#COVID19 Serikali ya Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje ya muda wa siku 10 katika mji mkuu wa Kigali na wilaya nane

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje ya muda wa siku 10 katika mji mkuu wa Kigali na wilaya nane baada ya ripoti za vifo na wagonjwa wa corona kuongezeka.

Watu wametakiwa kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia Jumamosi tarehe 17 mpaka tarehe 26 Julai, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Biashara, shughuli za umma na usafiri, shule, michezo na burudani vyote vimefungwa na mazishi yanatakiwa kuhudhuriwa na watu 15 tu.

Watu wanaweza kutoka nje ya nyumba zao kwa ajili ya huduma muhimu pekee au wafanyakazi muhimu.
Wiki nne zilizopita, taifa hilo limerekodi watu elfu moja waliopata maambukizi ya corona kwa siku na siku saba zilizopita hali ilikuwa mbaya zaidi.

Maofisa wa afya wamesema kusambaa kwa wimbi la tatu la kirusi kipya cha Delta ndio kinafanya taifa hilo kuwa na hali mbaya zaidi.

Rwanda imerekodi visa zaidi ya 50,000 vya covid , na zaidi ya waathirika 600 na zaidi ya watu mia nne wamepata chanjo.
 
Shida ni pale watu wanafikiri wako salama baada ya kuchanjwa.
Hakuna chanjo ya kuzuia corona ila ni biashara tu.Rwanda walichanjwa matokeo ndo haya.
Vifo vinaweza ongezeka siku kumi mtu Hana msosi ni marehemu tayari.
Wacha kupotosha! Waliochanjwa wangapi na wasiochanjwa wangapi? Hawajachanja taifa zima, hivyo lazima tatizo liendelee! Hivi wanavyofanya ni sahihi kabisa. Wao wanapima, wanatoa chanjo, na watoa takwimu sahihi, sisi je?
 
Bado uaweza kukosoa chanjo, maana kwakuwa tupo hatua za awali kimatumizi, mapungufu hayakosekani. Lakini si kwa staili hii. Hii ya kwako ni porojo kupitiliza. UNAPOTOSHA SANA!
 
Ni nchi gani watu wake waneacha kufa sababu wamechanjwa?
Virus anayebadilika unaweza kumsldhibiti kwa chanjo moja?
Endelea kujidanganya.
 
Wacha kupotosha! Waliochanjwa wangapi na wasiochanjwa wangapi? Hawajachanja taifa zima, hivyo lazima tatizo liendelee! Hivi wanavyofanya ni sahihi kabisa. Wao wanapima, wanatoa chanjo, na watoa takwimu sahihi, sisi je?
Takwimu na hizo chanjo zimesaidia Nini kuzuia vifo Ulaya na Marekani?
Barakoa za Nini Kama wamechanjwa?
Jidanganyeni.
 
Shida ni pale watu wanafikiri wako salama baada ya kuchanjwa. Hakuna chanjo ya kuzuia corona ila ni biashara tu.Rwanda walichanjwa matokeo ndo haya.

Vifo vinaweza ongezeka siku kumi mtu Hana msosi ni marehemu tayari.
Waliochanjwa ni 3% tu.

Kwani kipindi kile wamekaa lockdown zaidi ya mwezi walikufa wananchi wangapi?
 
Ni nchi gani watu wake waneacha kufa sababu wamechanjwa?
Virus anayebadilika unaweza kumsldhibiti kwa chanjo moja?
Endelea kujidanganya.
Mimi sijidanganyi, sema kama kawaida ya mbongo kukosolewa ni mwiko. Nimekwambia wazi kuwa kukosoa inawezekana lakini si kwa namna ufanyavyo. Si wewe wala mimi wenye ushahidi kwa kiasi gani chanjo zimefanikiwa au la. Kwahiyo, kuja tu na hoja ya jumla tu kuwa X ni sawa na Y ni makosa. Unahitaji vigezo kadhaa kujenga hoja yako ili kuonekana unatambua hali ya mambo.
 
Wakat mkuu wa kaya anaamua watu wake wasitoke nje ya nyumba zao ili kudhibit maambukiz mapya yey na kundi lake wametoka nje ya nchi kabisaaaaaa.
 
Serikali ya Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje ya muda wa siku 10 katika mji mkuu wa Kigali na wilaya nane baada ya ripoti za vifo na wagonjwa wa corona kuongezeka.

Watu wametakiwa kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia Jumamosi tarehe 17 mpaka tarehe 26 Julai, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Biashara, shughuli za umma na usafiri, shule, michezo na burudani vyote vimefungwa na mazishi yanatakiwa kuhudhuriwa na watu 15 tu.

Watu wanaweza kutoka nje ya nyumba zao kwa ajili ya huduma muhimu pekee au wafanyakazi muhimu.
Wiki nne zilizopita, taifa hilo limerekodi watu elfu moja waliopata maambukizi ya corona kwa siku na siku saba zilizopita hali ilikuwa mbaya zaidi.

Maofisa wa afya wamesema kusambaa kwa wimbi la tatu la kirusi kipya cha Delta ndio kinafanya taifa hilo kuwa na hali mbaya zaidi.

Rwanda imerekodi visa zaidi ya 50,000 vya covid , na zaidi ya waathirika 600 na zaidi ya watu mia nne wamepata chanjo.
mama ndio kwanza yupo burundi nyumabni kwa kina mpango VP
 
Sisi watanzania tunaisubiri CHANJO dhidi ya CORONA kwa hamu kubwa!

Ije tu tuchanjwe ,mengine mbele kwa mbele....
 
Mimi sijidanganyi, sema kama kawaida ya mbongo kukosolewa ni kama kumtia kidole takoni. Nimekwambia wazi kuwa kukosoa inawezekana lakini si kwa namna ufanyavyo. Si wewe wala mimi wenye ushahidi kwa kiasi gani chanjo zimefanikiwa au la. Kwahiyo, kuja tu na hoja ya jumla tu kuwa X ni sawa na Y ni makosa. Unahitaji vigezo kadhaa kujenga hoja yako ili kuonekana unatambua hali ya mambo.
Lugha uliyotumia mkuu ina makali sana
 
Shida ni pale watu wanafikiri wako salama baada ya kuchanjwa. Hakuna chanjo ya kuzuia corona ila ni biashara tu.Rwanda walichanjwa matokeo ndo haya.

Vifo vinaweza ongezeka siku kumi mtu Hana msosi ni marehemu tayari.
Rwanda imechanja watu wangapi? Acha upotoshaji. Rwanda ina watu milioni nane, sasa tuambie waliopata chanjo ni wangapi?
 
Back
Top Bottom