Serikali ya Tanzania mshawishini Trump arejeshe misaada

Lakini ujue yeye binafsi hatapata hasara sababu kodi zetu zipo. Raia wa kawaida ndo tutapata shida
Wote tutapata shida..
Ikiwa misaada ya US itakatwa na serikali haijajipanga kuziba pengo hilo, wananchi watahisi athari moja kwa moja, hasa katika sekta za afya, elimu, na upatikanaji wa chakula, kupungua kwa dawa za ukmw,miradi ya afya inaweza kuchochea hasira ya wananchi na hapa ndipo patamu sana...

Ikiwa Marekani itaondoa AGOA na biashara za Afrika zitapoteza soko la US, viwanda vinavyouza bidhaa kama mavazi na bidhaa za kilimo vinaweza kufungwa, na kusababisha ukosefu wa ajira hapa ni patamu sana sana... kwani wananchi wanaoweza kuathirika moja kwa moja wanaweza kuandamana kupinga hali ngumu ya maisha...(hapa wameanza kupata akili na kuacha kufuatilia Zuchu na Diamond, Aziz Ki na Mobeto, Simba na Yanga)

Kwa sababu viongozi wamekuwa wakitumia misaada kwa manufaa binafsi, wananchi wanaweza kuona upungufu wa misaada kama uthibitisho wa ufisadi wa serikali... hapa patamu sana tena sana ... kwani Ikiwa wananchi walikuwa hawaoni faida ya misaada hata kabla ya kukatwa, kukosekana kabisa kwa fedha hizo kunaweza kuzidisha hali ya kuchoshwa na uongozi mbaya....


Sasa ndipo kina mzee Tundu na wenzake wanatia timu panazidi kunoga zaidi.. kwani upinzani na wanaharakati wanaweza kutumia hali hii kama nafasi ya kushinikiza mabadiliko ya uongozi kwa kuhamasisha maandamano. Mitandao ya kijamii ikiwemo X na jf havitokaa mbali, inaweza kuongeza uhamasishaji na kusababisha maandamano makubwa zaidi.

Tumeshuhudia kwa wenzetu Kenya hapo maandamano dhidi ya serikali kwa sababu ya hali ngumu ya maisha, kodi kubwa, na ukosefu wa ajira.

Hivyo Ulaya, US, China, wazidi kukaza ili akili itukae sawa...
 
Mada ndefu afu umeandika upumbavu wako.
 
Una logic nzuri sana, wasiwasi wangu ni kwamba ni raia wachache sana nchi wanaweza kuandamana na kuishinikiza serikali kutokana na aidha kukosa elimu au uoga na uchawa uliopitiliza. Kuna mambo ya hovyo sana nchi hii toka kitambo lakini watu wanakufa kimya kimya. Hata wasomi wetu wa kuelimisha raia na kuwa mstari wa mbele wengi wao wameamua kuwa machawa tu
 
We ni mojawapo siyo, hujajiwekea akiba? Au ndiyo umeziponda zote km unavyowasifu kwa manunuzi na ulevi wao baa
 
Misaada ya neti, mseto, na arv ndio inafika kwa maskini lakini misaada ya fedha inaishia mifukoni mwao watawala, Trump afinye hapo hapo
Sasa wakikata na hiyo misaada si ndo hao raia watakufa ndugu. Hakuna atakayewajali nchi hii
 
We ni mojawapo siyo, hujajiwekea akiba? Au ndiyo umeziponda zote km unavyowasifu kwa manunuzi na ulevi wao baa
Mimi sio mmoja wapo lakini naliangalia swala hili kwa mapana yake. Kodi, ajira na kwa wafanya biashara na uchumi kwa ujumla
 
Mkuu linapokuja suala maisha ya wananchi kuathirika moja kwa moja lazima wataweka hofu pembeni..
ugumu w maisha ukifikia kiwango kisichovumilika, hata wale waliokuwa na hofu wanaweza kuona haja ya kuchukua hatua na hapo ndipo vyama vya upinzani au wanaharakati watahamasisha wananchi na kupata mwitikio mkubwa, maandamano yanaweza kutokea.

Trump aendelee kushikilia hapo hapo...
 
Daaa Kuna majitu yamenenepeana serikalin huko, yaan unakuta jitu linapumua kama limo kwenye chupa. Ukiulizia ni nani huyo utasikia ni afisa wa tra, mkurugez wa tanesko, mkurugenz wa nida, mkuu tanapa,mshauri wa mama yaan.
 
Acha tusonge hivihivi kuna baadhi ya mafuvu hayajifunzi Kwa kuambiwa Bali Kwa maumivu

Huruma siyo malezi
 
Daaa Kuna majitu yamenenepeana serikalin huko, yaan unakuta jitu linapumua kama limo kwenye chupa. Ukiulizia ni nani huyo utasikia ni afisa wa tra, mkurugez wa tanesko, mkurugenz wa nida, mkuu tanapa,mshauri wa mama yaan.
Hawa jamaa hata misaada ikikata hawajali na wala hawatahangaika kusaidia watu. Wao wana uhakika
 
Msaada siyo lazima, hizo ni kodi za wananchi kama nyie wa U.S.A. Jifunzeni kujitegemea na muanze kuhoji matumizi ya kodi zenu.
 
Msaada siyo lazima, hizo ni kodi za wananchi kama nyie wa U.S.A. Jifunzeni kujitegemea na muanze kuhoji matumizi ya kodi zenu.
Lakini mapato yetu madogo kuliko mahitaji. Bila misaada na mikopo hatutoboi
 
Tuchapwe viboko nchi nzima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…