Serikali wekeni Tozo kwenye Betting kupata pesa ya kujengea viwanja na kuendeleza michezo nchini

The Sunk Cost Fallacy

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
19,582
Reaction score
14,167
Michezo ni sekta rasmi kama sekta zingine inatakiwa ichangie Pato la Taifa na itoe ajira na burudani pia.

Ni aibu kwa Nchi kubwa kama Tanzania yenye washabiki wengi wa mpira na wacheza kamali yaani betting wa kuyosha kushindwa kuwa na viwanja vya kisasa vya michezo (sports complex) walau Kimoja kila Kanda.

Yaani tunazidiwa na vinchi vya ajabu ajabu na maskini kama Cameron, Ghana, Mauritania nk.

Kwa kuwa betting ni starehe kama starehe zingine wekeni Tozo kwa kila Shilingi inayotumika kwenye betting ambayo itaingia kwenye Mfuko wa kuendeleza michezo Tanzania, na moja ya activity zake iwe ni kujenga miundombinu ya michezo ya aina zote ya kisasa hasa sports complex na arena, walau tuwe navyo kila kanda.

Pili makampuni ya betting yanatakiwa kisheria kuchangia mfuko huo na pia kuyalazimisha kuwa wafadhili wa timu, pia nao lazima wachangie kwenye Mfuko huo on top of Kodi wanayolipa.

Tukienda hivyo itasaidia kuinua michezo yetu na kuifanya biashara rasmi,pia tutaweza kuandaa mashindano makubwa kama Afcon, CHan, All Africa Games nk.
 
Yaani kwa cerebral yako unafikiri betting ni mpira tu? Na unajua kuna kodi ngapi zinakatwa hapo? Shauri serikali itafute establishment ya vyanzo vipya vya mapato na sio kung’ang’ania biashara zenye zko established.
 
Achana na Kodi ya kawaida inayokatwa kwa.kampuni na mtu akishinda,iwekwe tozo kokote kwenye betting Ili kusaidia michezo.

Pesa hiyo ni ya starehe kama pombe watu wako addicted so hiyo ni sehemu nzuri ya kupata pesa ya kuendelezea michezo na kujenga viwanja.
 
Hapa ndio vijana wengi wamejiajiri. waweke tozo kwenye viingilio vya mpira tusiohusika tuachwe
 
Viwanja ni kitu kidogo sana kwa serikali sema sio kipaombele tu kama inanunua ndege ya billion 600 hadi 900B, Inaweza kushindwa kujenga viwanja vya billion 30 au 60 hata 10 ?
 
Hivi unajua kwanini Betting haipigwi vita na Serikali na hata matangazo yanafanywa kila wakati ili kusajili wadau ?

Sababu Serikali ndio mnufaika mkubwa wa hii kitu, pamoja na makato yote kuna Tax on winning yaani kila mara mtu yoyote akishinda Serikali inakula 15%..., jambo ambalo nchi nyingine ukiondoa East Africa huo Ujangili haupo.., Na usiseme kwamba wameweka hii ili kusaidia jamii na gambling hilo sio kweli ingekuwa wana vituo vya addiction na hizo pesa kuzipeleka huko ningeelewa, ila hili wamelifanya kama mtaji..., jambo ambalo wewe unataka liendelee
 
Ni kweli ila sasa ni bora kutafuta pesa kwenye vyanzo vya anasa zikatumika kufanya maendeleo ya sekta za burudani kuliko kuchukua pesa kwenye vyanzo vya kawaida vya Kodi kujengea viwanja .
 
Hivi unajua kwanini Betting haipigwi vita na Serikali na hata matangazo yanafanywa kila wakati ili kusajili wadau ?

Sababu Serikali ndio mnufaika mkubwa wa hii kitu, pamoja na makato yote kuna Tax on winning yaani kila mara mtu yoyote akishinda Serikali inakula 15%..., jambo ambalo nchi nyingine ukiondoa East Africa huo Ujangili haupo.., Na usiseme kwamba wameweka hii ili kusaidia jamii na gambling hilo sio kweli ingekuwa wana vituo vya addiction na hizo pesa kuzipeleka huko ningeelewa, ila hili wamelifanya kama mtaji..., jambo ambalo wewe unataka liendelee
Ndio sio tuu liendelee bali liongesewe tozo ya kusaidia michezo.

Tax on winning ni sawa tuu na Kodi ya PAYE,hata ukiuza kiwanja,nyumba,gari nk nk unatakiwa TRA wachukue Chao.
 
Unaonaje tukimaliza huko tuingie na wauza madawa na mihadarati ili tupate pesa ya kujengea hospitali ?

Gambling is an addiction na kuweka hili kama chanzo cha mapato hakuna tofauti na kupata gawio kutoka Polisi au Traffic kwa kushika waalifu...

All in all tutafute vyanzo vingine sababu kwa vyanzo hivi ni sawasawa na kuombea watu wafe ili muuza majeneza apate wateja (Long term kama Taifa hasara ya hili jambo ni kubwa kuliko Faida) Kwahio hizo pesa wanazopata zitumike kutoa elimu ya addiction na kujaribu kupunguza waathirika...
 
Of course ,Dunia kote inafanyika hivyo including Uingereza.

Hii ni starehe lazima ichangie maendeleo ya sekta inayowanufaisha.
Ndio maana nakwambia tayari kuna Tozo / Kodi za kutosha..., tayari gambling Tanzania ni more expensive kuliko sehemu nyingine na hili halikufanywa ili watu waache betting bali ili Serikali ipate chakula....
 
Michezo ni sekta rasmi kama sekta zingine inatakiwa ichangie Pato la Taifa na itoe ajira na burudani pia.

Ni aibu kwa Nchi kubwa kama Tanzania yenye washabiki wengi wa mpira na wacheza kamali yaani betting wa kuyosha kushindwa kuwa na viwanja vya kisasa vya michezo (sports complex) walau Kimoja kila Kanda.

Yaani tunazidiwa na vinchi vya ajabu ajabu na maskini kama Cameron, Ghana, Mauritania nk.

Kwa kuwa betting ni starehe kama starehe zingine wekeni Tozo kwa kila Shilingi inayotumika kwenye betting ambayo itaingia kwenye Mfuko wa kuendeleza michezo Tanzania, na moja ya activity zake iwe ni kujenga miundombinu ya michezo ya aina zote ya kisasa hasa sports complex na arena, walau tuwe navyo kila kanda.

Pili makampuni ya betting yanatakiwa kisheria kuchangia mfuko huo na pia kuyalazimisha kuwa wafadhili wa timu, pia nao lazima wachangie kwenye Mfuko huo on top of Kodi wanayolipa.

Tukienda hivyo itasaidia kuinua michezo yetu na kuifanya biashara rasmi,pia tutaweza kuandaa mashindano makubwa kama Afcon, CHan, All Africa Games nk.
Una mawazo ya kipuuzi sana
 
Back
Top Bottom