Serikali ya Tanzania na wezi wake - Sera ya kutumbua

Shocker

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2012
Posts
1,958
Reaction score
3,890
Sera ya kutumbua kisha ndio imetoka, ni dili ambazo huhitaji tena kufanya kazi serikalini.

Tumezoea kusikia enzi zile za rais Magufuli mara amemtumbua huyu mara amemtumbua yule ni wengi sana wametumbuliwa na wananchi wakishangilia wasiyokuwa na ujuzi wala uelewa nayo.

1) Watanzania niwaulize, nini faida ya kutumbuana huko?
2) Kitu gani kilifuata baada ya mtu kutumbuliwa?
3) Orodha ya waliotumbuliwa unaijua? Yupo yeyote aliefikishwa mahakamani na ukaisikia hukumu? Je, ni wote walifikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa sababu zilizowapelekea wao kutumbuliwa haswa pale palipoonekana hela imetafunwa?
4) Nililoliona ni kusikia utapangiwa shemu nyengine, hii nini maana yake?

Kutumbuana bila ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria ni unafiki na uzandiki dhidi ya wananchi, haswa pale panapohusishwa na upotevu au ubadhirifu wa fedha.

Eti mtu anambiwa arudishe hela ili asamehewe hii miCCM inaita eti ndio msamaha.
 
Mwendazake alitoa wafanyakazi feki akaweka wabunge feki.
 
Hii nchi ifike mahali matumizi mabaya ya pesa ya walipa kodi yapunguzwe
TEUZI NYINGI NI ZA KUPEANA PASIPO KUJALI UMUHIMU NA HASARA ZA CHEO HICHO
Mama Samia punguza matumizi
Hizi teuzi hazina tija ni bora mkabaki watu kumi mkaongoza vyema kuliko utitiri wa uteuzi usio na maana

Punguza Bunge
Punguza au komesha teuzi
Serikali ina matumizi makubwa mno kuliko nchi tajiri
Tuoneeni huruma walipa kodi
 
Sera ya kutumbua kisha ndio imetoka, ni dili ambazo huhitaji tena kufanya kazi serikalini.

Tumezoea kusikia enzi zile za rais Magufuli mara amemtumbua huyu mara amemtumbua yule ni wengi sana wametumbuliwa na wananchi wakishangilia wasiyokuwa na ujuzi wala uelewa nayo.

1) Watanzania niwaulize, nini faida ya kutumbuana huko?
2) Kitu gani kilifuata baada ya mtu kutumbuliwa?
3) Orodha ya waliotumbuliwa unaijua? Yupo yeyote aliefikishwa mahakamani na ukaisikia hukumu? Je, ni wote walifikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa sababu zilizowapelekea wao kutumbuliwa haswa pale palipoonekana hela imetafunwa?
4) Nililoliona ni kusikia utapangiwa shemu nyengine, hii nini maana yake?

Kutumbuana bila ya kufikishana kwenye vyombo vya sheria ni unafiki na uzandiki dhidi ya wananchi, haswa pale panapohusishwa na upotevu au ubadhirifu wa fedha.

Eti mtu anambiwa arudishe hela ili asamehewe hii miCCM inaita eti ndio msamaha.
Kutumbua kulitengeneza wafanyakazi hewa kimshahara ambao bado wanalipwa mshahara ulele
 
Back
Top Bottom