WOWOWO
JF-Expert Member
- Aug 3, 2011
- 599
- 456
Mwaka 2014 na Mwaka 2015 Chama cha Mapinduzi (CCM) kilikuwa kimeingia rasmi kipindi cha kuanguka na kutoweka katika medani za siasa. Matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, mtawalia pamoja na kuhujumiwa sana, yalionesha wazi kushindwa vibaya kwa CCM na kama isingekuwa “kitengo” kufanya kazi yake basi CCM ingekuwa historia.
Kimsingi vyombo vya dola (Hapa ieleweke Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa-TISS) toka wakati huo ndiyo vimejigeuza kuwa CCM. Oganaizesheni na ushawishi wa CCM vimekufa rasmi, kilichobaki ni instruments za vyombo hivi ambavyo kikatiba vinapaswa kuwa ‘politically impartial and disengaged’. Vinapaswa kuwa tayari kusimamia katiba na kuhakikisha maslahi ya Taifa na matakwa ya wananchi yanalindwa na kuakisiwa kila wakati.
Kuanzia kipindi hicho, ilieleweka na kuwa wazi rasmi kuwa CCM hakiwezi kushinda uchaguzi tena wowote kama utaachwa ufanyike kwa uwazi, safi, salama na kwa amani. Ilibainika kwamba, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ndicho kilishinda na kwa umaarufu wake ndicho chama cha kizazi cha sasa. Sasa nini CCM na dola iliamua kuanzia wakati huo?
Wakatabzabu, WOWOWO…

- Hakuna uchaguzi wowote kuachwa ufanyike kwa haki, uwazi na amani, ikiwa ni pamoja na kutoruhusu opposition voices kwenye siasa na state leadership. Hapa ni kwa miongo kadhaa ili ‘kuua’ political generation ya sasa, kupitia waliopo kuzeeka na wanaobaki kupoteza popularity. Kwa sasa imepotea miaka 10. Ikifika 2030 ni 15, 2035 ni 20. Umri na generation matters here.
- Kuzuia political activism mashuleni na kwa vijana ibuka. Hii inafanywa kwa lengo la kuua generational link. Inakwenda sambamba na kuzuia siasa vyuoni, kufukuza wanaojihusisha na wale wanaoibuka kutishwa au kupotezwa kabisa. Deus Soka na wenzake ni mfano.
- Kuharamisha shughuli za siasa za upinzani na uanaharakati na kuwavika uharamu na ujinai wale wote wanaojihusisha. Hii ni kazi inayofanywa na Jeshi la Polisi na TISS zaidi. Kwamba kila kunapotokea political oppression au hata utekaji na mauaji yao vyombo hivi haraka huhakikisha wakandamizwaji wanavishwa uharamu na ujinai. Kujenga picha ya ki-generation(generational imagination) kwamba shughuli hizo ni haramu na wanaozifanya wanastahili wanayoyapitia.
- Katika uharamishaji huu, CCM imesimama katika kujiingiza kikamilifu kwenye siasa za watoto na vijana wa mashuleni. Kujenga kizazi cha baadaye kulichopumbazika na kuwa indoctrinated na upuuzi, huku ikiharamisha actors wengine kufanya activism. Hapa utaona ni mkakati ulio dhahiri.
- Kujenga mazingira ya lawlessness, impunity na unconstitutionality bila accountability. Hii ni kama transitional state ambayo wametengeneza ili kutengeneza cover up kwa yeyote anayesaidia misheni yao ya “generational transition”. Hapa hautaona kukemea au hatua yotote dhidhi ya kiumbe yeyote anayetekeleza misheni hiyo pana. Actually, there is reward. Makonda’s comeback ni somo kuu.
- Kwakuwa msingi wa vyombo vya dola na utawala wa nchi umejengwa katika maslahi ya kujaza mifuko binafsi ya “wachache” na umma umelala usingizi wa pono, basi misheni hii wameipa uhakika wa 100% kutimia in 2035. Hawa wachache, wenye kunemeeka na mifumo wanaanda watoto na vijana wao kuendeleza wanapoishia. Kwahiyo, Wokovu pekee ni waliowengi, ambao wanaendelea kufukarishwa na kutwezwa kuamka na kusema hapana. Hili kama halitatokea na kuungwa mkono na wazalendo ndani ya mfumo uliooza wa CCM na wale walioko kwenye vyombo vya dola hususan TISS na JWTZ basi nchi iko kwenye kasi ya kupoteza utaifa na kuwa genge.
Wakatabzabu, WOWOWO…