KERO Serikali ya Mwanza iboreshe ‘maeneo korofi’ ambapo mvua ikinyesha hali inakuwa mbaya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607



Maeneo ya Daraja la Masai
Daraja la Masai
Moja ya changamoto kubwa wanayoipata wakazi wa eneo hilo ni wakati wa mvua kubwa au mafuriko, inapokuwa hivyo Daraja la Salamani na Daraja la Uhuru ambayo yana kina kifupi athari inazidi kuwa kubwa.

Kinachoombwa na watu wengi ni kusafishwa kwa Mto Mirongo ambao kwa muda mrefu haujatolewa mchanga, hali hiyo inasababisha changamoto maji kufurika ndani ya muda mfupi.

Eneo la Mabatini
Kuna ukimya kutoka kwa mamlaka, ni moja ya maeneo korofi na changamoto yake haijatatuliwa, vitu vingi huwa vinasombwa wakati wa mvua na maji kuzingira makaazi.

Inapokuwa hivyo ni hatari kwa Maisha ya watu na Wanyama wanaofugwa, pia Vyombo vya usafiri ni shida.





Eneo la Mkuyuni
Hapa kila mvua ikinyesha basi ujue shughuli itakuwa kubwa, maji yanaacha njia na kuingia sokoni na kwenye makazi ya watu, kuna Daraja hapo linajaa maji haraka na kutostahimili maji yanayotoka kwenye Mto Mrongo.







 
Duhhh hii nchi imeoza kila mahali na viongozi wanatazama hadi majanga yatokee ndipo waanze kumtafuta mchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…