Miss Judith.asilimia 4.5 kwa zanzibar ni kubwa sana ukizingatia uwiano wa idadi ya watu. kama watu 1m wanapata 4.5% na watu 43m wa nchi ileile wanabaki na 95.5% tu, kwa kweli hiyo si haki kabisa
halafu hilo la kudhaminiwa na serikali ya muungano, maana yake nchi ya zanzibar ikikataa kulipa, itailazimu nchi ta tamzania (bara) kubeba mzigo huo! hapa nahisi matope yalichukua nafasi ya ubongo ndani ya vichwa vilivyofikia uamuzi huu. kwa kweli maamuzi kama haya ndiyo yataharakisha kuvunjika kwa muungano huu
Mimi pia sioni sababu ya Muungano kuwepo kama unatutia hasara.
Tanganyika hautakiwi na Zanzibar hautakiwi....huu ni muungano wa viongozi tu.
Mimi nahisi umepiga mahesabu vibaya hapa.
Ungepiga mahesabu ya kibenki ungefahamu kuwa 4.5 ni ndogo sana kwa kuipatia nchi mshirika wa muungano.Regardless ya wingi au udogo ya wakaazi wake.
Ukienda benki kuweka akiba yako, benki inakupa riba.wakikupa 4.5%, wao huwa wanapata ngapi?
Siku mahesabu yakiwekwa wazi ndio tutajua kama hii biashara ina faida au haina.
Nafikiri ndio sababu viongozi wetu hawataki hata tuujadili.
Kama zilivyo rasilimali za TZ kuwa hazimsaidii mwananchi, na huu Muungano pia. Ni mtaji wa wajanja wachache tu.
Hata hivyo tuendelee kudai watuoneshe mapato na matumizi ya Muungano.
Kila kitu hapa TZ ni siri ya serikali.
Ama la kuwadhamini Zanzibar ni wazi kuwa viongozi wanaona ipo faida ya kufanya hivyo. kama kweli tunawabeba hawa na ni mzigo, basi tungewaacha wakajiondokea. wangejitafutia misaada bila ya udhamini wetu....bado nashawishika kuwa kuna siri kubwa ambayo watawala wetu hawataki sisi tuijue.
Mbona East African community ile ya mwanzo tulijitoa/tuliivunja tulipoona haina faida kwetu?