Serikali ya Mama inafeli wapi?

Serikali ya Mama inafeli wapi?

Joined
Jul 20, 2024
Posts
42
Reaction score
98
Habari zenu wanachama wa Jamiiforums. Mimi pia ni mzima wa afya, na nimeandika uzi huu mahsusi kwa minajili ya kudurusu mfumo wa uongozi wa serikali yetu. Ingawa watu wanasema mama ana upiga mwingi, kuna sehemu katika uongozi wake panavuja. Tunaweza kuchunguza namna mama anavyoliongoza taifa kana kwamba Watanzania tulio wengi tumefunikwa na giza nene.

Sitaki kuwa na maneno mengi, lakini nataka niende moja kwa moja kwa mifano. Viongozi anaowaweka kama wasaidizi wake hawana weledi na nidhamu ya kazi zao, aghalabu skandali chafu za viongozi wakuu wa wizara n.k. Mfano rahisi ni yule aliyekuwa Naibu Waziri, Mhe. Pauline Gekur, na sakata lake lile chafu la kuamuru vijana waingizwe chupa katika sehemu za haja kubwa. Siafiki moja kwa moja kama ni kweli ama la, lakini kiongozi mkubwa wa wizara anawezaje kuwa na skandali chafu kama hizo?

Haitoshi basi tuseme ni bahati mbaya, mkuu wa mkoa wa Simiyu naye ana skandali chafu ya kumlawiti mwanafunzi wa chuo. Siwezi kusema moja kwa moja lakini ni kwanini serikali inaruhusu haya? Yaani, ukija kuchunguza kiundani ni kwamba ama mama hayuko makini au kuna mianya sehemu za juu.

Hivi kwanini tusijiulize matukio ya utekaji yamezidi? Mara Kagera albino kauawa, mara huku fulani kachinjwa, mara fulani amepotea, mara huku fulani amelawitiwa? Ni kwanini matukio yanazidi na ilhali tunaambiwa nchi ina amani? Mama, sipo kwa ajili ya kukosoa isipokuwa madhaifu yamezidi sana serikalini mwako. Tukikumbuka lile suala la Rais kumteua mkurugenzi ambaye alishafariki takribani wiki moja iliyopita, je, ni kweli kwamba Rais anaongozwa na wahuni wachache ambapo kazi yake yeye ni kuwaapisha tu?

Hakuna mkamilifu chini ya jua, lakini ni mengi mno. Mama anasikia ripoti ya CAG, anavunga kwanini? Ifike mahali tukuombe mama uvae kiatu cha mtangulizi wako. Uwe mkali na katili ili siku moja Watanzania wakupongeze kutoka moyoni kwani waliowengi wanakupromoti ili kujipatia ulaji. Mama, isipokuwa makini, Watanzania tutakushangaza mwaka 2025. Ninayo mengi ya kusema ila kwa leo naomba niishie hapa.

#TheDoctorOfPhilosophy - BGG Makaveli

Tanzania First 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Back
Top Bottom