Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 44,096 na kupandisha madaraja watumishi 92, 619

Huyu Waziri toka 2016 mpaka leo Hadithi ni hii hii hakuna jipya hapo
 
Serikali kuajiri kwa wingi wakati huu iko sahihi sababu asilimia kubwa ya miundo mbinu iomeshajengwa hivyo mfanyakazi wa serikali hata akijikopea kagari kake used kataweza kudumu bila shida barabara nyingi nzuri

Kinachotakiwa kwa sasa serikali isiongeze sana miradi mipya iwe kidogo sana imalizie iliyopo ili serikali iwe na extra ya kulipa wafanyayakazi nyongeza nk

Bajeti ya miradi ya maendeleo inabidi ishuke sana hili kila mwananchi anatakiwa kulijua kuwa huwezi kila siuku familia ile pilau hela ukiwa nayo ndogo na wakati huo huo ujenge gorofa!!!
 
uongo vyuo vyetu vyote ukijumlisha vinatoa graduate 1200 tu wa ualimu kwa mwaka ukipiga kwa miaka 20 nyuma ni elfu 24 tu!! hiyo laki tano umeitoa wapi?
Ndugu hivi uko tanzania ya wapi hiyo au bado uko fm6

Udsm Baed tu ni zaidi ya 1000
Bado Bed kama 300
Bado wale wa science Conas 300
Bado coed special need kama 300

Haya Bado branches za udsm Duce na Muce chuo kizima kinatoa degree za education tu

Nenda udom ndio inaongoza kwa udahili utachoka asee hao 1200 ni udom pekee inatema na zaidi,

Hapo sijagusia vyuo vingine vya kati na waajiriwa wengi wanatoka humo.
 
Laah Inaonekana awamu ya tano hii inayoombewa ati iwe na distinguished Legacy haikuajiri hata mtumishi mmoja - likewise haikupandisha daraja mfanyakazi yoyote - Kweli nchi imepata Uhuru wake tena. (Freedom is back baada ya mwendazake kufanya yake)

Ushauri: Wangesubiri subiri watu wasahau sahau kwanza ndipo waanze kumwaga hizi neema.
 
Iboreshwe uku ikitoa ajira ndio formula
 
Miaka 5 bila ajira wahitimu laki tano maana yake kila mwaka wahitimu laki moja wa ualimu.
 
Huu ni mpango wa kuharibu legacy ya magufuli
Dah cjui unawaza nn ndugu..kwa hio serikali isifanye chochote ..maaana kwa mtazamo wako wakiajir itakua wanataka kuharaib legacy ya magu hata wakijenga miundo mbinu bhc itakua wanataka kuharib legacy ..kwa maana hio nchi isifanye jambo lolote la kimaendeleo ili tuzid kumkumbuka huyo magu
 
Mkuu huoni wakiajiriwa hawa automatic sekta binafsi nayo inaneemeka?

Chukulia mfano average wanalipwa laki 5 kwa mwezi, hizo ni kama Bilioni 20 kwa mwezi zinaenda kwenye mabeki, maduka ya nguo, vyakula, viatu, vocha etc.

Sekta binafsi pia inaweza kukua kukiwa na mzunguko wa pesa, mtu hawezi kuja kuwekeza ikiwa purchasing power ni ndogo.
 
Huyo ni mpiga propaganda achananae.
 
Annual increments na nyongeza ya ziada ya mishahara ipo au tuendelee kuchapika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…