PreGE2025 Serikali ya Samia yazidi kuanikwa dunia nzima-Maria Sarungi atoa presentation kali kuieleza dunia yanayojiri Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Aisee mambo yanazidi kubamba, Kitanzi kinazidi kukaza, na hali imekuwa si hali tena, kiufupi hamkani si shwari tena.

Huku wajinga wakiamini kuwa kwa kuteka na kupoteza watu sauti ya kudai haki na mabadiliko ya msingi itanyamazishwa, lakini ukweli na haki siku zote huwa havipendwi kupuuzwapuuzwa.

Shangazi Maria leo amewasimamisha wafadhili na wapenda haki duniani kwa kutoa presentation moja kali sana.

Aisee usiogope mwenye msuli mnene bali ogopa mwenye akili kubwa.

Shangazi kapiga, katandika kwelikweli. Kapukutisha sifa na credentials zote za wapenda vyeo. Sijui Bi mkubwa akienda huko nje atajisikiaje maana wenyeji watakuwa wanamg'ong'a pindi akizingumzia 4R au democracy. Maana alichokifanya Maria huko ni counter attack moja kali sana kwenye credentials za mtu fulani.

Hebu msikilize wewe mwenyewe hapa uone shangazi alivyokinukisha kwa medani za kifield marshall.

Tumeshawaambia hawa wakubwa hapa nchini, kuwa bila kuleta mabadiliko ya msingi hapa nchini ni kujitoa ufahamu kama Ceasescu wa Romania, alisubiri wanaompinga wawe wengi zaidi, kilichotokea baada ya hapo the rest is history.

Tunataka mabadiliko nchini, la sivyo hii nchi itastuck, mbele haitokwenda, nyuma haitorudi


View: https://youtu.be/8lNHdfF15tk?si=eP21aiSnKrIYNrYu
 

Umeona shangazi alivyotandika mtu huko mkutanoni?

Yaani kachapa, kachapa kwelikweli
 
Nimemsikiliza na kumwangalia kwa makini, kumbe taifa lina watu wazuri kiasi hiki wakati kina jerry mulo, msukuma na wale vilaza kule bungeni wanatamba...

Ukiwasikiliza wanasiasa wetu wengi walivyo mbumbumbu unaweza dhani ndivyo watanzania wote tulivyo kiakili kumbe watu makini wapo nje ya mfumo wa utawala wetu.

Hongera sana Maria
 

Baba yake alikuwa profesa cream of the cream ya nchi hii. Inawezekana huyo binti karithi brains za baba yake ndiyo maana unaona presentation yake si ya viwango vya kawaida.
 
Yajayo yanatafakarisha
 
Siku wakienda waangalie isije ikawa kama ya Ramaphosa unasutwa kama mwajuma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…