Kidagaa kimemwozea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 3,680
- 6,554
Watanzania wote hatujui Kiingereza katika viwango vya 3.5-4 hii ni kutokana na kukaririshwa zaidi sarufi ya Kiingereza kuliko lugha yenyewe/mawasiliano.
Serikali inapaswa kugharamia waalimu wageni ambao watakuja kufundisha lugha ya kingereza kwa ufasaha ambapo watatumia mbinu za ufundishaji wa lugha ya kigeni.
Aidha syllabus ya kufundisha somo la kingereza ubadilishwe ili ilenge kumwezesha mwanafunzi kuzungumza Kiingereza kuliko kuijua sarufi ya kingereza. Hoja hii inapwewa mashiko na wataalam kama Martha Qorro ma na prof. F.E.M. K . senkorro.
Hakuna haja ya kuendelea kufundisha tena Kingereza kama somo la history au biology badala yake Kiingereza kifundishwe kama lugha kwa kutumia mbinu za kufundisha lugha ya kigeni.
Hii itasaidia kupata Watanzania wanaojua kingereza kuliko hawa tulionao wanaodhani wanajua Ila kiuhalisia ukiwasikiliza wakiongea wanaongea kama Kitabu, lugha ya kiuandishi. Aka Kingereza cha kitabuni.
Rai yangu ni kuwa serikali tafuteni waalimu wa kingereza wazawa wa lugha yenyewe kwaajili ya kufundisha Watanzania lugha ya Kingereza.