eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,356
- 16,379
Hivi, serikali inayowajali watu inaowaongoza na kuwasimamia, kweli inakosa mbinu za kuhakikisha bidhaa muhimu kama mafuta ya kupikia inashuka bei ili kupunguza gharama za maisha? Sababu kuu ya kupanda kwa gharama za vyakula mitaani ni mafuta ya kupikia kuwa juu mno.
Kwa mfano, maeneo ya mama ntilie na baba ntilie kwenye mitaa yetu tunayoishi, bei za chakula zimefikia:
• Wali na samaki: 3,000
• Ugali na mboga: 3,000
• Pilau na mboga: 3,000
• Wali maharage (chakula pendwa): 2,500
• Chipsi kavu: 2,500
• Chapati: 500-700
Tatizo si gharama za viambato vingine vinavyotumika kuandaa vyakula hivi, bali ni mafuta ya kupikia ambayo yako juu mno. Serikali, tusaidieni wananchi wa kawaida kama kweli mnatujali. Kwa hali kama hii, itafika mahali tutabaki kuweka chumvi tu badala ya mafuta.
Soma: Asante Serikali ya CCM kwa kupunguza bei ya Vinywaji, punguzeni na bei ya mafuta