Rais Kikwete ndiye rais aliyekuwa akisikiliza kelele za wapinzani. Walikuwa wakisema anawaita ikulu kwa ajili ya mashauriano na kutafuta suluhu.
Rais Magufuli alipoingia madarakani, alitangaza hadharani kabisa akasema "mimi huwa sishauriki na huwa sipangiwi. Tena ukinishauri ndiyo unaharibu kabisa".
Naye mama Samia alianza kwa mtindo wa Kikwete lkn baadaye akageuka. Kwenye sakata la DP World akasema "nanyamaza, sitaufungua mdomo wangu". Na hivi karibuni ndiyo amonesha rangi yake halisi kwa kuutangazia umma na kusema "mimi ni chura kiziwi". Akimanisha kuwa hasikilizi la maamuma wala la mnadi swala.
Leo Mbowe kaandaa nondo zake nzuri kabisa za kuishauri serikali ya rais Samia. Lkn binafsi naona kama Mbowe kajichosha tu.
Kwasababu, baada ya kifo cha rais Magufuli Mbowe alilaani sana mauaji, utekaji na uporaji uliokuwa ukifanywa na utawala awamu ya tano. Mbowe akashauri kuwa kamwe, na kamwe tena mambo yale yasijirudie (never and never again)
Je, kinachoendelea hivi sasa nchini kinatofuti na kile cha awamu ya Tano?
Ndiyo kusema ushauri wa Mbowe wa baada ya kifo cha Magufuli ulipuuzwa, na hata huu wa leo utapuuzwa pia.