Binafsi sikubaliani na huu mfumo wa ajira wa sasa wa kutegemea ajira za serikali tu.
Serikali iboreshe mazingira watu wengi waajiriwe na sekta binafsi.
Serikali itaajiri hadi lini? Kwa presha ya sasa itabidi kila mwaka serikali ilazimike kuajiri ili kuwaziba watu midomo lakini hii sio njia nzuri ya kutatua tatizo.
Kwa mtindo huu wa kutegemea ajira za serikali na serikali ikawa inaajiri kila mwaka itafika wakati mapato yote na makusanyo yanaishia kwenye kulipana mishahara tu.
Serikali kwanza irekebishe mifumo, isambaze pesa sekta binafsi. Pili ipitie upya muundo wa watumishi wake. Unaenda shule za mjini waalimu 80, shule za vijijini waalimu 2.
Kabla ya kufikiria kuajiri, kwanza pitia miundo upya, boresha mazingira ya hao watumishi waliopo watafanya kazi kwa morali, mfano mwalimu leo analipwa 720,000. Unataka utajiri mwalimu mwingine, wakati hiyo hela ya mwalimu mpya ukiboresha mazingira kwa mwalimu aliepo ukamlipa 1M ama 1.1M, huyu atakua moralized sana na atafanya kazi hata ya waalimu 2.
Tuboreshe sekta binafsi kwanza, pili tuboreshe maslahi ya watumishi tulionao kabla ya kufikiria kuajiri wapya.