Serikali ya Kenya imewasikiliza Wakenya. Sisi tunajadili Mwijaku na Masoud Kipanya

Serikali ya Kenya imewasikiliza Wakenya. Sisi tunajadili Mwijaku na Masoud Kipanya

Safari yetu ni ndefu Sana na ngumu kupindukia.

Watawala wetu wanajua nini tunachokitaka.

Wewe lini umeona mvumbuzi yeyote wa jambo lolote amewahi kukaribishwa Bungeni!??

Lakini Piere Liquid aliwahi kukaribishwa Bungeni na kushangiliwa Sana na wabunge.
Pierre,mandonga,poshy qeen
Misomisondo na wakata mauno wengine wote wamekaribushwa mjengoni

Ova
 
Muda huu William Ruto Rais wa Kenya amewaongoza wabunge wa Muungano wa Kenya Kwanza, kukubaliana na mambo mengi yaliyokuwa kwenye Bajeti ya nchi hiyo ambayo yalikuwa yanapingwa na Wakenya kuondolewa.

Baada ya mbinyo toka Kwa Wakenya Kwa zaidi ya wiki Moja hatimaye serikali imekubali yaishe.

Sisi tuko bize na jamaa anayesema baada Mtumie Muhammad (SAW) na Yesu Kristo anayefuatia ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Mara mambo ya Mwijaku na Masoud Kipanya.Nani aliyetuloga!!??
Kama siyo mtu mnafiki, basi utakubaliana na Mimi kwamba upeo wa kufikiri kwa Wakenya wengi zaidi upo juu zaidi ukilinganisha na Watanzania walio wengi zaidi.
Mfumo wetu mbaya wa Elimu na Mfumo wetu wa Siasa za mrengo wa Ujamaa/Ukomunisti ndio umewalemaza Wananchi wengi zaidi wa Tanzania katika kila nyanja ya maisha yao.
 
Umesahau pia,watu wanajadili mlinzi wa rais mwanaume kaingia msikitini,kila mtu anaisambaza hiyo picha kwa kadiri awezavyo!
 
Tanzania na Kenya zimekaribiana kijiografia, ila kuna tofauti kubwa sana ya uelewa na utayari wa raia wao.
Ni Sawa na darasa linaweza kuwa na wanafunzi A class na F class
 
Safari yetu ni ndefu Sana na ngumu kupindukia.

Watawala wetu wanajua nini tunachokitaka.

Wewe lini umeona mvumbuzi yeyote wa jambo lolote amewahi kukaribishwa Bungeni!??

Lakini Piere Liquid aliwahi kukaribishwa Bungeni na kushangiliwa Sana na wabunge.
Ndio mambo wanayopenda kuwahadaa watanzania, UDAKU, POMBE, NGONO, UMALAYA, USHOGA, UYANGA, USIMBA, MZIKI,..ongezea kwenye list.
 
Ndio mambo wanayopenda kuwahadaa watanzania, UDAKU, POMBE, NGONO, UMALAYA, USHOGA, UYANGA, USIMBA, MZIKI,..ongezea kwenye list.
Maujinga mengi mengi Sana... Na vyombo vyetu vya habari ni vioga balaa.

Kabla ya kurushwa live unaelekezwa mambo lukuki usiyotakiwa kusema dhidi ya Serikali.

Mzee njaa Pascal Mayalla analijua sana hili.
 
Tanzania na Kenya zimekaribiana kijiografia, ila kuna tofauti kubwa sana ya uelewa na utayari wa raia wao.
Ni Sawa na darasa linaweza kuwa na wanafunzi A class na F class
Sababu au Kiini Cha kuwepo kwa tatizo hili hapa Tanzania ni:-
1. Mfumo Mbaya wa Elimu, kuanzia Elimu ya Msingi hadi Elimu ya Juu.
2. Mfumo Mbaya wa Siasa za Ujamaa/Ukomunisti ambao tumeiga kutoka Urusi na China bila ya kuufanyia Upembuzi Yakinifu kwanza.
 
Tanzakiza ni channel ya vichekesho EAC.
Ndiyo maana wachekeshaji ndiyo watu maarufu na wanaosikilizwa Sana...

Utawaona wachekeshaji wakiwa sehemu ya misafara ya wakubwa...

Yaani eti wachekeshaji ndiyo tunaowatumia kwenye kukuza utalii wetu...😛😃😜
 
Hili la Kenya, hata mimi nawapongeza majirani zetu.

Lakini sikubaliani na maneno aliyotumia mleta mada katika kichwa cha mada yake. "Serikali ya Kenya haijawasikiliza waKenya". Ni sahihi kusema Serikali ya Kenya imelazimishwa/imesalimu amri, kwani hawakufanya hivyo kwa hisani.
Na uzuri wa haya yaliyotokea Kenya, ni kwamba hayakusimamiwa na vyama vya upinzani, bali wananchi wenyewe ndio wameamua kukataa.
 
ACHA UJINGA WA BONGO NINI SASA ? TZ HAKUNA SHID NDIYO MAANA UNAONA HAKUNA MAANDAMANO YA HOVYO HUKO YAPO KWAKUWA KUNA SHIDA ACHA AKILI ZA KUSHIKIWA
Unaposema "bongo" hakuna shida hiyo bongo unakusudia kusema Tanzania!!??

Kweli Tanzania hakuna shida!? Yaani watanzania wote humu JF tunaweza kukubaliana kwamba Bajeti yetu haina shida!??
 
Muda huu William Ruto Rais wa Kenya amewaongoza wabunge wa Muungano wa Kenya Kwanza, kukubaliana na mambo mengi yaliyokuwa kwenye Bajeti ya nchi hiyo ambayo yalikuwa yanapingwa na Wakenya kuondolewa.

Baada ya mbinyo toka Kwa Wakenya Kwa zaidi ya wiki Moja hatimaye serikali imekubali yaishe.

Sisi tuko bize na jamaa anayesema baada Mtumie Muhammad (SAW) na Yesu Kristo anayefuatia ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Mara mambo ya Mwijaku na Masoud Kipanya.Nani aliyetuloga!!??
Watu wa hovyo na tunazimikia vitu vya hovyo na ndomana tunapelekwa hovyo.
 
Subiri kwanza mambo ni mengi tukimalizana na Mwijaku na Kipanya kuna jambo la Yule aliyevaa hijabu, kuna Madada poa waliokamatwa, kuna mengi Sana kwenye vipaumbele vyetu
 
Yawezekana hili sakata la Mpina limepandikizwa na serikali ili kuwahadaa wananchi wajadili sakata wasijadili bajeti.
 
Muda huu William Ruto Rais wa Kenya amewaongoza wabunge wa Muungano wa Kenya Kwanza, kukubaliana na mambo mengi yaliyokuwa kwenye Bajeti ya nchi hiyo ambayo yalikuwa yanapingwa na Wakenya kuondolewa.

Baada ya mbinyo toka Kwa Wakenya Kwa zaidi ya wiki Moja hatimaye serikali imekubali yaishe.

Sisi tuko bize na jamaa anayesema baada Mtumie Muhammad (SAW) na Yesu Kristo anayefuatia ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Mara mambo ya Mwijaku na Masoud Kipanya.Nani aliyetuloga!!??
Kenyatta Jommo alitengeneza Watu 😂😂
 
Yawezekana hili sakata la Mpina limepandikizwa na serikali ili kuwahadaa wananchi wajadili sakata wasijadili bajeti.
Kabisa... Yaani maelezo ya mpina yamenyooka lakini ndiyo hivyo tena anapelekwa kwenye Kamati ili kukuza sarakasi zao za kisiasa.

Mpina anatengenezwa aonekane muasi/mpinzani ndani ya mfumo ili aonekane shujaa huku wakiendelea kula mema ya nchi.

Mfumo ni kama bahari. Kama Mpina angekuwa ni tatizo Kwa mfumo wangeshamuondoa fasta.

Mbona Ndugai kidogo tu wakapita naye!!!
 
Back
Top Bottom