Serikali: Ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa utagharimu jumla ya Tsh. Bilioni 31 hadi kukamilika

Serikali: Ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa utagharimu jumla ya Tsh. Bilioni 31 hadi kukamilika

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Serikali inatarajia kutumia Tsh. 31,329,180,963.16 kwaajili ya Ukarabati wa Uwanja wa Michezo wa Benjamin Mkapa kwa awamu ya kwanza ambapo hadi kufikia Aprili 2024 Tsh. Bilioni. 7.44 zimelipwa kwa Mkandarasi

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, ukarabati huo unajumuisha Vyumba vya Wachezaji, Waandishi wa Habari, Watu Mashuhuri, Taa na Eneo la Kuchezea pamoja na Matangazo ya Kidigitali

Aidha, Wizara imesema awamu ya kwanza ya ukarabati katika maeneo mbalimbali katika Uwanja huo umefikia wastani wa kati ya Wastani wa 60%, 80%, 98% na maeneo mengine yamekamilika kwa 100%

Pia Soma:
 
Hivi hii nchi mbona wanatuona wananchi wapumbavu kiasi hiki? Yani ukarabati bilion 31? Je ulijengwa kwa sh ngapi? Upuuzi gani huu? hiyo hela inajenga viwanja vingapi vinavyolingana hadhi na wa azam complex? Na kuondos uhaba wa viwanja vyenye hadhi ya ligi yetu kwa miaka 20 ijayo? Kwanini huo uwanja usifanyiwe ukarabati wa kawaida tu? Yanga kila siku na hoja zao za bure wamekuwa wakihujumu uwanja na hakuna hatua zinachukuliwa upuuzi tupu hiyo hela ni nyingi sana wabunge wakikubaliana na hiyo hoja tutakutana nao majimboni 2025 huo ni upigaji wamefunga advertisement board kwenye uzinduzi wa AFL leo zimekingwa na mabodu ya mabati ufafanuzi hela ngapi zilitumika hakuna haziwaki kwanni ufafanuzi hakuna yaani nchi hii uwazi kwenye masuala ya matumizi ya fedha ni kinyaa na yale mabodi ni used lini serikali ikanunua mali used?📢🤗
 
HAya ndio mambo Lucas Mwashambwa unatakiwa kujibia serikali yako na chama chako kama unakubaliana nayo au kueleza mapungufu kama yapo!

Unatakiwa kuendana na

Ahadi za CCM: Binadamu wote ni sawa, Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko na Sitatoa wala kupokea rushwa johnthebaptist

Wacha wajipigie tu,hakuna kazi inayotajirisha haraka kama siasa.
 
this pitch is geting service after every 6 months and nothing is change in it
 
Halafu wanasema serikali haina hela ya kuajiri watumishi wengi,wakati wanachezea pesa namna hi aisee.
 
Alafu mbona kama vile zile screen za matangazo wamezitoa
 
InShot_20240415_194747455.jpg
 
Hiyo pesa bora wangenunua makapeti ya maana wangeweka kwenye viwanja hata kumi vya hapa bongo
 
The math does not mathing! Mradi utagharimu bilioni 30. Mradi umekamilika kwa 60-70% na sehemu nyingine 100% kwa kutumia bilioni 7. Kazi iliyobaki itagharimu bilioni 23?

Amandla...
 
Hivi hii nchi mbona wanatuona wananchi wapumbavu kiasi hiki? Yani ukarabati bilion 31? Je ulijengwa kwa sh ngapi? Upuuzi gani huu? hiyo hela inajenga viwanja vingapi vinavyolingana hadhi na wa azam complex? Na kuondos uhaba wa viwanja vyenye hadhi ya ligi yetu kwa miaka 20 ijayo? Kwanini huo uwanja usifanyiwe ukarabati wa kawaida tu? Yanga kila siku na hoja zao za bure wamekuwa wakihujumu uwanja na hakuna hatua zinachukuliwa upuuzi tupu hiyo hela ni nyingi sana wabunge wakikubaliana na hiyo hoja tutakutana nao majimboni 2025 huo ni upigaji wamefunga advertisement board kwenye uzinduzi wa AFL leo zimekingwa na mabodu ya mabati ufafanuzi hela ngapi zilitumika hakuna haziwaki kwanni ufafanuzi hakuna yaani nchi hii uwazi kwenye masuala ya matumizi ya fedha ni kinyaa na yale mabodi ni used lini serikali ikanunua mali used?📢🤗
Yanga ni ccm
Kijani
Njano
 
Back
Top Bottom