Serikali ya Tanzania imesema inatarajia kuanza kutoa huduma ya upandikizaji wa mimba (IVF)

Wale wanawake wanaosema wameolewa ili wapate watoto wanajiuliza bora wazae na mwanaume au bomba la sindano[emoji23][emoji23]
 
Nafikiri ni vyema ufike wakati sheria itungwe ya watu wanaotaka kijitolea mbegu wajitolee, watu wana mbegu kibao hadi wanamwaga bafuni kwanini mwingine anunue kwa 10ml?

Ikitungwa nitakuwa wa kwanzwa ku donate
 
Serikali ya Tanzania hivi karibuni inatarajia kuanza kutoa huduma ya upandikizaji wa mimba (IVF) kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22.

Hayo yamesemwa na Waziri waAfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri Dk Dorothy Gwajima alipokuwa akiwasilisha bajeti kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2021/22.

Pia huduma za upandikizaji wa uboho (yaani rojorojo lililoko katika mifupa) ama bone marrow kwa Kiingereza kwa wagonjwa wenye saratani ya damu.

‘’Tutaendelea kutoa huduma zote za kibingwa kama vile upasuaji wa kutumia tundi dogo,upasuaji wa kichwa, shingo na koo, ‘’. alisema waziri Gwajima.

Huduma hiyo inaanza ikiwa ni miaka miwili sasa imepita tangu Hospitali ya Taifa Muhimbili kuanza maandalizi ya utoaji wa huduma hiyo ikiwemo kusomesha wataalamu na kuandaa jengo litakalotumika kutolea huduma hiyo.
 
Nafikiri ni vyema ufike wakati sheria itungwe ya watu wanaotaka kijitolea mbegu wajitolee, watu wana mbegu kibao hadi wanamwaga bafuni kwanini mwingine anunue kwa 10ml?

Ikitungwa nitakuwa wa kwanzwa ku donate
Hao wanaomwaga bafuni wana donate kwa mapepo
 
Tuanzie hapa, nini chanzo cha hii changamoto kuongezeka kwa kasi namna hii
Je ni hewa tunayovuta?
Je ni maji tunayokunywa?
Je ni kasi ya teknolojia?
Hakuna kilichoongezeka kwa kasi.haya mi maradhi tu na vilema vya watu na ni vitu ambavyo vipo toka zamani ndo maana watu wameumiza kichwa kutafuta suluhisho.
 
Hao jamaa unaoangaika kuwataja kila saa hadi hadi waje wakuzalishe ndo utatulia.naona unawashwa sana.wenzako wanaleta mada za maana wewe unakuja na ujinga.
 
Afadhali manake ile IVF clinic bei zao unanunua Alphard.
 
wakuu habri zenu i hope safari hii muhimbili wataanzisha kweli

upandikizaji wa mimba, mkiangalia gazeti la leo

habari leo,
wameweka kihead line juu hapo kama mtu anamaelezo zaidi tunaomba atupe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…