulishwa mpaka na kiasi kwa kila atakaeondolewa

Ukweli zoezi hili limekuwa kinya kana yaliyotokea 2017 mkumbuke 2022 nako wakashauri wapangaji wahame wakahama watu wasijenge wakasimamisha ujenzi

Jaman march imetimia mwaka mmoja tangu waapimiwe na kuhaidiwa fidia waachie maeneo yao

Swali

Wale wapangaji waliofukuzwa na wajane huku wakitegemea peda za watoto shule nani anawalipa wamiliki

2;tuwe na ubinadamu jaman 2017...2022 yaleyale kwann msiseme hadharani wananchi pesa kwa sasa no waendeleee kujenga wakodishe waendelee kula mema ya nchi

Kuna wazee wamekufa hawataona fidia zao kama zitakuwepo

Tuwaangalie ubinadamu kwanza kwenye hili jamboo mbunge husika naamini utalizingatia na kuwatetea wananchi wakoo

Kiujumla wana kipungun tumechoka na siasa kwenye hili semen ukweli wapen watu uhuru wa kufanya yao kwenye ardhi zao kama pesa haipo kwa sasaaaa

Wananchi watakufa hawajaenjoy maisha ya ardhi zao walizojenga ati

Alldbest
 
Aliyekudanganya kwamba ccm ina huruma ni nani ?

Hicho ndio chama kinachoongoza kwa ukatili kwa sasa duniani
 
Back
Top Bottom