KERO Serikali ya Mtaa Yombo Vituka, mnatuchanganya, wekeni ufafanuzi wa kiasi cha kulipa “hela ya Taka”

KERO Serikali ya Mtaa Yombo Vituka, mnatuchanganya, wekeni ufafanuzi wa kiasi cha kulipa “hela ya Taka”

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

NBica

Member
Joined
Sep 13, 2010
Posts
39
Reaction score
36
Mimi ni Mkazi wa Kata ya Yombo Vituka, hapa mtaani kwetu moja ya kero kubwa ni kukosekana kwa utaratibu mzuri wa utaratibu wa kulipia malipo ya taka.

Viongozi wetu wa Serikali ya Mtaa wanaweza kuona ni kitu kidogo lakini kina kera, kwanza tunapolipa tunatakiwa kulipa kwa kila chumba au kwa nyumba?

Ikifika mwisho wa mwezi jamaa wanaokusanya hela ya taka wanazunguka na kututaka tulipe Sh 3,000 au zaidi ya hapo kwa kila chumba hata kama hukuwepo unatakiwa kulipa tu, unakuta nyumba ikiwa na vyumba sita au nane wanatoza kwa kila chumba.

Nashauri mamlaka zinazohusika nitoe muongozo jinsi ya kulipa, kwani utaratibu uliopo unatuumiza hasa sisi mabachela ambao hatuna familia na hatukai nyumbani lakini ukirudi tu unakutana na madeni ya taka.
 
Back
Top Bottom