Serikali ya Bulgaria yajiuzulu baada ya wananchi kuandamana kupinga Rushwa

Serikali ya Bulgaria yajiuzulu baada ya wananchi kuandamana kupinga Rushwa

Wenzetu uongozi ni sehemu ya kutumikia watu kwa dhati sio sehemu ya kujilimbikizia mali za umma kwa msaada wa katiba na vyombo vya ulinzi.

In short wenzetu kila mtu anabeba msalaba wake.
Na wanajua wajibikaji, wala hawaogopi kuwajibika, sasa njoo Afrika uone maajabu ya chaguo la Mungu. Nakusingizia mabeberu kwa hoja nyepesi nyepesi.
 
Bongo, Mwingine anasema, Hata nchi nyingine zinafanya kama sisi, tulivyofanya kulinda nchi.
 
Vipi huko Wamechoma Moto vituo vya daladala na Mabus?VP Kuhusu kuiba maduka ya Watu yamevunjwa huko Bulgaria?,kuchomea Watu nyumba zao je?
Hakuna haja ya kuchoma vitu ili kuonyesha hisia zenu ikiwa uhuru wenu wa kutoa maoni na kukosoa haujakandamizwa, lakini ukute kufanya tu maandamano ya amani hamruhusiwi, na hapo ukikosoa unatekwa, vyombo vya habari havina uhuru, vyama vya upinzani vinazuiliwa kufanya shughuli zake za kisiasa na viongozi wake wanakamatwa wapo jela, mitandao ya kijamii inafungiwa.

Hapo hakuna pa kutokea ndipo inajenga hasira na kufikia kuchoma vitu ili kuonyesha hisia zenu ila a pia bado ukichoma hivyo vitu unaambiwa unataka kupindua serikali kisa ni kuchoma moto vitu na kuiba mali za watu binafsi hivyo unamiminiwa shaba maana huko ni kupindua nchi.
 
FB_IMG_1765504992884.jpg
kwetu
 
Wanaojielewa hao wanaachia wengine wanakuja maisha yanaendelea,kwetu wanakuua ukipona wanakuuzia uhaini, in Africa nimeamini wengi bado level ya nyani ubinadamu bado
Huku kiongozi ambaye yupo hapo kwa ajiri ya hao wananchi anawaambia hao hao wananchi kuwa kama hamnipendi subirini hadi muda wangu uishe ndio mumeweke mnaemtaka.
 
Mmeona hiyo idadi ya watu?

Hiyo idadi hakuna cha polisi wala jeshi la Tanzania linaloweza kukabiliana nayo.

Hapo ndo siri ilipo.
Ila kama jeshi lingeziba njia na kuwa wapo teyari kupiga shaba ukisogea sidhani kama wangefikia hivyo.
 
Kwani Bulgaria nao walifungia mitandao ya kijamii? Waliteka wakosoaji na kuwauwa?
Mkosoaji gani tz alitekwa na kuuawa?.. vurugu na uhalifu mliofanya ni kwa kuwa mitandao ilifungwa au kudai mabadiliko ya katiba?..mnajua hata mnachokitaka?
 
Bulgaria wamechoma moto miundombinu,sheli na mali za watu,wameua askari?..ukitaka mtazamwe tu mpindue?
Inaonekana huna mchango wala maana yoyote katika Taifa hili, watu wakichoshwa na serikali dhalimu ni muhimu wakajitoa mapema bila shinikizo, lakini wanapokaidi matakwa ya wananchi ndipo yanatokea ya kutokea wanaanza kufyeka raia kwa mtutu wa bunduki.
 
Inaonekana huna mchango wala maana yoyote katika Taifa hili, watu wakichoshwa na serikali dhalimu ni muhimu wakajitoa mapema bila shinikizo, lakini wanapokaidi matakwa ya wananchi ndipo yanatokea ya kutokea wanaanza kufyeka raia kwa mtutu wa bunduki.
Matakwa ya wananchi au ya wahuni tu wakiongozwa na chuki za kidini walizojazwa na viongozi wao!?
 
Njoo Afrika sasa, ndio maana trump alituita shithole countries, samia and Co wanangangania ofisi hata kama umma hauwataki, wanazidi kuifuja nchi na kuiibia.
 
Mkosoaji gani tz alitekwa na kuuawa?.. vurugu na uhalifu mliofanya ni kwa kuwa mitandao ilifungwa au kudai mabadiliko ya katiba?..mnajua hata mnachokitaka?
Kwamba haujui kuwa Tanzania kuna utekaji na watekaji hawakamatwi wanaishia kuitwa wasiojulikana? Wakina Mdude, Polepole n.k

Ukiacha kutekwa na wasiojulikana kuna kukamatwa na polisi kwa katika hali ambayo ni kinyume na sheria na hadi Simbachawene kalizungumzia kwamba mtu akaongea tu kitu kidogo anavamiwa na mapolisi na mabunduki huku wameficha nyuso zao na kipondo juu.

Nani asiyejua Tanzania hii kuwa ukiwa unakosoa kosoa serikali unajiweka hatarini kutekwa ama kuuwawa?

Halafu katika mazingira hayo bado serikali inafungia mitandao ya kijamii ambako ndipo wananchi wanatoa madukuduku yao, mfano halisi hii Jamiiforums ambayo hata wewe unatumia hapa.

Sasa haya yote huko Bulgaria yapo? Au unadhani hicho walichokifanya wananchi wa huko serikali ya Tanzania ingeruhusu?
 
Back
Top Bottom