Hii hapa taarifa Rasmi
Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri wa kibiashara na Malawi katika biashara ya bidhaa mbalimbali za kilimo. Biashara hii ya kikanda na kimataifa inaongozwa na miongozo iliyotolewa na Baraza la Afrika la Masuala ya Afya ya Mimea (IAPSC) pamoja na Mkataba wa Kimataifa wa Kulinda Mimea (IPPC), ambayo nchi zote mbili zimeridhia. Miongozo hiyo inazitaka Mamlaka za Kitaifa za Kulinda Mimea (NPPO) kusimamia uingizaji na usafirishaji wa bidhaa za kilimo, hasa kwa kuzingatia usalama wa afya ya mimea na bidhaa zinazohusiana na mimea.
Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viwatilifu Tanzania (TPHPA) ndiyo taasisi ya kitaifa inayohusika na ulinzi wa mimea nchini Tanzania. Kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Mimea Na. 4 ya mwaka 2020 (Sura ya 133) pamoja na Kanuni za Afya ya Mimea za mwaka 2023 (zilizofanyiwa marekebisho mwaka 2024), Mamlaka hii ina jukumu la kuzuia uingizaji, uanzishaji na usambazaji wa wadudu wa karantini na wadudu wa karantini wanaodhibitiwa nchini Tanzania.
Kufuatia jitihada za serikali ya Malawi kuwasiliana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa kwa zuio hilo, kwa lengo la kuanzisha na kushiriki katika mazungumzo ya kidiplomasia ili kutatua changamoto hiyo, Tanzania sasa inafutilia mbali zuio la usafirishaji na uingizaji wa bidhaa za kilimo kwenda na kutoka Malawi.
Soma Pia: Bashe apiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini kuingizwa nchini
Kwa mantiki hiyo, Tanzania inafuta rasmi zuio hilo kuanzia tarehe 25 Aprili, 2025 hadi hapo itakapotolewa taarifa nyingine, hatua inayofungua njia kwa ajili ya mazungumzo ya kidiplomasia ya ngazi ya mawaziri yatakayofanyika tarehe 2 Mei, 2025.
View attachment 3315910