Kwanini wagombea binafsi wanaogopwa?
[Hapa mtaona jinsi serikali itavyogaragazwa kwenye mavumbi na kuangukia pua, mgombea binafsi October yupo!, ila nadhani ataishia kwenye ubunge na udiwani, kwenye urais itakuwa fujo!.
Lazima serikali iogope mgombea binafsi kwani ule msemo wake maaarufu wa kuweka mgombea asiyekubalika halafu wananchi mnaambiwa kuwa msichague mtu ila chama wataupeleka wapi? Piga ua garagaza Mgombea binafsi hatakubaliwa na serikali kwani CCm itapoteza wengi waliochoshwa na hali ilivyo sasa.
Kwani mahakama ya Rufani ya Tanzania inayo meno mbele ya Serikali? Majaji wote si ni wateule wa Rais? Utaweza vipi kumlaani mzazi wako na ikaw?
.
June ni mbali, April wanamaliza kila kitu na kufunga kazi. Issue ya kisheria sio uwepo wa mgombea binafsi, wanabishania legal techcalities on jurisdiction of the court over the constitution, kwamba mahakama kuu haina uwezo wa kutengua kipengele kwenye katiba kwa sababu hiyo mahakama ni subject ya hiyo katiba. Hoja za serikali ni bunge ndilo lenye mamlaka hiyo.
Hapa mtaona jinsi serikali itavyogaragazwa kwenye mafumbi na kuangukia pua, mgombea binafsi October yupo!, ila nadhani ataishia kwenye ubunge na udiwani, kwenye urais itakuwa fujo!.
Ndio hapo sasa! Kuchanganyikiwa kwa wakuu na waheshimiwa wetu kisa tu, wao ni wafanyakazi maarufu wa serikali.Jamani, ndio mnaanza kudharau mahakama? Hivi siku mkifika kule mnalialia na shida zenu halafu mahakama ikawatupilia mbali mtamlaumu nani?23rd February 2010
B-pepe
Chapa
Maoni
Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani
Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani, amewaonya watu wanaotoa msimamo kuhusu mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Alisema hakuna raia wa kawaida, mwenye dhamana ama mamlaka inayopaswa kutoa msimamo wa suala hilo, isipokuwa mahakama pekee.
Jaji Ramadhani alisema: Hata mimi binafsi ingawa ni Jaji Mkuu, siwezi na sina uwezo wa kulizungumzia suala hilo, sasa sijui hawa watu wanaofanya hivyo wanapata wapi mamlaka hayo.
Wakati Jaji Mkuu akitoa kauli hiyo, tayari mawaziri wawili wamekwisha kutoa misimamo kwa niaba ya serikali, kwamba hakutakuwa na mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mawaziri ambao wamezungumzia suala hilo na kutoa misimamo kwa niaba ya serikali ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera na Uratibu wa Bunge), Philip Marmo.
Jaji Mkuu alisisitiza: Hata mimi sina uwezo wa kuzungumzia suala ambalo bado lipo mahakamani kwa mujibu taaluma yangu, lakini hao wengine wanaofanya hivyo sijui.
Hata hivyo, Jaji Ramadhani hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo na badala yake alisema wananchi wasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ifikapo Aprili 8 mwaka huu.
Mbali na mawaziri hao, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (Nec), Rajabu Kiravu, alizungumzia suala hilo na kusema mabadiliko yatakayoruhusu mgombea binafsi, lazima yahusishwe mabadiliko ya sheria.
Pia Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, aliyefungua kesi iliyosababisha kutolewa uamuzi wa kuwepo mgombea binafsi, amekuwa akilizungumzia suala hilo mara kadhaa.
Wiki iliyopita Membe aliwaeleza mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, kuwa suala la mgombea binafsi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu halitawezekana.
Mabalozi hao waliomba kukutana na Waziri Membe ili awaeleleze hali ya kisiasa nchini na maandalizi ya uchaguzi huo.
Membe alisema serikali haipingi suala la mgombea binafsi, lakini kwa kuwa suala hilo linagusa katiba inabidi kwanza mabadiliko ya sheria yafanyike.
Alisema mabadiliko ya katiba ni mchakato unaochukua muda mrefu, hivyo ni dhahiri kwamba mgombea binafsi hawezi kushiriki katika uchaguzi wa mwaka huu.
Mahakama kuu mwaka 2006 iliruhusu kuwepo mgombea binafsi hakumu ambayo haijabadilishwa mpaka sasa.
Wakati huo huo, Jaji Ramadhani jana alifungua mafunzo ya masuala ya takwimu kwa watendaji wa mahakama kutoka mikoa mbalimbali.
Akizungumza na watumishi hao, alisema mahakama hapa nchini inakabiliwa na uhaba wa takwimu hatua inayosababisha kusikiliza tena kimakosa kwa kesi zilizowahi kutolewa uamuzi.
Alisema kutokana na kutokuwepo takwimu za kesi mba limbali kunawafanya majaji kupelekewa kesi zilizotolewa maamuzi bila kujua.
Mafunzo hayo ya watumishi wa mahakama yaliyofunguliwa jana na Jaji Ramadhani yanafanyika chuo cha takwimu kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE
23rd February 2010

Pasco mkuu vipi unamlinda muungwana? Kama kwenye urais itakuwa fujo kwanini huku kwenye ubunge na udiwani kusiwe fujo? Mimi nadhani kwenye Urais itakuwa rahisi zaidi kwani sio wengi wenye uwezo wa kuzunguka nchi nzima kujinadi; na kwasababu hiyo sitegemei fujo kwenye kinyang'anyiro cha UKULU!!
.
Nazungumzia practicability, unless sheria itamke wazi mgombea binafsi wa urais, atajigharimia,
Kwa sasa kila mgombea urais anapewa ulinzi 24/7, logistics na media access kwenye public media kwa fedha za umma, wakijitokeza watu 100 kwenye urais, we don't have the capacity to do all that for all of them.