Serikali ya Tanzania imesema, haitaruhusu kuingiza vifaranga vya kuku nchini na haitatoa tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo kuaniza Julai 30, 20

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Serikali ya Tanzania imesema, haitaruhusu kuingiza vifaranga vya kuku nchini na haitatoa tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo kuaniza Julai 30, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Jumamosi Julai 23, 2022 imesema Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema baada ya Julai 30, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na Serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.

Taarifa hiyo imesema, Ulega amebainisha hayo jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo,

Lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo Serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi.

Akifungua kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Ulega amesema Serikali inategemea haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi.

Ametaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga vya kuku kuanzia wazalishaji wakubwa hadi wadogo ambao wamesajiliwa na kutoa taarifa serikalini ili kuiwezesha kujua kiwango cha uzalishaji na kuwa na takwimu sahihi juu ya mahitaji ya vifaranga nchini.

“Ni mategemeo yetu ni kutokuona baada ya tarehe 30 mtu anaingiza vifaranga hapa nchini kutoka mahali popote pale, jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi,” amesema Ulega

Ulega amesema tasnia hiyo imekua kwa kasi miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo kwa soko linalotokana na ongezeko la watu na kipato, ongezeko la uwekezaji na uwepo wa mazingira bora ya uwekezaji katika tasnia ya kuku, urahisi wa kufuga kuku na uwezekano mkubwa wa kuwamiliki kuliko wanyama wakubwa.
 
Piga nikupige, Nyang'au.

Jamaa wajinga sana ndio mana jembe alivichoma.
Mkuu 'Liwagu'

Unapotosha kwa maksudi tu, au hukuisoma hiyo taarifa iliyoandikwa.

Kwani nikiagiza vifaranga toka Zambia itakuwaje?
 
Soko la ndani litatosheleza mahitaji na bei itakuwa rafiki? Au ni siasa
 
Tabia za watanzania zinajulikana hasa kwenye kutengeneza u-monopoly wakiona competition ni ndogo, kitakachoenda kutokea uhaba wa vifaranga lazima utokee kwa kuwa watanzania si wazuri kwenye kuzalisha na uzalishaji ukiwa mdogo huku uhitaji ni mkubwa bei itakuwa kubwa. je, Serikali imejiandaaje kwa hili?
 
Serikali ya Tanzania imesema, haitaruhusu kuingiza vifaranga vya kuku nchini na haitatoa tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo kuaniza Julai 30, 2022.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Jumamosi Julai 23, 2022 imesema Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema baada ya Julai 30, hakuna vifaranga vya kuku vitakavyoingizwa hapa nchini na Serikali haitoi tena vibali vya kuingiza vifaranga hivyo.

Taarifa hiyo imesema, Ulega amebainisha hayo jijini Dodoma wakati wa kikao cha wizara na wadau wa tasnia ya kuku, kujadili namna ya kukuza tasnia hiyo,

Lengo la hatua hiyo ni utekelezaji wa sheria ya mwaka 2006 ambapo Serikali imekuwa ikizuia uingizaji wa vifaranga nchini kutoka nje ya nchi ili kudhibiti ugonjwa wa mafua ya ndege kwa mifugo jamii ya ndege na kulinda wazalishaji wa kuku ndani ya nchi.

Akifungua kikao hicho kilichojadili ajenda mbalimbali zikiwemo za upatikanaji wa vifaranga vya kuku, chakula cha kuku na bei ya kuku sokoni, Ulega amesema Serikali inategemea haitaona vifaranga vinaingizwa nchini kutoka nje ya nchi.

Ametaka kuwepo kwa mfumo wa taarifa zinazohusu wazalishaji wa vifaranga vya kuku kuanzia wazalishaji wakubwa hadi wadogo ambao wamesajiliwa na kutoa taarifa serikalini ili kuiwezesha kujua kiwango cha uzalishaji na kuwa na takwimu sahihi juu ya mahitaji ya vifaranga nchini.

“Ni mategemeo yetu ni kutokuona baada ya tarehe 30 mtu anaingiza vifaranga hapa nchini kutoka mahali popote pale, jambo la pili kuwepo na mfumo ambao utasaidia serikali kujua ni kiasi gani cha uzalishaji vifaranga ndani ya nchi yetu ili kujipima uwezo wetu na mahitaji yetu ndani ya nchi,” amesema Ulega

Ulega amesema tasnia hiyo imekua kwa kasi miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwepo kwa soko linalotokana na ongezeko la watu na kipato, ongezeko la uwekezaji na uwepo wa mazingira bora ya uwekezaji katika tasnia ya kuku, urahisi wa kufuga kuku na uwezekano mkubwa wa kuwamiliki kuliko wanyama wakubwa.
Mada hii imekwishajadiliwa humu JF.

Wizara hawana hata takwimu za idadi ya vifaranga vinavyozalishwa nchini, lakini wanapiga marufuku kuingiza vifaranga, halafu ndipo waanze kukusanya taarifa ambazo zingewasaidia kutoa uamzi wa kuingiza au kutoingiza.

Nchi yetu hii imekuwa na upumbavu wa kipekee sana.
 
Mkuu 'Liwagu'

Unapotosha kwa maksudi tu, au hukuisoma hiyo taarifa iliyoandikwa.

Kwani nikiagiza vifaranga toka Zambia itakuwaje?

Acha kuweka mawazoyako kichwani kwangu mkuu, kwani nimepotosha nini hapo.
 
Andiko hilo halionyeshi mahali popote kuwa hatua hiyo ya serikali imetokana na hao Manyang'ao unaowaweka wewe.

Huoni kuwa huo ni upotoshaji?
 
Manyang'ao ndio kitugani.
 
Marufuku vifaranga kutoka nje kwazuwa maoni tofauti.

Naibu waziri wa uvuvi na mifungo kweli umejua kunifurahisha, Mwenyezi Mungu awe pamoja nawe, na akujaalie mwisho mwema ewe naibu waziri, ABDALLAH, kwakweli anaulizwa maswali na mwandishi wa habari bwana JAMAL HASHIM, na majibu yake anayajibu kwa kujiamini sana, hatetereki, wala hana unafiki.

Kwakweli amenifurahisha sana, especially hapo alipotamka neno
"MSAHAFU" 👉🏽kwahivyo si msahafu wa kusema bwana huu haubadilishiki"👈🏽
 
Back
Top Bottom