carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump, umebatilisha zaidi ya visa 300,000 tangu aanze muhula wake wa pili, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema Jumanne, huku serikali ikiendeleza hatua kali dhidi ya wahamiaji.
Trump amesema hatua hizo, pamoja na kampeni ya kuwafukuza wahamiaji wasio na uhalali wa kuishi nchini humo, zinalenga kuimarisha usalama wa taifa. Hata hivyo, watetezi wa haki za binadamu wanapinga operesheni hiyo, wakisema imeibua wasiwasi kuhusu uzingatiaji wa taratibu za kisheria, uhuru wa kujieleza na usalama wa makundi ya wachache, ambao baadhi yao wanahofia kulengwa kwa misingi ya rangi au asili yao.
Akitoa takwimu hizo kupitia mtandao wa kijamii wa X, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Tommy Pigott, alisema utawala wa Trump umebatilisha visa vingi zaidi kwa kasi kubwa kuliko utawala mwingine wowote katika historia ya nchi hiyo.
Pigott alisisitiza kuwa serikali haitawavumilia wageni walio nchini Marekani kwa kutumia visa ambao wanakiuka sheria, wanajihusisha na ulaghai au wanatishia usalama wa taifa.
Chanzo: Reuters