Serikali ya Sweden Imepiga Marufuku Matumizi ya ChatGPT na Claude Kwa Watumishi wa Umma na Badala yake watatumia Microsoft Copilot kama Mbadala

Serikali ya Sweden Imepiga Marufuku Matumizi ya ChatGPT na Claude Kwa Watumishi wa Umma na Badala yake watatumia Microsoft Copilot kama Mbadala

Ntemi_Ntale

Member
Joined
Aug 23, 2026
Posts
20
Reaction score
16
Kwa Ufupi ni Kwamba:
  • Serikali ya Sweden imepiga Marufuku matumizi ya ChartGPT na Claude kwa watumishi wa Umma(Public servant) kuanzia tarehe 26 Oktoba.​
  • Serikali inataja wasiwasi kuhusu usalama wa taarifa (information security), ambapo serikali imesema watumishi watatumia Microsoft Copilot Kama Mbadala(Altenative)​
  • Mamlaka ya Kodi ya Sweden (Swedish Tax Agency) na Bodi ya Taifa ya Huduma za Kitaasisi (National Board of Institutional Care) tayari zimewekewa marufuku hio , na Mamlaka ya Utekelezaji (Enforcement Authority) inatarajiwa kutangaza uamuzi wake hivi karibuni.

    ----------------------

    Wafanyakazi wa serikali ya Sweden hawawezi tena kutumia matoleo ya kivinjari (browser-based versions) ya ChatGPT ya OpenAI wala Claude (Anthropic) kwenye kompyuta zao za kazini, kufuatia wasiwasi wa kiusalama unaohusiana na uchakataji wa data nyeti.

    Uamuzi huu umekuja baada ya tathmini ya zana za AI zilizokuwa zikitumiwa na wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri ya Sweden (Swedish Transport Administration) mapema mwaka huu, ambayo ilibaini matumizi “yenye matatizo(problematic)” ya majukwaa hayo ya AI katika kutekeleza kazi za serikali.


    Maafisa walikuwa na wasiwasi kwamba kuingiza taarifa nyeti kwenye mifumo hii bila kuwa na makubaliano yanayoeleza namna ya kulinda na kuhifadhi data kwa usalama, kungeweza kusababisha taarifa hizo kuingizwa kwenye mfumo (model) na kuhifadhiwa kwa ajili ya mafunzo (training).


    Matumizi ya majukwaa yasiyodhibitiwa (Unregulated Platforms) wala kulindwa na makubaliano kama hayo, yanayojulikana pia kama shadow IT, yanaweza kuleta “madhara kwa usalama wa taarifa zetu(consequences for our information security),” alisema Mikael Wettercrantz, Mkurugenzi wa Masuala ya Kidijitali katika Ofisi za Serikali ya Sweden (Government Offices of Sweden).


    Microsoft Copilot ambayo imepita mchakato wa ukaguzi wa kiusalama(security screening process) na inalindwa na makubaliano ya kiusalama kati ya kampuni hiyo ya Marekani na serikali ya Sweden, inapendekezwa kama mbadala(Recommended as an alternative)


    Ingawa wafanyakazi wa serikali bado wataweza kutumia AI kuwasaidia katika kazi zao, watafanya hivyo chini ya udhibiti mkali zaidi wa kiusalama(Tighter security controls). Ni idadi ndogo tu ya wafanyakazi watakaoruhusiwa kuendelea kutumia ChatGPT na Claude, na hilo litawezekana tu kupitia jukwaa maalum la wasaidizi wa AI (AI assistants) lililotengenezwa na mamlaka za Sweden.


    Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la umma la Sweden, Sveriges Radio, vikwazo vya matumizi ya ChatGPT na Claude pia vimewekwa katika Mamlaka ya Kodi ya Sweden (Swedish Tax Agency) na Bodi ya Taifa ya Huduma za Kitaasisi (National Board of Institutional Care). Mamlaka ya Utekelezaji ya Sweden (Swedish Enforcement Authority) kwa sasa inalifanyia tathmini suala hili.


    Majukwaa haya ya AI (ChartGPT Na Claude) sasa yanaungana na DeepSeek kwenye orodha ya zana za AI( AI tools) ambazo hazijaidhinishwa na serikali ya Sweden kutokana na hofu ya usalama wa data.

    --------------
    Source:euronews​




    openai-jpg.3699714
 
Back
Top Bottom