Kitimoto
JF-Expert Member
- Aug 25, 2012
- 6,941
- 7,808
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumwamrisha Polisi akufanyie kitu ni rahisi sana! Kuna hadithi jamaa alitaka polisi wamlimie shamba. Akawatumia ujumbe kuna maiti wamezikwa kwneye shamba lake. Wacha polisi watimke kwenda kufukua na majembe kutafuta wapi wamezikwa - wakalima shamba lote jmaa kaja kupanda mbegu tu!😅😅😅 POLISI leo wameandamana
donkey donkey, habishi anapowekewa mzigo wowoteBaadhi ya Mapolisi nimekutana nayo yamechooka sijui kama wamekula.
Polisi wakiwa mitaani wakifanya maandano kufikisha ujumbe kwa jumuia kwa niaba ya Chadema
Chadema wametumia akili sana, na Serikali ya Raisi Samia ikaingia katika mtego wao bila kujitambua na kwa kukurupuka. Chadema walichotaka si wao wenyewe kuandamana, bali maandamano yamefanywa kwa niaba yao na Polisi wenyewe waliotumwa mitaani na serikali ya Raisi Samia. Kwa hiyo vyombo vya habari, badala ya kuonyesha wafuasi wa Chadema wakiandamana kudai haki za binadamu, lengo hili linatimizwa kwa wadau kupitia polisi walio mitaani kuzuia maandamano ya Chadema ya kudai serikali ikomeshe ukiukwaji wa haki za binadamu!
Kuna baadhi ya viongozi wakuu hata wametoa kauli za kuwaua wafuasi wa Chadema na kumvunja mguu wa pili Lissu. Yote haya yamesikiwa na umma wa watu, ndani na nje ya nchi.
Sasa hata mtoto mdogo anajua kwa nini leo Chadema walitaka kuandamana - anapouliza Polisi wanafanya nini mitaani! Maandamano yaliyofanywa na Polisi kwa niamba ya Chadema yamekuwa makubwa kwa kuingia mitaa mingi kuliko ambavyo Chadema wenyewe waneweza kufanya!
In fact, Chadema hapa wameua ndege wawili kwa jiwe moja; ujumbe wao kwa wananchi na hata nje ya nchi umefika, na pili wameonyesha kwa ushahidi ulio wazi ni jinsi gani serikali ya Raisi Samia inatumia vyombo vya dola na nguvu kubwa kukandamiza demokrasia nchini.
Kwa hiyo kwa hapa mpaka hii game inavyomalizika, magoli ni Chadema 2 Serikali 0
Anaemshauri Raisi Samia ni zero kabisa! Lakini Raisi Samia nae anatakiwa afuate ushauri wa Kikwete - za kuambiwa changanya na za kwako upate jibu sahihi!
Pia, soma: LIVE - Yanayojiri kwenye Maandamano ya CHADEMA 23/9/2024