Serikali wapeni nguvu Usalama wa Taifa wazuie uovu NIDA na wimbi la wahamiaji haramu

Serikali wapeni nguvu Usalama wa Taifa wazuie uovu NIDA na wimbi la wahamiaji haramu

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Nchi hii hasa serikali na mamlaka zake Mungu anawaona, naandika nikiwa na hasira sio NIDA wala Uhamiaji, au Polisi kote kumeoza.

Wahamiaji haramu wametapakaa sio kwenye bar, shambani, kwa house girls, vibarua wa kufuga mbuzi, nguruwe, kuku ambao wako nchini kwenye maeneo mbalimbali wasio na vibali, wenye vibali feki, wenye Vitambulisho vya NIDA.

Napata hofu kubwa, naiona Boko Haram, naiona ISIS, naona Tawi la ADF nyakati fupi zijazo. Kwanini tuwe hivi kama taifa? Watu wengi, mamilioni hawana ajira, hali ni mbaya sana, ni nyakati za utawala kuwa macho na madhubuti kwenye mambo msingi kwenye ulinzi na usalama.

Hii ni mara ya mwisho sitaonya wala kushauri tena.

👍👍👍
Wadiz
 
Tatizo mkuu na hao TISS wakipewa meno, wanaweza fanya mazito kuliko tunavowategemea. Ngozi nyeusi huwa tuna shida sana mkuu.
Bora wabebe lawama hao kuliko hao vilaza waliopo maeneo hayo.
 
Inauma sana mwaka wa tano huu nanyimwa kitambulisho kwamba taarufa sio sahihi wakati kuna msomali anamiliki Nida wakati hta kaburi la baba yake hajui lilipo
 
Back
Top Bottom