Serikali: Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi walioajiriwa ni elfu nane pekee

Serikali: Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi walioajiriwa ni elfu nane pekee

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Serikali imesema idadi ya walimu wa shule za msingi na sekondari walioajiriwa ni 8,000 pekee tofauti na 13,000 inayolalamikiwa na wadau. Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt Laurean Ndumbalo amefafanua kuwa katika kibali cha ajira za walimu elfu 13 alichotoa Rais Magufuli wameajiri Walimu 8000 kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili wataajiri Walimu 5000 ilikufikia idadi ya ajira elfu 13.

PIA, SOMA=> https://www.jamiiforums.com/threads/tazama-baadhi-ya-mapungufu-yaliyojitokeza-katika-majina-ya-ajira-za-ualimu-yaliyotolewa-jina-la-abadallah-leonard-shonde-lajirudia-mara-196.1814578/
 
Maelezo kuhusu hiyo elfu5 pungufu yakoje?

Naona kabisa kuna mtu ameshapoteza kibarua pale TAMISEMI 😎
Wameona wameshashitukiwa jina moja lina appear mala196!!! Ili kuongeza idadi!! Hakuna wakufukuzwa kazi kwani ni maelekezo sio kuwa ni tamko lake!! Mkisema sana watatangaza nafasi za kazi hizo 5000!!kishaaa kimya!! Watakwambia majina yapo kwenye data base walishaitwa kuripoti kazini.
 
Baada ya wadau kulalamika idadi ya walioajiriwa kuwa siyo iliyotangazwa na serikali ikiwemo baadhi ya majina kujirudia mara nyingi, leo serikali imesema walioajiriwa ni 8,000 pekee. Idadi hii mpya iliyotangazwa ni pungufu ya watu 5,000 ya idadi iliyotajwa awali.

PIA, SOMA=> Madudu yaliyofanyika kwenye ajira za Ualimu zilizotangazwa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE S3630-0099/2013' lajirudia mara 196
Bwana Shonde a k a Shonde boy,ameula maana kaajiriwa mara 196.
 
Baada ya wadau kulalamika idadi ya walioajiriwa kuwa siyo iliyotangazwa na serikali ikiwemo baadhi ya majina kujirudia mara nyingi, leo serikali imesema walioajiriwa ni 8,000 pekee. Idadi hii mpya iliyotangazwa ni pungufu ya watu 5,000 ya idadi iliyotajwa awali.

PIA, SOMA=> Madudu yaliyofanyika kwenye ajira za Ualimu zilizotangazwa. Jina la 'ABADALLAH LEONARD SHONDE S3630-0099/2013' lajirudia mara 196
Mimi niko tofauti Sana, na izo ajira, mfano iyo idadi kila mmoja angepewa m 5 na kila mmoja azirudishe ndani ya miaka mitano bila riba, ndani ya miaka mitano wangefanya mahajabu,ajira ni utumwa wa fukra, wawezeshe watu wapambane na fulsa mbali mbali.

Mtaji wa ml tano mtu hawezi kosa Cha kufanya kuweza ingiza elfu 40 kila siku hivyo
Chukua 40×30= 1.2m
1.2×12=14.4 per year
14.4m×5yrs =almost 72 m
Wakati mshahara wa ualim
Ametengeneza pesa nyingi kwa miaka mitano sidhani Kama hata 30m inafika,
 
Maelezo kuhusu hiyo elfu5 pungufu yakoje?

Naona kabisa kuna mtu ameshapoteza kibarua pale TAMISEMI 😎
Huwez kuwalaumu Tamisemi wakati maelekezo yote yametoka juu , sema wananchi mmelivalia njuga maagizo yakatoka juu tena kuwaweka Sawa na awamu ya pili fake ..... Kimsingi kila sintofahamu iliyopo kwenye hzo ajira ina baraka zote , na walioajiliwa hawazidi 3000 hata hao 8000 kuna majina hewa zaidi ya buku dansi.....hata hvyo hali ikiwa mbaya kuna mmoja au wawili wanaweza tolewa kafara na badae wakaajiriwa tena kimya kimya hata BOT huko au wizara/Ofisi nyingine..
 
Back
Top Bottom