Kikwete wetu na Basil Pesambili Mramba!
Johnson Mbwambo
Septemba 22, 2010
WAPENDWA, leo, nimeshawishika kuandika rejeo (rejoinder) kuhusu makala iliyoandikwa na Msomaji Raia katika toleo la gazeti hili, wiki iliyopita, ukurasa wa 10, yenye kichwa cha habari: Rais Kikwete msahaulifu au mzembe?
Msomaji Raia alichagua kichwa cha habari chenye swali. Angeweza kuchagua kichwa cha habari hicho hicho bila ya kuweka alama ya kuuliza, lakini hakuchagua kufanya hivyo. Nadhani aliamua kumalizia kwa alama ya kuuliza ili kukwepa kuhukumu, na badala yake kumuachia msomaji aamue mwenyewe kama Rais Kikwete ni msahaulifu au ni mzembe.
Ingawa simfahamu Kikwete kwa karibu kama Msomaji Raia, lakini hata mimi nahangaishwa na kutafuta jibu la swali hilo hilo: Je, tatizo la Kikwete ni usahaulifu au ana tatizo jingine kubwa zaidi?
Yawezekanaje (kama alivyobainisha Msomaji Raia) Kikwete atoe tamko thabiti kwa Watanzania kwamba urais wake hauna ubia na mtu mwingine yeyote, na kisha miaka mitano baadaye rais huyo huyo awe na ujasiri wa kuuambia tena umma wa Watanzania kwamba urais ni suala la kifamilia? Yawezekana aliisahau kauli yake hiyo ya mwanzo?
Kwa hakika, ukitaka kuandika kauli ambazo Kikwete alipata kuzitoa na baadaye akatoa nyingine kinyume kabisa na zile za mwanzo, au hatua alizochukua na baadaye akafanya kinyume chake, unaweza kujaza kitabu kizima.
Chukulia, kwa mfano, tukio la wiki iliyopita la huko Rombo ambako alijipa ujasiri kupanda jukwaani na kuwasihi wana-Rombo wamchague tena Basil Pesambili Mramba kuwa mbunge wao kwa kipindi kingine cha miaka mitano kwa kuwa ni mbunge safi, na kummwagia sifa kemkem.
Akiwa ameunyanyua juu mkono wa Mramba, Rais Jakaya Kikwete alisema hivi kuhusu mgombea ubunge huyo wa CCM: Huyu kwa maneno ya mjini ni mzee kijana kwani ni mwenye mawazo mapya yenye manufaa wakati wote siyo wale wazee ambao wakichoka la mbele linawekwa nyuma na la nyuma linawekwa mbele. Huyu ubongo wake unajadidika, ni chimbuko la maarifa mapya (rejea blogu ya kampeni za CCM inayoitwa Chagua Kikwete 2010 ambayo anuani yake ni jakayakikwete2010.blogspot.com).
Tukio hilo la Rais Kikwete kumnadi Mramba kwa kummwagia sifa kemkem liliibua maswali mengi kichwani mwangu; hasa nikikumbuka kwamba ni Kikwete huyo huyo ambaye aliidhinisha Basil Pesambili Mramba apelekwe mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi. Je, yawezekana Rais Kikwete amelisahau hilo au rais wetu ana tatizo jingine kubwa zaidi? Jibu unalo wewe msomaji.
Source raiamwema :Kikwete wetu na Basil Pesambili Mramba!
Novemba 23, 2008, Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona walifikishwa mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Kufikishwa kizimbani wakati ule kwa mawaziri hao wawili wa zamani kuliashiria mwanzo wa utekelezaji wa ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na Serikali ya Kikwete kuwa itawashughulikia vigogo wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi baada ya wananchi wengi kutoridhishwa na ukubwa wa majina ya watu walioshitakiwa katika kesi ya ufisadi ya EPA.
Ingawa katika mahojiano ambayo Kikwete aliyafanya na Tido Mhando na kurushwa na TBC (mwaka jana) aliahidi kwamba vigogo wengine watatu wangefikishwa mahakamani karibuni, sote tunajua kwamba mpaka leo hakuna kigogo mwingine aliyefikishwa mahakamani, na hivyo Basil Pesambili Mramba na Daniel Yona wanabakia kuwa vigogo pekee waliofikishwa mahakamani mpaka sasa.
Hivyo; inapotokea (kama ilivyotokea wiki iliyopita) Rais Kikwete anasimama jukwaani na kuwasihi wana-Rombo wamchague tena Basil Pesambili Mramba kuwa mbunge wao kwa kuwa ni kiongozi safi, inatuacha sote midomo wazi kwa mshangao.
Je, amesahau kuwa serikali yake imemfikisha Mramba mahakamani kwa tuhuma za ufisadi, na kesi bado inanguruma Mahakama Kuu? Ni kusahau tu au rais wetu ana tatizo jingine kubwa zaidi?
Lakini kuna upande wa pili wa shilingi wa kauli yake hiyo aliyoitoa Rombo kuhusu Basil Pesambili Mramba. Je, Mahakama Kuu inaweza bado kuendelea na kesi hiyo na kutoa hukumu ya haki; ilhali mkuu wa nchi (ambaye yu juu ya sheria) tayari ameshamsafisha hadharani Basil Pesambili Mramba kuwa ni mtu safi?
Je, Mahakama Kuu ambayo majaji wake huteuliwa na Rais, inaweza kuwa na ujasiri wa kumtia hatiani Basil Pesambili Mramba; ilhali mkuu wa nchi ameshamsafisha hadharani kuwa ni mtu safi?
Je, kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa huko Rombo kumhusu Basil Pesambili Mramba, si kuingilia uhuru wa Mahakama? Je, Kikwete aliikumbuka kesi hiyo ya Mramba wakati alipokuwa akimnadi au aliisahau. Je, ni tatizo la kusahau au ni uzembe kama alivyouliza Msomaji Raia?
Binafsi, ningependa kuujua msimamo wa Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani kuhusu kauli hiyo ya Kikwete juu ya Mramba; maana ni jaji mkuu huyo huyo ambaye, Februari 6, 2009, kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria Duniani, alimsifu Rais Kikwete kwa kutoingilia uhuru wa mahakama, hata mara moja, iwe ni kwa matendo ama kwa kauli tangu aingie madarakani.
Ningependa pia kusikia kutoka kwa Kikwete mwenyewe kuhusu suala hili hasa ikizingatiwa kuwa Februari 14, 2006 Ikulu ilisambaza taarifa kwa vyombo vya habari nchini iliyomnukuu Rais akisema kwamba hataingilia kamwe uhuru wa mahakama. Alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza na uongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Sitashangaa Mahakama Kuu kuitupilia mbali kesi dhidi ya Mramba baada ya rais mwenyewe kumsafisha kuwa ni mtu safi.
Ndugu zangu, nimelijadili kwa kirefu suala hili la Rais Kikwete na Basil Pesambili Mramba, kwa sababu si mara ya kwanza kukerwa nalo.
Mara ya kwanza ilikuwa Agosti mwaka huu wakati Rais Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, aliposimamia kikao cha NEC cha kupitisha majina ya wagombea ubunge wa CCM na akawa na ujasiri wa kuruhusu majina ya Basil Pesambili Mramba na Andrew Chenge kugombea ubunge.
Nilimtarajia Kikwete angeweka ngumu majina angalau ya watu hawa wawili yasipitishwe kwa kuwa Chenge bado anaandamwa na kashfa ya rada na Mramba yeye amefikishwa kabisa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi baada ya serikali yake mwenyewe kusaka na kuridhishwa na ushahidi dhidi yake.
Ndugu zangu, Mwalimu Nyerere alikuwa na msemo wake: Caesars wife must be above suspicion; yaani ile suspicion tu ingetosha kwa Kikwete kuwaengua Chenge na Mramba. Na kusema kweli, kwa Mramba si suspicion tu; kwani serikali yenyewe ilishafanya uchunguzi na kuridhika na tuhuma dhidi yake, na ndiyo maana iliamua kumpeleka mahakamani.
Sasa, Mwenyekiti huyo wa CCM kuruhusu kupitishwa jina la Basil Pesambili Mramba kugombea ubunge katika kikao kile cha NEC, lilikuwa kosa kubwa kwake kufanya lakini kurudia tena kosa hilo hilo kwa kusimama tena hadharani na kuwataka wana-Rombo kumchagua tena Mramba kuwa mbunge wao kwa kuwa ni kiongozi safi, hakika kunaibua maswali kuhusu uwezo wa uongozi wa rais wetu huyu!
Najua wapo wasomaji watakaouliza: Angefanyaje? Mimi nadhani, baada ya kufanya kosa lile la kwanza, angekataa kufanya kosa la pili la kumkampenia Mramba; hasa kwa sababu kuna kesi ya ufisadi mahakamani dhidi yake.
Alipofika Rombo angekataa kabisa kumsimamisha Mramba na kumpigia kampeni. Angepanda jukwaani na kujipigia mwenyewe kampeni, na kisha kuendelea na safari yake.
Nyerere alifanya hivyo mwaka 1995 alipokataa jukwaani kumpigia kampeni mgombea wa CCM wa jimbo la Musoma Mjini, Dk. Emmanuel Magoti, kwa kuwa alikuwa na tuhuma za rushwa. Nyerere aliwaambia wapiga kura kwamba angekuwa yeye angempigia kura mgombea wa NCCR, Balozi Ndobo (na ndivyo wapiga kura wale walivyofanya).
Kwa mtazamo wangu, kama kweli Kikwete angekuwa ni mfuasi wa Nyerere, angefuata nyayo zake kwa kufanya hivyo hivyo huko Rombo kwa Mramba.
Niishie hapa, lakini huyo ndiye Kikwete wetu. Kama alivyohoji Msomaji Raia katika makala yake ya wiki iliyopita; nami sijui kama tatizo la rais wetu ni kusahau tu au ana tatizo jingine kubwa zaidi! Tafaka