Serikali: Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi walioajiriwa ni elfu nane pekee

Serikali: Walimu wa Shule za Sekondari na Msingi walioajiriwa ni elfu nane pekee

NOTE: Mods msiunganishe huu uzi kuna hoja zinahitaji kujibiwa.

Kwanza naomba nianze kwa kutoa masikitiko yangu juu ya wizara ya Tamisemi.

Tamisemi ipo chini ya ofisi ya Rais kwa maana hiyo ndicho kioo cha Rais. Wizara ikiboronga maana yake inamchafua Rais na ikifanya vizuri na Rais anakuwa amefanya vizuri.

Kwahiyo, Kitendo cha katibu mkuu kutoa majibu mapesi kwenye hoja nzito zilizo ibuliwa na wadau kuhusu madudu kwenye ajira za ualimu ni kitendo kinacho tia mashaka juu ya weledi wa watendaji katika hiyo wizara.
Hili pia naomba mheshimiwa Rais aliangalie kama ikimpendeza kwenye baraza jipya la mawaziri atakaloteua, hii wizara ipewe waziri mwingine. Hii itasaidia kuwepo kwa uwajibikaji na kuepusha tabia ya watendaji kufanya kazi kwa mazoea.

Sasa Turudi kwenye mjadala wetu wa majibu ya tamisemi kutolea ufafanuzi wa madudu kwenye ajira za walimu. Press conference hiyo ya kujibu madudu ili hudhuriwa na makatibu wakuu watatu siku ya jana.
1. Eng. Joseph Nyamhanga- katibu mkuu tamisemi
2. Dkt. Laurean Ndumbaro- katibu mkuu utumishi
3. Dkt. Leonard Akwilapo- katibu mkuu wizara ya elimu.

1. HOJA YA KWANZA: kuhusu jina la ABDALLAH SHONDE kujirudia mara 196.
-katika kutetea hoja hiyo, katibu mkuu alisema hilo jina kujirudia halikuongeza idadi wala kupunguza ajira za walimu wengine bali iliongeza wingi wa majina tu. Hapa naomba aliyemwelewa katibu mkuu anifafanulie. Na kufuatia utetezi huo naomba nimuulize katibu mkuu swali moja;
(i) kama jina hilo kujirudia kila ukurasa halikuwa na madhara. Kwanini mlifanyia marekebisho na baada ya marekebisho hayo baadhi ya majina mapya ya walimu wakaongezewa na kurasa za majina kuongezeka toka kurasa 196 hadi kurasa 197?

HOJA YA PILI: kuhusu waliomaliza kidato cha nne 2019
- katika utetezi wake katibu mkuu alidai wamepitia majina hayo upya na kubaini kuwa walimaliza kidato cha nne 2013.
Utetezi huo wa katibu ni dhaifu kwa sababu zifuatazo;

(i) katibu mkuu hakuwa na uhakika wa kulithibitisha hilo hivyo aliishia kutoa ufafanuzi kwa hisia na kubahatisha. Ili kuthibitisha ninacho kisema nimefanya uchunguzi wa matokeo ya walimu watatu wenye index za kidato cha nne za 2019 na kubaini yafuatayo;
(a) WINNIE ELIAS MBISE
-huyu ametumia index: S0687-0124/2019. kutokana na kauli ya katibu mkuu kuwa wenye hizi index za 2019 wamemaliza 2013 nimefanya utafiti mdogo wa matokeo ya mwanafunzi huyu kwa mwaka 2013 kwa kutumia index:S0687-0124/2013) nimegundua kuwa shule aliyohitimu inaitwa KIKATITI SECONDARY na kwa mwaka huo ni watahiniwa 116 tu waliokuwa wamesajiliwa kufanya mitihani na hivyo namba ya mtahiniwa wa mwisho ilikuwa S0687-0116/2013. Je, hii index: S0687-0124/2013 ambayo katibu anataka kutuaminisha inatoka wapi?

(b) BAKARI LAUZI BAKARI
-huyu ametumia index: S3678-0064/2019. Kwa mujibu wa maelezo ya katibu mkuu kuwa wamemaliza 2013, nilipofuatilia matokeo ya index hiyo kwa mwaka 2013 nimegundua kuwa mwalimu mwenye namba hiyo (S3678-0064/2013) alipata divisheni sifuri. Kutokana na matokeo hayo, je katibu mkuu anakubaliana na mimi kwamba wameajiri mwalimu aliyepata divisheni zero kidato cha nne?
(c) DAVID LAMECK NDOSSA
- huyu ametumia index: S1943-0147/2019 ameajiriwa kama fundi sanifu wa maabara. Lakini kwakuwa katibu mkuu alisema wamemaliza 2013 nilipofuatilia matokeo yake nimegundua kuwa mtahiniwa mwenye namba hiyo (S1943-0147/2013) alipata F ya biology na wala hakusoma somo la fizikia au kemia. Kutokana na matokeo hayo, je katibu mkuu anakubaliana na mimi kwamba wameajiri mtu ambaye hakusoma masomo ya sayansi kwenda kufundisha practicals?

(ii) utetezi wa katibu mkuu ni dhaifu kwa sababu siku ya kutangaza ajira alisema moja ya kigezo cha kuwapangia watu ajira walizingatia ulinganifu wa taarifa zilizopo kwenye vyeti na taarifa zilizojazwa kwenye mfumo. Kama kweli walizingatia ulinganifu huo, kwanini wameajiri walimu ambao taarifa zao za kwenye mfumo haziendani na taarifa zilizopo kwenye vyeti mfano hawa wenye index za 2019?

(iii) utetezi wa katibu mkuu ni dhaifu kwa sababu mfumo ulikuwa na uwezo wa kuthibitisha index za waombaji. Katika kuthibitisha hilo nanukuu sehemu ya maelezo yaliyokuwepo kwenye mfumo " Your form four index number and any other used certificate should be valid as they will be verified before you are selected. Invalid number will lead to rejection of your application". Kama mfumo uliweza kutambua index za waombaji kwanini watu wenye index zenye utata wameajiriwa?. Katika hili usikimbilie kwenye kichaka cha matatizo ya kwenye mfumo kwa sababu majina ya waombaji mlikaa nayo kwa zaidi ya mwezi mmoja na mlifanya zoezi kwa umakini kwa kuzingatia ulinganifu wa taarifa.

Pia kufuatia utetezi huo naomba katibu mkuu atoe ufafanuzi wa walimu walio ajiriwa kwa namba hizi za kidato cha nne;
(i) S0660-0541/2019
(ii) S0566-1215/2019
(iii) S0151-0785/2015
(iv) S1380-1058/2019
(v)S1380-0852/2019
(vi) S0440-0963/2019

(a)katibu mkuu atwambie majina ya shule ya center namba zilizo tumika kwenye hizo index na ni shule gani hizo amabazo wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wanahitimu ndani ya mwaka mmoja kwa idadi kubwa hiyo ya 800+, 900+ na 1000+

(b) katibu mkuu aseme kwanini waajiriwa hao namba zao za kidato cha nne hazitambuliki na baraza la mitihani(NECTA)


HOJA YA TATU: kuhusu idadi ya ajira
Katika kujitetea katibu mkuu amekiri wazi ya kuwa ajira zilizotolewa siyo 13000 bali ni ajira 8000. Sasa najiuliza siku zilipotangazwa katibu mkuu alisema ni ajira 13000 alidanganya umma kwa maslahi ya nani na je, hiyo ndio ilikuwa ahadi ya Rais Magufuri kuajiri walimu 8000?

Katika press conference hiyo, katibu mkuu amekwepa kujibu madudu ya kuajiri walimu waliotumia namba za wanafunzi wa kidato cha tano wanaoendelea na masomo. Hili nalo linahitaji ufafanuzi

Mwisho, kutokana na utetezi mwepesi uliotolewa na katibu siku ya jana tunaomba tamisemi ijipange upya ije na utetezi ulioshiba na wenye uthibitisho wa majibu ya madudu yote usio na mashaka au watoe orodha mpya ya majina ambayo madudu yote yaliyoibuliwa yawe yamefanyiwa kazi
 
Kwa uzembe wakijinga Kama huu Hao viongozi wajihuzulu, zoezi lilijaa rushwa ,huyo Katibu kaongea juu juu huku akidai watu walioomba walikosea na zoezi halitarudiwa........! ,zoezi hilo lifanyiwe tathmini wizara nyeti Kama hii yenye kusimamia na wasomi haiwezi kufanya mambo yakijinga bila kuwajibishwa....!
 
Ndumbaro acha upumbavu wa kina ndugai na mahera. Tangazo la ajira lilikuwa walimu 13,000. Baada ya wananchi kuona mapungufu makubwa kwenye orodha yenu ya waajiriwa ndiyo unakuja na usanii wa kijinga eti eti hii ni awamu ya kwanza ya walimu 8000. Wengine 5000 itakuwa awamu ya pili. Bila ya kukosolewa haya maelezo ungetoa ahera? Kwa taarifa yako hata awamu hii ya kwanza hawajafikia idadi ya 8000. Majina wamejirudiarudia na wengine hawana sifa.bHivi ujinga huu mtaacha lini? Wote mmekuwa watu wa kuokotwa majalalani? Serikali gani hii?
Nenda tena tamisemi kasome tangazo lao naona umeandika kwa mihemko sana.
 
Mimi niko tofauti Sana, na izo ajira, mfano iyo idadi kila mmoja angepewa m 5 na kila mmoja azirudishe ndani ya miaka mitano bila riba, ndani ya miaka mitano wangefanya mahajabu,ajira ni utumwa wa fukra, wawezeshe watu wapambane na fulsa mbali mbali.

Mtaji wa ml tano mtu hawezi kosa Cha kufanya kuweza ingiza elfu 40 kila siku hivyo
Chukua 40×30= 1.2m
1.2×12=14.4 per year
14.4m×5yrs =almost 72 m
Wakati mshahara wa ualim
Ametengeneza pesa nyingi kwa miaka mitano sidhani Kama hata 30m inafika,
Watu mkiwa nje mnaona poa sana......kwa siku watu tunatoka hata hatujauza na ni biashara za uhakika.
 
Swali gum mkuu, Sina jibu, waliokua kwenye serikali zao wanawaza tujuza, na nakubali kabisa kipindi hicho nafasi za kazi zilikuwa nyingi, KWA waliokua na uhitaji wa kufanya kazi serikalini, wengi walikua wanazikimbia kwenda secta binfsi kutokana na malipo,KWA Sasa kote kumebana,
Acha nikwambie kutokana na kuongezeka kwa uandikishaji wa wanafunzi drs la 1 na kidato Cha Kwanza TZ kuna uhaba was walimu zaidi ya 40% Kama hujui ndo nakujuza. Serikali haiajiri kwa kuwa elimu sio kipaumbele chake kwa Sasa. Nikifikiriaga chozi huwa linanitoka.
 
Back
Top Bottom