mugomangara
JF-Expert Member
- Jul 7, 2019
- 259
- 671
Kumekuwa na sintofahamu baada ya Trump kuzuia misaada kwa nchi mbambali kutokana na kile anachokiita misaada hiyo kutoinufaisha Marekani moja kwa moja. Hapa nchini marufuku hiii imezua mijadala mingi sana ikiwemo kwenye jukwaa letu hili pendwa. Watu mbali mbali wamekuwa wakionekana kufurahia swala hili na kufikia hatua ya kuzitaka serikali ianze kujitegemea kwa kutumia rasilimali nyingi zilizopo kutoa huduma zilizositishwa na Trump. Katika baadhi ya mijadala wapo watu wamefikia hadi hatua ya kufurahia wenzao kukosa kazi kwenye mashirika mbali mbali yasiyo ya serikali (NGOs) kwa kile wanachosema watu hawa walikuwa wanaringa sana kutokana na maslahi makubwa waliyokuwa wakipata
Japo sipingani na hoja ya kutaka mataifa ya ki Afrika kupunguza kutegemea misaada kutoka kwa wahisani lakini ukweli na uhalisia ni kwamba viongozi wengi wa nchi za ki Afrika hawana muda na hawawajali wanachi wao. Na kwa hivyo misaada hiyo ikikosekana tusitegemee vipaumbele kubadilika. Hizi ni nchi ambazo viongozi wako tayari raia wale nyasi ili wanunue ndege ya rais na magari ya kifahari kwa ajili ya viongozi. Ni nchi ambazo wananchi wakilalalamika kuhusu tozo na kodi mbali mbali wanaambiwa wahame nchi.
Ni nchi ambazo viongozi wanathaminiwa kuliko wananchi, mnaweza mkasimamishwa zaidi ya dakika 40 mkisubiri msafara wa kiongozi upite bila kujali mnawahi wapi. Hizi nchi amabazo raia wanaotoa kodi wanaweza kuwa wanapita barabara mbovu yenye mashimo kila siku na hakuna anayejali lakini akija kiongozi mkuu wa chama tawala mashimo yote yanafukiwa siku hiyo hiyo
Trump ni mfanyabiashara na kwa hivyo kila kitu kwake ni mauziano (nakupa hiki na we nipe kile) tumeona mifano mingi ya nchi kama Canada na Mexico alivyoweka tariffs lakini baada ya kufanya naye mazungumzo na kumwahidi mambo aliyokuwa anataka kasogeza muda wa tarrifs kwa siku 30 na inawezekana akaondoa kabisa. Wakati wanasitisha misaada hiyo, waziri wa mambo ya nje (secretary of state) Bwana Rubio alisema wanataka waangalie misaada hiyo inanufaisha vipi Marekani.
Ni wakati muafaka kwa wana diplomasia wa nchi yetu kuongea na Trump na kumsikiliza anataka nini. Kama tumeweza kuwapa waarabu Ngorongoro na bandari huku wachina tukiwazawadia gesi kwanini tusitafute cha kuwapa wamarekani. Wao wanatupa misaada inayonufaisha watu wengi lakini mikataba ya madini na uwekezaji mingi tunawapa wachina, waarabu na waturuki, lazima wasione faida ya misaada yao. Na wakati mwingine tunawadhihaki na kuwaita mabeberu. Hawa waarabu na wachina wanatoa misaada gani? Wengine hapa misaada yao ni tende na kujenga tu nyumba za ibada, wachina ndo kwanza wameanza hadi kufanya kazi za wazawa na si tunawaangalia tu.
Na kwa wale mnaofurahia mnajua hasara kwa nchi na uchumi kwa ujumla? Kuna NGO hapa wilayani inapeleka PAYE zaidi ya Tsh 11M kwa mwezi, kuna NGO ngapi nchi hii? Vipi pesa wanayopeleka NSSF na PSSSF?. Wanatoa tender za magari, insurance na stationeries kwa wadau wengi tu. Nchi yetu ina uwezo wa kuwaajiri wafanyakazi wote kama watapoteza kazi? Familia ngapi zinawategemea?
Hivi unajua wafanyakazi hawa huwa wanajua kutumia pesa ipasavyo na kusababisha mzunguko mkubwa wa pesa? Waulize watu wenye baa, lodge na hotel jinsi wanavyopata pesa hawa jamaa wakienda semina na mafunzo mbali mbali na mapumziko (retreat). Kama una hotel au mgahawa na unawategemea wafanyakazi wa serikalini jiandae kuufunga, mara nyingi wanakunywa chai ya rangi na chapati au andazi. Ukiwatajia bei ya supu ya samaki au kuku wanatoa macho utafikiri umewaambia rangi ya nguo ya ndani ya wapenzi wao. Na hawa ndio wanaongoza kwa kuwakejeli wafanyakazi wa hizi NGO. Hawa watu wanajenga nyumba za hatari na mafundi wananufaika, faida ni nyingi sana. Wafanyabiashara wengi wanajua umuhimu wa hawa watu.
Ni wakati muafaka sasa kwa Balozi wetu wa USA, na wanadiplomasia wote kuzngumza na wenzao ili hali isiharibike zaidi
Soma: Pre GE2025 - Wabunge waiomba Serikali kuwatumia watumishi walisimamishwa kazi USAID