Serikali ya Kenya yaamuru Wachina wanne waliomchapa Mkenya warudishwe kwao

Serikali ya Kenya yaamuru Wachina wanne waliomchapa Mkenya warudishwe kwao

Wachina wajinga sana! Yaani unaenda kwenye nchi ambayo ina sovereignty unaenda kuwachapa watu viboko?![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Walishashitakiwa na kuamriwa wafukuzwe nchini Kenya, isitoshe bila shaka wamefwata Sheria Kenya inavyosema kuhusu mgeni vinginevyo hao wageni wangepinga Mahakamani kufukuzwa, hata hivyo mimi siyo Mwanasheria.
Tujadili hoja iliyoletwa,wapi pameandikwa kuwa walishashitakiwa mahakamani?amri ya kuwaondoa imetolea na Home Affairs minister sio mahakama,na ukisoma vema mtoa hoja vile vile amesema kuwa vibali vyao vilikuwa batili(ndio maana nakuambia huku kwetu Lingusenguse ukinyakwa na vibali batili ndio utaijua sharia ya nchi hii,bora ukamatwe na kibali halali ila kimeisha muda sio feki)na ninaamini Kenya nao wana sharia kuhusu kwa mtuhumiwa kukumatwa na vibali feki
 
Mimi siyo Mwanasheria na sijui Sheria za Kenya zikoje hivyo siwezi kujadili sana kuhusu hilo hata mazingira yenyewe ya ishu ya Mchina kuchapa viboko Wakenya siyajui, lkn ninachojua ni kawaida nchi nyingi kuna baadhi ya makosa ukifanya kama wewe ni mgeni uhalali wako wa kuishi hiyo nchi unakoma moja kwa moja.
 
yes mkuu ila ni lazima mashitaka haya mahakama iamue.
 
Hii haitoshi na huo mgahawa ufungwe

Raia wanne wa Uchina waliokamatwa na Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) wanatarajiwa kurudishwa kwao baada ya amri iliyotolewa na Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i.

Agizo hilo lilisainiwa na Matiang'i Jumatano baada ya mahakama kuruhusu polisi kuwashikilia wachina wanne kwa siku 15 huku uchunguzi ukiendelea juu ya tukio la kumchapa viboko raia wa Kenya aliyekua akifanya kazi katika mgahawa ulioendeshwa na Wachina hao mjini Nairobi.

Raia hao wa Uchina waliotambuliwa kwa majina; Ou Qiang, Deng Hailan, Chang Yueping, na Yu-Ling; walitiwa nguvuni Jumapili baada ya video iliyoonyesha mmoja wa wahudumu wa mgahawa wa wachina akipigwa viboko na mmoja wao katika mgahawa wao kueneo kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo mwanaume wa Kichina alionekana akimpiga viboko Mkenya aliyekua akifanya kazi katika mgahawa unaouza vyakula vya kichina Chez Wou Restaurant katika eneo la Kileleshwa jijini Nairobi.

Iliripotiwa kuwa Mkenya, Simon Oseko, alikua akichapwa viboko kwa kosa la kuchelewa kufika kazini.

Alipigwa viboko viwili na meneja huku wafanyakazi wenzake wakishuhudia kwa mbali.

Oseko aliripoti tukio hilo katika kituo cha polisi. Iliripotiwa kuwa mpishi wa Kichina katika mgahawa huo pia aliwatisha wafanyakazi wengine raia wa Kenya ili wasizungumzie kuhusu mateso wanayopitia katika mgahawa.

Walikamatwa kwa kumiliki vibali vilivyopitwa na wakati vya kuishi nchini Kenya na kufanya kazi nchini humo bila kuwa na vibali vya kazi. Baadhi walikua na vibali vya kutembea Kenya.

Balozi wa Uchina nchini Kenya Wu Peng amesema anaafiki hatua iliyochukuliwa na serikali ya Kenya dhidi ya Wachina hao wanne: ''Serikali ya Uchina na ubalozi wangu unawashauri Wachina binafsi na kampuni zinazowekeza nchini Kenya kufanya kazi kwa faida ya nchi iliyowapokea, na bila shaka kila mara tunawaomba raia wetu hapa kuheshimu sheria za Kenya na kuishi kwa amani na Wakenya, yeyote atakayevunja sheria atapata athari zake, uhusiano wa nchi zetu unategemea sio tu serikali zetu bali watu wa nchi zetu'' alisisitiza balozi Peng mjini Nairobi.

Chanzo: BBC Swahili

Pia Soma: Raia wa China wakamatwa kwa kumcharaza viboko mfanyakazi aliyefika ofisini kwa kuchelewa

Jr[emoji769]
 
Wakenya sijui wamejiamini nini wakati wanadaiwa namna ile.

Ngoja wakasirike.
 
Wakenya sijui wamejiamini nini wakati wanadaiwa namna ile.

Ngoja wakasirike.

Hivi nyie kwa mlivyo maskini, mbona mnakua na deni kubwa hivi

2306968_FB_IMG_1581684371554.jpg
 
Back
Top Bottom