The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kazi ya kilimo ni kazi ngumu sana isiyo na staha tena yenye jina baya kwani hunasibishwa na umaskini, yenye karaha nyingi na risk factors za kutosha.
Mbaya sana ndiyo kazi inayoajiri zaidi ya 70% ya watanzania kwa uhakika. Hivyo kuchezea kilimo ni kuchezea maisha ya watanzania na kutotendea haki kilimo ni kuwanyonya wakulima wa Tanzania kwa makusudi kabisa. Yaani kupuuza kero za kilimo ni kama mauaji ya kukusudia ya wakulima wetu.
Nakumbuka mheshimiwa bashe alipochukua kuongoza wizara ya kilimo alikuja na slogan yake kwamba mazao ya mkulima sio mali ya umma. Alisema hivi akipinga utaratibu wa kuzuia mkulima kuuza mazao kokote anakopata bei nzuri. Niliposikia Ile kauli nikadhani labda ni mwanzo mpya wa kuwa kumbuka wakulima wa kitanzania.
Bahati mbaya hakufika mbali na hiyo kauli yake ikapinduliwa na wananchi wakazuiwa kuuza mazao nje kwa kisingizio cha tishio la njaa.
Tishio la njaa limeisha soko la nataka limekufa bei ya mazao haiendani kabisa na gharama za uzalishaji na kupambana na athari za mfumuko wa bei ambao pia serikali imeshindwa kuudhibiti.
Alafu rais anakuja na tangazo jepesi tu eti mahindi nunueni shs 700. alafu kina mwashambwa wanashangilia.
Nani alimtuma kuzuia kuuza nje ili wakulima wapate bei nzuri!?
Nani atafidia hasara ya wakulima inayotokana na kuuza bei ndogo!?
Niwaombe ccm badilikeni!!
Msiwafanye vijana wa kitanzania waendelee kukichukia kilimo.