Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuimarisha Mashirika yake matatu, TRC, Air Tanzania, na Posta. Wananchi tunasubiri TTCL na BRT

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Hatimaye Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuimarisha Mashirika yake matatu, TRC, Air Tanzania, POSTA, Wananchi tunasubiri TTCL na BRT.

Hongera sana Serikali ya Tanzania kwa kufanikiwa kurejesha heshima ya nchi iliyokuwa imepotea kwa muda mrefu mmejitahidi sana.

Miakaka ya nyuma hatukuwa na ndege wala tren za kisasa vilevile POSTA iliyumba sana tulibakiwa na masanduku tu ya kupokea barua ambazo kwa ulimwengu wa sasa zimepitwa na wakati lakini sasa tunatuma na kupokea mizigo kutoka mataifa mbalimbali.

Tunaomba mrejeshe shirika la TTCL ili Watanzani tujivunie kuwa na chetu na kuimarisha BRT kwasababu wananchi wanapata usumbufu mkubwa sana kwenye Mwendokasi.

1000004564.jpg
1000004565.jpg
1000004566.jpg
1000004567.jpg
1000004568.jpg
 
Air Tanzania sio rafiki kwa watanzania tulio wengi. Tangu wameiondoa Fast Jet sijawahi tena kupanda ndege kwa safari za hapa bongo. Nauli si rafiki hata kidogo kwa sisi akina pangu pakavu.
Itabidi waulizwe
 
Pamoja na juhudi hizo, Kuna haja tukabadirisha namna ya Uendeshaji wake ili tujikite kibiashara zaidi.

Haya mashirika, ni Serikali yenyewe ndiyo itayaua.

Mathalani Viongozi wa mashirika hayo kuteuliwa na Mhe. Rais

Unakuta anapelekwa pale CEO ambaye ukiachana na Ukada wake wa Chama, Hana historia kwenye kufanya biashara hata Kwa Mwaka mmoja na akapata Faida.

Pia tuache Siasa kwenye biashara hizi Kwa hayo mashirika.

Mathalani Mwaka Jana, safari yetu ya ndege ilicheleweshwa Kwa saa 1 na dakika 25 zaidi kutokana na eti kumsubiria Kiongozi fulani wa Kiserikali apande.

Yaani ndege inatakiwa kuondoka saa 6:00 Mchana, lakini inaondoka saa 7:30 kisa tu kumsubiria Mkubwa wa Serikali afike na tuondoke naye.

Vitu vya kipuuzi kama hivi, vikiachwa viendelee wateja wataona bora apande basi ijulikane hivyo kuliko kusubirishana kijinga namna hiyo.

Kila abiria akizira kusafiri na ndege si mashirika yatakosa abiria hivyo kuathiri Uwekezaji huu Mkubwa uliofanywa Kwa Kodi zetu Wananchi🙌
 
Kumbe kuna kusubiri tena wakubwa wapande? Kwahiyo wao hawafuati ratiba ni ratiba ndio inawafwata wao!
 
Hatimaye Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuimarisha Mashirika yake matatu, TRC, Air Tanzania, POSTA, Wananchi tunasubiri TTCL na BRT.

Hongera sana Serikali ya Tanzania kwa kufanikiwa kurejesha heshima ya nchi iliyokuwa imepotea kwa muda mrefu mmejitahidi sana

Miakaka ya nyuma hatukuwa na ndege wala tren za kisasa vilevile POSTA iliyumba sana tulibakiwa na masanduku tu ya kupokea barua ambazo kwa ulimwengu wa sasa zimepitwa na wakati lakini sasa tunatuma na kupokea mizigo kutoka mataifa mbalimbali

Tunaomba mrejeshe shirika la TTCL ili Watanzani tujivunie kuwa na chetu na kuimarisha BRT kwasababu wananchi wanapata usumbufu mkubwa sana kwenye Mwendokasi
View attachment 3038081View attachment 3038082View attachment 3038083View attachment 3038084View attachment 3038085
Hakuna shirika hata moja hapo lililoimarika, yote hayo ni jini kamua damu, yanatumika na wakubwa kuibia pesa za watanzania.
 
Tutajie watu wangapi wamepata ajira,naona unatuletea hadithi za Abunuasi na nchi ya kusadikika.
 
Kumbe kuna kusubiri tena wakubwa wapande? Kwahiyo wao hawafuati ratiba ni ratiba ndio inawafwata wao!
Ni uzembe tu, yaani unawasubirisha abiria 200+ Kwa zaidi ya dakika 90 kwaajili ya abiria mmoja 🙌

Kwenye kushuka nayo ni hivyo hivyo, unasubiri nusu saa nzima ili protocal zao zifanyike kabla ya kushuka.

Hii Nchi kuendelea itachukua muda sana as Kuna watu wanachezea Kodi zetu watakavyo.
 
Posta hii ambayo Bwana Nape aliruka na chopa na kutumia billions of money kuweka vibao vya anawani za makazi akidai kuwa sasa barua zitaanza kuwa delivered home na sasa tunaelekea mwaka wa 4 hakuna kitu kama hicho. Sijui kwanini wabunge huwa hawahoji vitu kama hivi.
 
Pamoja na juhudi hizo, Kuna haja tukabadirisha namna ya Uendeshaji wake ili tujikite kibiashara zaidi.

Haya mashirika, ni Serikali yenyewe ndiyo itayaua.

Mathalani Viongozi wa mashirika hayo kuteuliwa na Mhe. Rais

Unakuta anapelekwa pale CEO ambaye ukiachana na Ukada wake wa Chama, Hana historia kwenye kufanya biashara hata Kwa Mwaka mmoja na akapata Faida.

Pia tuache Siasa kwenye biashara hizi Kwa hayo mashirika.

Mathalani Mwaka Jana, safari yetu ya ndege ilicheleweshwa Kwa saa 1 na dakika 25 zaidi kutokana na eti kumsubiria Kiongozi fulani wa Kiserikali apande.

Yaani ndege inatakiwa kuondoka saa 6:00 Mchana, lakini inaondoka saa 7:30 kisa tu kumsubiria Mkubwa wa Serikali afike na tuondoke naye.

Vitu vya kipuuzi kama hivi, vikiachwa viendelee wateja wataona bora apande basi ijulikane hivyo kuliko kusubirishana kijinga namna hiyo.

Kila abiria akizira kusafiri na ndege si mashirika yatakosa abiria hivyo kuathiri Uwekezaji huu Mkubwa uliofanywa Kwa Kodi zetu Wananchi🙌
Mheshimiwa ndege hafanyi safari kama bodaboda , mngekuwa mnapotea angani kila siku .

Ndege lazima ipate certificate of Airworthiness ili kujiridhisha flight iyo ni safari , kuna mengi yanafanyiwa utafiti kabla kama hali ya hewa , uangalizi wa vifaa . Tena katika mda wa akribu kabisa kabla ya safari .

Hii ni kwa usalama zaidi .

Ndege sio daladala za Mbagala rangi tatu au mabasi ya mkoani , la sivyo mkienda kinyume kila siku mtakuwa mnazika watu
 
Kwahiyo unataka kusema ndege zote tiketi ikiandikwa muda wa kuondoka/Kupaa ni saa 1 asubuhi basi zitatakiwa kuondoka saa 2:30 asubuhi ili kusubiria hiyo certificate airworthiness unayosema?

Sio mara moja ama mbili natumia Usafiri huu, nina ufahamu nao kiasi.

Ninavyoandika haya sio kwamba nina Nia mbaya, lengo ni Kwa Wenye mamlaka kuona namna ya kuboresha.

Serikali imetumia fedha nyingi za Walipa Kodi kufanya Uwekezaji huu. Tukiona kilichofanyika ni sahihi, tutapoteza wateja na hivyo kurudisha nyuma Uwekezaji uliofanyika.

Nashauri Kwa kuwa Viongozi huwa Wana safiri mara nyingi na usafiri huu, ni vyema ratiba zao zi -accomodate ratiba za ndege ama kama ndege watafata ratiba za hao Viongozi sawa.

Ila muhimu kama ndege ilitakiwa kuondoka saa 7 Mchana ili kumbeba na huyo Kiongozi basi abiria anapokata tiketi akate hiyo ya saa 7, badala ya kusema mnaondoka saa 7 badala yake mnaondoka saa 9 Jioni
 
Ndege lazima pafanyike mawasiliano ya kabla ndege sio rahsi kufanya safari kwa sababu ni usafiri salama ila ni hatari .

Inawezekana nusu saa kabla pakatokea hali ya hewa isiyo rafiki basi lazima wasitishe safari.
 
Nadhani hunielewi

Ndege ilisitishwa safari zake Kwa dakika 90 zaidi sio kwasababu ya hali mbaya ya hewa, ni kwasababu ya kumsubiria huyo Mheshimiwa.

Na wakati anaingia nilikuwa nimekaa siti ya dirishani, hivyo nilimuona tangu anaingia kwenye board. Na hata wakati wa kushuka pia nilimuona.

Najua una nia nzuri ya kutetea hichi kilichofanyika, ila waambie hili Shirika likifa ni Kodi zetu zitakuwa zimetumika vibaya.
 
Hatimaye Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuimarisha Mashirika yake matatu, TRC, Air Tanzania, POSTA, Wananchi tunasubiri TTCL na BRT.

Hongera sana Serikali ya Tanzania kwa kufanikiwa kurejesha heshima ya nchi iliyokuwa imepotea kwa muda mrefu mmejitahidi sana

Miakaka ya nyuma hatukuwa na ndege wala tren za kisasa vilevile POSTA iliyumba sana tulibakiwa na masanduku tu ya kupokea barua ambazo kwa ulimwengu wa sasa zimepitwa na wakati lakini sasa tunatuma na kupokea mizigo kutoka mataifa mbalimbali

Tunaomba mrejeshe shirika la TTCL ili Watanzani tujivunie kuwa na chetu na kuimarisha BRT kwasababu wananchi wanapata usumbufu mkubwa sana kwenye Mwendokasi
View attachment 3038081View attachment 3038082View attachment 3038083View attachment 3038084View attachment 3038085
mashirika yote yako taaban zoof lihali ila hapo kwenye BRT ndio balaaaaa kabisaaaaaa wanatakiwa kuuawa.
 
Serikali imetumia pesa nyingi sana kuwekeza ili yaimarike, suala, ni Je, wanayoyaendesha wataweza kuyaendesha kwa faida ya umma au yao binafsi?

Hesabu zao za matumizi na mapato yua kila mwaka tunaoneshwa?

Kwa Watanzania hayo ni ma "white elephant".
 
Waache kula sasa badala yake wakuze umakini unahitajika
 
Back
Top Bottom