Wakuu,
Katika ulimwengu wa siasa na diplomasia za kimataifa, taswira ni kila kitu. Lakini taswira hiyo inagharimu kiasi gani, na ni nani anayelipa ankara hiyo?
Uchunguzi wa kina umebaini mkataba wa kushtusha wa Dola za Marekani milioni 3 (takriban Shilingi bilioni 7.8 za Kitanzania) ulioingiwa kimya kimya kati ya Tanzania na kampuni kubwa ya ushawishi na uhusiano wa umma (PR) yenye makao yake jijini Washington, D.C., inayojulikana kama BGR Group.
Mkataba huu wa mwaka mmoja, ulioanza kutekelezwa rasmi Juni 15, 2026, unaibua maswali mazito: Je, kodi za Watanzania zinatumika kuficha makovu ya ukiukwaji wa haki za binadamu na machafuko ya kisiasa badala ya kutatua changamoto za kimsingi zinazolikabili taifa hili?
Nini Kiko Ndani ya Mkataba?
Kwa mujibu wa nyaraka zinazohusiana na mkataba huu, kutoka mtandao wa habari za PR wa O'Dwyer's, kampuni ya BGR italipwa kitita cha Dola 250,000 (zaidi ya Shilingi milioni 650) kila mwezi. Kazi yao kuu imeainishwa kama kufanya "ushawishi (lobbying), promosheni, kusimamia mtazamo na taswira (perception management), na kusambaza taarifa." Kampuni hii inatarajiwa kuwafikia maafisa wa serikali ya Marekani, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), na vyombo vya habari vya kimataifa kwa niaba ya Tanzania.
Jambo la kutiliwa shaka zaidi ni namna mkataba huu ulivyoingiwa. Haikuwekwa wazi kupitia Balozi zetu wala michakato ya manunuzi ya Serikali inayoonekana, badala yake mkataba umesainiwa na BGR kupitia kampuni au taasisi inayoitwa Drift Advisors, SL kwa niaba ya Tanzania. Je, Drift Advisors, SL ni nani? Ni kampuni ya udalali iliyowekwa katikati ili kuficha njia za fedha (shell company)? Na imepata asilimia ngapi kwenye dili hili? Sheria na taratibu ziko wazi, zimekiukwa wazi.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama (na sasa ikiwemo hadi JWTZ) wameanza kuingia kwenye siasa badala ya kutusaidia wananchi kuwawajibisha wanasiasa ili wafuate sheria za manunuzi na uwepo uwazi katika michakato ya upatikanaji wa wazabuni.
Mazingira ya Mkataba: Kwanini Sasa?
Huwezi kutenganisha mkataba huu mnono na matukio ya giza ya hivi karibuni ya kisiasa nchini. Mnamo Desemba mwaka jana, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani (State Department) ilitangaza rasmi kuwa inafanya mapitio ya kina ya uhusiano wake na Tanzania. Hatua hiyo ilitokana na kile Serikali ya Marekani ilichokitaja kama "Ukandamizaji unaoendelea wa uhuru wa kidini na uhuru wa kujieleza," lakini kubwa zaidi, "msako mkali na ghasia zilizofuatia uchaguzi wa Oktoba 29," ambazo inadaiwa na Wamarekani zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 500.
Mnamo mwezi Aprili mwaka huu, Tume iliyoundwa na Serikali yetu kufuatia shinikizo hilo ilitoa ripoti yake na kuwatupia lawama "wachochezi wa nje" (outside agitators) kuwa ndio chanzo cha machafuko hayo ya uchaguzi.
Inaonekana wazi kuwa mkataba huu wa BGR Group umeundwa mahususi kusafisha kashfa hii. Serikali imenunua wataalamu wakongwe wa ushawishi kama kina Lester Munson, Steven Eisner, na Alex Ellis ili waiaminishe dunia na Washington kwamba simulizi ya serikali ya Tanzania ni ya kweli, na kupunguza shinikizo au vikwazo vyovyote vya kiuchumi kutoka mataifa ya magharibi.
Kama wananchi, tunaonataka kuhoji:
Fedha za umma zinapaswa kutumika kuboresha maisha ya wananchi, sio kuficha damu na makosa yanayofanywa na watawala!

- Matumizi ya Kodi zetu: Je, ni halali kwa nchi inayoendelea yenye changamoto za upatikanaji wa dawa mahospitalini, bajeti finyu ya elimu na maji safi, kutumia karibu Shilingi Bilioni 8 kwa mwaka kumlipa mzungumzaji mmoja huko Marekani ili "atusafishe" kisiasa?
- Kutibu Dalili Badala ya Ugonjwa: Badala ya kutumia mabilioni kuwalipa wasafisha taswira (PR), kwanini Serikali isitumie fedha hizo na nia hiyo njema kuunda Tume Huru za Kimahakama au kuruhusu wachunguzi wa kimataifa kuchunguza ghasia za uchaguzi, kuwawajibisha waliohusika na vifo vya raia, na kuboresha mazingira ya haki za binadamu ndani ya nchi? Matendo mema ya Serikali hujisemea yenyewe na hayasubiri kununuliwa taswira ya Dola milioni 3!
- Uwazi na Uwajibikaji wa Taasisi: Upi ulikuwa mchakato wa kuipata na kuipa zabuni BGR Group? Drift Advisors, SL inamilikiwa na nani na ina uhusiano gani na vigogo serikalini? Fedha hizi zimepitishwa kwenye Fungu lipi la bajeti ambalo Bunge lililipitisha? JWTZ mnaotuchimba mikwara wananchi, ninyi mnaujua ukweli wake?