Serikali ya Tanzania kuajiri watumishi 44,096 na kupandisha madaraja watumishi 92, 619

Umepata wapi data. Kuna graduates, kuna diploma, kuna certificate.... Vyuo vya ualimu vipo vingapi halafu useme 1200
JF ya zamani tofauti na ya sasa kabisa, yeye anamwita mwenzie muongo kumbe yeye ndo muongo kabisa
 
uongo vyuo vyetu vyote ukijumlisha vinatoa graduate 1200 tu wa ualimu kwa mwaka ukipiga kwa miaka 20 nyuma ni elfu 24 tu!! hiyo laki tano umeitoa wapi?
Wewe hujasoma vyuo naona.
Hebu ulizia wahitimu wa kozi ya ualimu pale udom mwaka jana.
Kumbe Kuna watu huwa mnaongea ongea tu!
 
bora tu watu wapate ajira sio wote tujiajiri sasa tutamuuzia nani. tupate wateja wapya na hela izunguke
 
afanye hivyo fasta kamzunguko ka pesa kaongezeke mifukoni. watu mtaani hawana kazi, hawana pesa. ni term hii tu mtu aliwahi kumaliza chuo akakaa miaka mitano bila kupata kazi yeyote hata ya kujishikiza tu. wahitimu wengi wameenda kuwa wakulima, wengine wameenda kuwa wanasiasa yaani shida tupu.
 
uongo vyuo vyetu vyote ukijumlisha vinatoa graduate 1200 tu wa ualimu kwa mwaka ukipiga kwa miaka 20 nyuma ni elfu 24 tu!! hiyo laki tano umeitoa wapi?
Kwa ualimu pekee ni zaidi ya laki moja maana serikal haijaajiri kwa miaka mingi kwa laki tano labda na sekta nyingine ila hiyo takwimu ya graduate 1200 sio kwel ni chache mno
 
afanye hivyo fasta kamzunguko ka pesa kaongezeke mifukoni. watu mtaani hawana kazi, hawana pesa. ni term hii tu mtu aliwahi kumaliza chuo akakaa miaka mitano bila kupata kazi yeyote hata ya kujishikiza tu. wahitimu wengi wameenda kuwa wakulima, wengine wameenda kuwa wanasiasa yaani shida tupu.
 
Pongezi kwa Mhe. Rais pia kwa Waziri wa Utumishi Mhe. Mchengelwa kwa kudhamiria kurudisha heshima kwa watumishi wa Umma maaana walifikia hatua mbaya sana, walilia sana mpaka machozi yamewa kauka, wamedai haki zao kwa kipindi kirefu sana!!
wamelalamika sana!! wametaabika sana!! wamedhalalika sana!!

kwa dhamira hii ya serikali ya awamu ya 6 kwa watumishi wa umma, hakika Mungu atazidisha neema na Baraka ktk Taifa letu.
 
JWZT sio watumishi wa umma kwa maana ya utumishi. Wana taratibu zao tofauti kidogo na watumishi wengine wa serikali.

Hawalindwi na sheria za utumishi wa umma.

Hilo halina maana kua hawalipwi mshahara kutoka kwenye pesa za umma.
Kwan polisi ni watumishi wa umma?
 
Mungu amzidishie baraka mama yetu
 
mkuu tshs 720,000/= kwa mwalimu wa shule ya kata ni ndogo? siuache ufungue duka ujiajiri
 
Huu ni uongo
 
mkuu tshs 720,000/= kwa mwalimu wa shule ya kata ni ndogo? siuache ufungue duka ujiajiri
Hiyo ni kwa mwalimu wa degree, unafahamu wa certificate analipwa sh ngapi?
 
Hiyo ni kwa mwalimu wa degree, unafahamu wa certificate analipwa sh ngapi?
hiyo degree ya geography na history hiyo hela nyingi hivyo kwa kazi gani unayofanya? naona tuanzishe opras na walimu waajiriwe kwa mkataba wa miaka mitatu mitatu kama Elitrea
 
hiyo degree ya geography na history hiyo hela nyingi hivyo kwa kazi gani unayofanya? naona tuanzishe opras na walimu waajiriwe kwa mkataba wa miaka mitatu mitatu kama Elitrea
Hujajibu swali, certificate analipwa ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…