Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 44,096 na kupandisha madaraja watumishi 92, 619

Vipi ajira za Wizara ya nishati,ikiwemo tanesco, TPDC,pura,ewura, wizara ya madini, wizara ya ujenzi, miundombinu na mawasiliano . Wizara ya fedha, bot, tra. Au ajira za huko ni kugawana wakubwa,? Mnakimbilia ualimu kila mara
 
Kwani nani alimzuia Magufuli kwa ajiri watu. Isipokua roho mbaya ubinafsi ukabira ukanda kafikiri Tz imekua mari yake binfsi na ndg zake bora kafa tu.
Acha hazira za neutrophil aliyesisimka😂😜!
 
uongo vyuo vyetu vyote ukijumlisha vinatoa graduate 1200 tu wa ualimu kwa mwaka ukipiga kwa miaka 20 nyuma ni elfu 24 tu!! hiyo laki tano umeitoa wapi?
Sekta ya elimu wameajiriwa technicians wa maabara mbalimbali, umeme, civil/architectural, electronics, chemistry/biological etc...

Hivyo na hawa wana soma kozi ambazo sio za elimu ktk vyuo vya ngazi ya veta na technical colleges kama arusha tech, Must, Dit etc

Ina wezekana ndg alikuwa ana zungumzia wadau hao waelimu sababu kuna technical schools pia, shule za kilimo kama kibiti boys kilosa etc...

Ukiwa una toa ufafanuzi basi anza kuuliza kwanza kama amelenga kitu gani...

Mtaani watu hawana ajira tangu 2013... Mpaka sasa 2020 ni miaka saba nq walio pata ajira ni wachache... Kuqnzia ngazi ya certificate, diploma mpaka degree na kuendelea
 
Mashirika yana taratibu zake za Ajira kupitia Sekretarieti ya Ajira.
Nilitaka usema hayo,sekretariet ya ajira, ni bomu litalipuka soon . Ajira zote zirudishwe kwenye wizara husika . Sekretariet huwa haitoi nafasi za juu, ni wahudimu na Ps. Zile nafasi muhimu zinajazwa kihuni
 
Nilitaka usema hayo,sekretariet ya ajira, ni bomu litalipuka soon . Ajira zote zirudishwe kwenye wizara husika . Sekretariet huwa haitoi nafasi za juu, ni wahudimu na Ps. Zile nafasi muhimu zinajazwa kihuni
Sasa huko Wizarani ndio wataacha kuwekana. At least kupitia Sekretarieti kunakuwa na uwazi fulani kidogo.
 
Tena hawa wakiajiriwa inakuwa ni chanzo cha mapato ya serikali kupitia kodi.
 
uongo vyuo vyetu vyote ukijumlisha vinatoa graduate 1200 tu wa ualimu kwa mwaka ukipiga kwa miaka 20 nyuma ni elfu 24 tu!! hiyo laki tano umeitoa wapi?
we
uongo vyuo vyetu vyote ukijumlisha vinatoa graduate 1200 tu wa ualimu kwa mwaka ukipiga kwa miaka 20 nyuma ni elfu 24 tu!! hiyo laki tano umeitoa wapi?
wewe ndo muongo, nimemaliza UDSM 2015 namba yangu 01366 surname yangu inaanza na M , rafiki yangu surname yake A inaanza reg no yake ni 00730 sasa mwenye surname inayoanza na na Z atakuwa na reg no ngapi? Mahaba yakizid hupunguza uwezo wa kufiri, hicho ni chuo kimoja tu je hapa nchini kuna vyuo vingapi?
 
Huu ni mpango wa kuharibu legacy ya magufuli
Kwamba watu wasiajiriwe, wasipandishwe madaraja na kulipwa malimbikizo ya mishahara ili kulinda legacy ya mtu?
After all, nani hapendi kutengeneza legacy yake?
Kiongozi yeyote hata ngazi ya kijiji & kitongoji lazima uwe na followers.
Utawapataje kama siyo kwa kutenda yanayostahili kutendwa kwa wakati?
 
Unarudi nyuma au unarudi kinyume kinyume?! Unamsaliti mwendazake kwa kumbusuuu?!!
 
Huu ni mpango wa kuharibu legacy ya magufuli

Waganga na walozi nao warudishe vile vibao vyao vya kutangaza amali zao mabarabarani na mitaani. Mwendazake aliwaharabia ajira zao pale alipo hamasisha kumtegemea Mungu kwanza.

Na watapiga fedha wakiongezea kwenye matangazo yao kuwa wana dawa ya kinga ya jini funika legacy kutoka Anjuan.
 
Mh. Hakimu unaweza kutuambia kuwa...
Je, watu waliosomea ualimu wanaweza kuajiriwa katika sekta gani binafsi tofauti na shule za binafsi licha ya kuwa waajiri katika shule hizi wanawasimanga walimu wahanga wa ajira? Na ni kwa kiwango gani sekta binafsi inaweza kutoa ajira kwa walimu?...
Je, ni maeneo gani mtu aliyesomea ualimu yaani MWALIMU anaweza kujiajiri tofauti na kufundisha?
.
ANGALIZO: Hadhi ya walimu iheshimiwe kwani kuna watu walioshiba hadi kusahau wengine hawakawii kuwaambia walimu kuwa wasitegemee serikali iwaajiri kwani kuna fursa nyingi za kujiajiri hata kuokota chupa za plastic, vyuma chakavu, n.k kuwa nazo ni fursa tosha ambazo mwalimu anaweza kuzitumia kujiingizia kipato!
Narudia hayo ni maneno/mawazo ya watu walioshiba na kuwasahau wenye njaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…