Serikali ya Mapinduzi Zanzibar naomba mulione hilo

aleesha

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
798
Reaction score
1,178
Nikiwa Mtanzania mwenye mwingiliano mkubwa na watu wa visiwa vya Zanzibar, sina budi kusimama kidete kwa masilahi mapana ya Nchi hii bila kupepesa Macho.

Nitazungumza kuhusu suala la umiliki wa ardhi kwa wageni.

Kwa mujibu wa sheria, ardhi ni ya serikali lakini pia serikali ikaweka utararibu wa Wananchi wake kumiliki ardhi.

Shida yangu ipo kwenye umiliki wa ardhi visiwani humu kwa wageni, jamani. Kasi ya kununua maeneo kwa wageni ni kubwa mno, nafahamu kwamba lazima wageni wawekeze maana hatuwezi kukataa.

Ninachoona serikali ijaribu kuweka vigezo kwa wageni wanaonunua, je wananunua kwasababu zipi?

Nimwfwatilia vizuri sana, wageni wanaonunua ardhi kwa kuwekeza sio wengi kama wale wanaonunua kwa ajili ya kujenga makaazi yao ya kuishi tu.

Hivi sasa ukienda Paje, Jambiani na Michamvi utakuta wageni wanamikiki Nyumba za kuishi.

Lakini hali ni mbaya zaidi Jambiani na Paje, sikutarajia kwamba ipo siku wageni wataacha kununua maeneo ya Beach na kununua maeneo ya Viamboni wanakoishi wenyeji. Ni kawaida kuona Nyumba ya Mgeni Kiamboni huku jirani yake akiwa ni mzawa.

Lakini wageni wameenda mbali zaidi, yale maeneo ya mbali kabisa na makaazi ya watu wenyewe wanaita Maweni, ndiko sasa kumekuwa kama Ulaya au Marekani wamenunua sana, hayo ni maeneo ambayo wananchi wameyadharau hawajengi japo ni maeneo yao. Hata kulimwa hayalumwi.

Lakini kinachoniliza zaidi ni ule ukubwa wa ardhi ambayo mgeni ananunua, yaani mgeni anaweza kununua kutoka kwa mtu mmoja Ekari 5 kisha akatafuta majirani wa eneo alilonunua, akaunga unga hadi kupata ukubwa Hata wa kiwanja cha Mpira.

Akimaliza anapiga Bonge la Ukuta! Hawaishii hapo wanaenda tena sehemu nyingine pia. Kwa hiyo ukitembea maeneo ya countryside utakuta kwamba maeneo makubwa yanamilikiwa na wageni.

Nimefwatilia matumizi ya ardhi kwa uchache, ni kwamba wengi wao wanatarajia kujenga Nyumba za kukodisha wenzao wanaokuja kutembea, lakini pia za makaazi yao wenyewe.
Kinachoumiza zaidi hata bei ya kuuza ni ndogo mno! Mwananchi anaona akipewa milioni Kumi ni nyingi sana! Yapo maeneo yanauzwa milioni 40 mpaka milioni 7 .

Wiki iliyopita Kuna kijana akanipigia simu ananiambia huna Milioni 2 hapo ununue Eneo? Kuna jamaa anauza sehemu yake na Kuna mgeni anataka apanunue, alafu ni eneo zuri. Akasema kuliko anunue mgeni afadhali anunue mwenyeji.

Nikasema Lahaula! Imefikia hatua hii?

HATIMA YA KIZAZI KIJACHO.

Kutokana na kasi hiyo nina wasiwasi kwamba baadae vizazi vyetu vitakuwa vigeni.

Hicho kizazi hakitapata nafasi ya kumiliki ardhi maana itakuwa imejaa na haipo.

Zanzibar ni ndogo ni nchi ya visiwa hakuna uwezekano wa kutanua ardhi. Ni muhimu kuliangalia hilo. Ninachoona huenda sheria ya kuuza ardhi iongezewe nguvu haswa pale ardhi inapotoka kwa mzawa kwenda kwa mgeni.

Hata kama ardhi ni ya mwananchi, lakini wasiruhusiwe kuuza tu kiholela.

Unajua hata maeneo ya Beach Ambayo 95% yametwaliwa na wageni, wananchi waliuza kwa bei chee 😢

Sijuwi kama huko Ulaya na kwingineko eneo la Beach linaweza kuuzwa million 300? Au milioni 600?

Sasa hivi Mgeni aliyewekeza Beach akipachoka ama akifilisika anamtafuta mgeni mwenziwe anamuuzia na hamuuzii mswahili. Ni kwanini? Unatakiwa uumize Kichwa ni kwanini.

Mimi nitakwambia, ni kwasababu bei atakayomuuzia Mswahili hasogei, labda hawa mamilionea wetu wachache Tanzania.

Kwa sababu wanatambua umuhimu wa maeneo hayo ndio maana hageuki nyuma kumwangalia mwenyeji.

Sasa wageni wameachana na Beach wamevamia maeneo ambayo Mzawa anaona hayana maana kwake, wageni sasa wamefanya juhudi za kufikisha umeme maana maeneo hayo mengi hayana.

Wito wangu kwa serikali turudi Mezani tuangalie Sera zetu za ardhi, tutaaibika katika siku za usoni.

Sisi ni waafrika tunazaliana kwa wingi, kizazi cha baadae kitaenda wapi?

Ahsante
 
Hao wageni ni kutoka nchi gani? Hebu nyoosha maelezo kwanza. Kabla sijachangia chochote.
 
mleta mada pole sana, hua unaumia sana lakini ndio mambo yalivyo, CCM Zanzibar kwa miaka karibu 60 ya utawala wao wame completely fail kwenye uongozi. hakuna hata kimoja wanachoweza kusimamia zaidi ya kuiba kura.
 
Nikiwa Mtanzania mwenye mwingiliano mkubwa na watu wa visiwa vya Zanzibar, sina budi kusimama kidete kwa masilahi mapana ya Nchi hii bila kupepesa Macho.

Nitazungumza kuhusu suala la umiliki wa ardhi kwa wageni.

Kwa mujibu wa sheria, ardhi ni ya serikali lakini pia serikali ikaweka utararibu wa Wananchi wake kumiliki ardhi.

Shida yangu ipo kwenye umiliki wa ardhi visiwani humu kwa wageni, jamani. Kasi ya kununua maeneo kwa wageni ni kubwa mno, nafahamu kwamba lazima wageni wawekeze maana hatuwezi kukataa.

Ninachoona serikali ijaribu kuweka vigezo kwa wageni wanaonunua, je wananunua kwasababu zipi?

Nimwfwatilia vizuri sana, wageni wanaonunua ardhi kwa kuwekeza sio wengi kama wale wanaonunua kwa ajili ya kujenga makaazi yao ya kuishi tu.

Hivi sasa ukienda Paje, Jambiani na Michamvi utakuta wageni wanamikiki Nyumba za kuishi.

Lakini hali ni mbaya zaidi Jambiani na Paje, sikutarajia kwamba ipo siku wageni wataacha kununua maeneo ya Beach na kununua maeneo ya Viamboni wanakoishi wenyeji. Ni kawaida kuona Nyumba ya Mgeni Kiamboni huku jirani yake akiwa ni mzawa.

Lakini wageni wameenda mbali zaidi, yale maeneo ya mbali kabisa na makaazi ya watu wenyewe wanaita Maweni, ndiko sasa kumekuwa kama Ulaya au Marekani wamenunua sana, hayo ni maeneo ambayo wananchi wameyadharau hawajengi japo ni maeneo yao. Hata kulimwa hayalumwi.

Lakini kinachoniliza zaidi ni ule ukubwa wa ardhi ambayo mgeni ananunua, yaani mgeni anaweza kununua kutoka kwa mtu mmoja Ekari 5 kisha akatafuta majirani wa eneo alilonunua, akaunga unga hadi kupata ukubwa Hata wa kiwanja cha Mpira.

Akimaliza anapiga Bonge la Ukuta! Hawaishii hapo wanaenda tena sehemu nyingine pia. Kwa hiyo ukitembea maeneo ya countryside utakuta kwamba maeneo makubwa yanamilikiwa na wageni.

Nimefwatilia matumizi ya ardhi kwa uchache, ni kwamba wengi wao wanatarajia kujenga Nyumba za kukodisha wenzao wanaokuja kutembea, lakini pia za makaazi yao wenyewe.
Kinachoumiza zaidi hata bei ya kuuza ni ndogo mno! Mwananchi anaona akipewa milioni Kumi ni nyingi sana! Yapo maeneo yanauzwa milioni 40 mpaka milioni 7 .

Wiki iliyopita Kuna kijana akanipigia simu ananiambia huna Milioni 2 hapo ununue Eneo? Kuna jamaa anauza sehemu yake na Kuna mgeni anataka apanunue, alafu ni eneo zuri. Akasema kuliko anunue mgeni afadhali anunue mwenyeji.

Nikasema Lahaula! Imefikia hatua hii?

HATIMA YA KIZAZI KIJACHO.

Kutokana na kasi hiyo nina wasiwasi kwamba baadae vizazi vyetu vitakuwa vigeni.

Hicho kizazi hakitapata nafasi ya kumiliki ardhi maana itakuwa imejaa na haipo.

Zanzibar ni ndogo ni nchi ya visiwa hakuna uwezekano wa kutanua ardhi. Ni muhimu kuliangalia hilo. Ninachoona huenda sheria ya kuuza ardhi iongezewe nguvu haswa pale ardhi inapotoka kwa mzawa kwenda kwa mgeni.

Hata kama ardhi ni ya mwananchi, lakini wasiruhusiwe kuuza tu kiholela.

Unajua hata maeneo ya Beach Ambayo 95% yametwaliwa na wageni, wananchi waliuza kwa bei chee [emoji22]

Sijuwi kama huko Ulaya na kwingineko eneo la Beach linaweza kuuzwa million 300? Au milioni 600?

Sasa hivi Mgeni aliyewekeza Beach akipachoka ama akifilisika anamtafuta mgeni mwenziwe anamuuzia na hamuuzii mswahili. Ni kwanini? Unatakiwa uumize Kichwa ni kwanini.

Mimi nitakwambia, ni kwasababu bei atakayomuuzia Mswahili hasogei, labda hawa mamilionea wetu wachache Tanzania.

Kwa sababu wanatambua umuhimu wa maeneo hayo ndio maana hageuki nyuma kumwangalia mwenyeji.

Sasa wageni wameachana na Beach wamevamia maeneo ambayo Mzawa anaona hayana maana kwake, wageni sasa wamefanya juhudi za kufikisha umeme maana maeneo hayo mengi hayana.

Wito wangu kwa serikali turudi Mezani tuangalie Sera zetu za ardhi, tutaaibika katika siku za usoni.

Sisi ni waafrika tunazaliana kwa wingi, kizazi cha baadae kitaenda wapi?

Ahsante
Inabidi mjikusanye halafu mkamuone waziri au katibu mkuu husika. Ukweli ni kwamba Zanzibar kuiepusha na uvamizi wa wageni ni ngumu sana.

Njoeni Tanganyika nanyi mnunue ardhi maana huko mbele kuna hatari watu watakosa hata sehemu ya kucheza bao.
 
Back
Top Bottom